Jeshi la Polisi angalieni basi la Arusha Express linalofanya safari za Arusha - Bukoba

Jeshi la Polisi angalieni basi la Arusha Express linalofanya safari za Arusha - Bukoba

kasenene

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2008
Posts
1,632
Reaction score
2,413
Wiki iliyopita nimepanda basi hili nikitokea Arusha kuelekea Kahama. Aisee hili basi linakimbia saana.

Nina wasiwasi kama limefungwa speed governor manake mwendo wake ni zaidi ya speed 100km/h hasa likiwa kwenye bara bara zisizokuwa na traffic wengi.

Kazi kwenu jeshi la polisi kabla halijachinja chinja.
 
Mambo ya wiki iliyopita unayaleta leo ulitakiwa kureport on spot

Sasa wakisema umetumwa kuharibu biashara za watu una utetezi?
 
Kwa msaada zaidi siku nyingine jaribu basi lisilokua na mwendo na sijui utalipata wapi maana chombo cha usafiri kimeundiwa mwendo
 
Nilimeisha shauri humu lianzishwe jukwaa la usalama barabarani. Ili watu waweke kwenye jukwaa hilo kero, pongezi na mengineyo juu ya usalama barabarani. Nina imani hata mkuu wa usalama barabarani nchini atakuwa anawahi kuangalia kwenye jukwaa hilo na kuchukua hatua. Nadhani moderators bado wanafanyia kazi ushauri wangu.
Watanzania kwenye kushauri hamjambo.

Na ushauri wenu usipofatwa mnawaka.
 
Kaz ya gari ni kukimbia , kazi ya dereva ni kulikimbiza , je kaz ya traffic ni kulifanyaje?
 
Laumu serikali yako kuwa na miundo mbinu mibovu sio kukimbia kwa basi
 
Unaweza kuta haujala hata chakula umekimbilia kuwalaumu Arusha Express
 
Wiki iliyopita nimepanda basi hili nikitokea Arusha kuelekea Kahama. Aisee hili basi linakimbia saana.

Nina wasiwasi kama limefungwa speed governor manake mwendo wake ni zaidi ya speed 100km/h hasa likiwa kwenye bara bara zisizokuwa na traffic wengi.

Kazi kwgeshjeshi la polisi kabla halijachinja chinja.
Wewe hukuwa na GPS track ya kugundua speed ya gari unatumia hisia tu kuleta matatizo siku mabasi yakikosekana utasafiri na punda?
 
Mkuu kapande Sauli au Golden Dear za Dar Mbeya utaomba hao Arusha Express waongeze Speed.
 
Comments za baadhi ya watu humu kwa kweli zinasikitisha sana.......

Kweli milembe wanapelekwa wazima vichaa wanaachwa tunaishi nao mitaani.......

Yaani mtu anatoa taarifa ambayo ikifanyiwa kazi inaweza kuokoa maisha na mali za watu lakini kuna baadhi ya Wana mbeza na kumzodoa......ndugu zangu tunaelekea wapi.........
 
Mambo ya wiki iliyopita unayaleta leo ulitakiwa kureport on spot

Sasa wakisema umetumwa kuharibu biashara za watu una utetezi?
sikuwa nimepata mda wa kuingia online..arafu mabasi ya mikoni inaonekana hayana number simu za polisi kama yalivyo mabasi ya barabara kuu na ndio yanaua saana....sio kila andiko lazima kucomment wakati mwingine kukaa kimya ni busara zaidi
 
Nilimeisha shauri humu lianzishwe jukwaa la usalama barabarani. Ili watu waweke kwenye jukwaa hilo kero, pongezi na mengineyo juu ya usalama barabarani. Nina imani hata mkuu wa usalama barabarani nchini atakuwa anawahi kuangalia kwenye jukwaa hilo na kuchukua hatua. Nadhani moderators bado wanafanyia kazi ushauri wangu.
Nami pia nawaomba wafanyie kazi wazo hili na tena lianzishwe mapema sana litasaidia saana kwa kiasi fulani na kuokoa maisha ya watu na kadhia mbalimbali za wasafiri.
 
Comments za baadhi ya watu humu kwa kweli zinasikitisha sana.......

Kweli milembe wanapelekwa wazima vichaa wanaachwa tunaishi nao mitaani.......

Yaani mtu anatoa taarifa ambayo ikifanyiwa kazi inaweza kuokoa maisha na mali za watu lakini kuna baadhi ya Wana mbeza na kumzodoa......ndugu zangu tunaelekea wapi.........
Anatolea sehemu husika? Ana ushahidi au kuchafua tu biashara ya watu?
 
Anatolea sehemu husika? Ana ushahidi au kuchafua tu biashara ya watu?
Inawezekana isiwe sehemu husika lakini ikawa ndio chanzo Cha kufika sehemu husika......kimsingi suala linalohusisha maisha na mali za watu ni suala nyeti......wewe unajua sehemu husika sio vibaya kuzipeleka kwani utakuwa umetimiza wajibu wako kama raia mwema.......

Ajali zimesababisha madhara makubwa kwenye familia na taifa kwa ujumla hivyo basi hatupaswi hata kupuuzia taarifa za viashiria vya ajali........
 
Back
Top Bottom