Jeshi la polisi Arusha linachunguza kifo cha Raia wa Rwanda anayeelezwa kujinyonga akiwa mahabusu

Jeshi la polisi Arusha linachunguza kifo cha Raia wa Rwanda anayeelezwa kujinyonga akiwa mahabusu

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Jeshi la polisi limesema linafanya uchunguzi kifo cha Viollete Uwumuhoza, raia wa Rwanda, aliyefariki tarehe 7 Januari, 2026 ikielezwa kuwa ni baada ya kujinyonga akiwa mahabusu katika kituo cha Polisi Jijini Arusha, alikokuwa akishikiliwa kwa kosa la kuingia na kuishi nchini kinyume cha sheria.

Polisi wamesema uchunguzi wa haraka na wa kisayansi unaendelea ili kubaini mazingira kamili ya tukio hilo.
 
Mumemnyonga mtu wa Kagame?

Mwanakulitafuta mwanakulipata
 
Jeshi la polisi limesema linafanya uchunguzi kifo cha Viollete Uwumuhoza, raia wa Rwanda, aliyefariki tarehe 7 Januari, 2026 baada ya kujinyonga akiwa mahabusu katika kituo cha Polisi Jijini Arusha, alikokuwa akishikiliwa kwa kosa la kuingia na kuishi nchini kinyume cha sheria. Polisi wamesema uchunguzi wa haraka na wa kisayansi unaendelea ili kubaini mazingira kamili ya tukio hilo.
okey
 
asijekuwa alikuwa JASUSI nimewaza tu sinauhakika.
 
Drama baada ya drama.Zitaisha lini?Ajinyonge tu mtu aliyetoka mbali kuja kutafuta maisha!?Kuna jambo hapo.Aidha alikuwa na mali/fedha nyingi na kuporwa/kudhilumiwa,kuteswa sana au kuuliwa na hao majambazi waliomkamata.Hawaaminiki.
 
Mambo kama haya, kwa jinsi jeshi la Polisi linavhofanya kazi, litakuja kusababisha vita na majirani zetu.

Kwanza inakuwaje raia wa Afrika Mashariki, eti aliingia kinyume cha sheria! Afadhali angrkuwa na kosa la jinai, lakini siyo kosa la kuingia nchini. Raia wa Afrika Mashariki kuingia nchi yoyote ya Afrika Mashariki hahitaji passport, wala visa. Anatakiwa tu kuwa na national ID.
 
Jeshi la polisi limesema linafanya uchunguzi kifo cha Viollete Uwumuhoza, raia wa Rwanda, aliyefariki tarehe 7 Januari, 2026 baada ya kujinyonga akiwa mahabusu katika kituo cha Polisi Jijini Arusha, alikokuwa akishikiliwa kwa kosa la kuingia na kuishi nchini kinyume cha sheria. Polisi wamesema uchunguzi wa haraka na wa kisayansi unaendelea ili kubaini mazingira kamili ya tukio hilo.
Hakujinyonga, amenyongwa. Story hizi ni za kila leo ndani ya jeshi la polisi!
 
Usikute wamemfanyia vitendo vya ukatili na udhalilishaji! Ili kuficha uovu wao, wakaamua kumuua! Hakika tuna watu wa ajabu sana kwenye hilo jeshi.

Inawezekana vipi mtu ajinyonge kirahisi tu akiwa chini ya ulinzi wao? Hivi hawa watu wataacha lini maigizo, na pia kujipa mamlaka ya kuondoa uhai wa binadamu anayelindwa na sheria kibao tu za Kimataifa?
 
Back
Top Bottom