Jeshi la Polisi: Hakuna ushahidi kuwa Freeman Mbowe alishambuliwa. Alikuwa ametoka kwa Joyce Mukya. Alikuwa amelewa chakari

Polisi bana wamewahoji watu waliokuwa karibu hawakusikia kelele yoyote du. Je hao watu walimuona Mbowe akianguka peke yake na mbona hakumpa msaada? Inatia shaka sana tunakuwa na ubaguzi wa namna hii kwenye jeshi letu na polisi.yanayoendelea Marekani ni mambo kama haya unakuja na vitu havina mantiki kwenye maswala ya kiuchunguzi.
 
Ungejifunza kwanza kuandika vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema ilijengwa kwa ghilba,uongo na uchonganishi
Mungu fundi sana,safari hii wamepata aibu ya mwaka
 

 
Mnavyomtafuta mtatoa ripoti zaidi ya hiyo? Chuki ya wazi kwake mliyonayo hatuoni ajabu!
Lijamaa linakunywa vinywaji Vikali sana wakati umri wake umeenda sana.
Likishauliwa kupunguza mvinyo mkali nasikia linakuwa mbogho.
 
Mimi nimeandika kiswahili na hiyo ni typing error. Tofautisha na makosa ya mtoa mada. Naomba niishie hapo. Binadamu ndio nilimaanisha.
Hacha kujifanya mwalimu wa mwndiko pata concept sepa mwandiko fata nyumbani kwako kwa mkeo
 
Safi good analysis safi sanaAaa.
 
Hapa tu ndio penye kila kitu. Sasa nazidi kupata shaka na huu ushahidi wa kuzunguka wakati kuna CCTV Cameras, na Bado hazitumiki kwenye ushahidi wa tukio hili!
Mkuu inaonekana umesoma na mihemuko hii taarifa ya uchunguzi,, Kama unajua kuchambua Mambo ya kiitelinjesia utagundua kuwa hata CCTV cameras zimetumika katika kukamilisha ushahidi.

Nanukuu aya kutoka kwenye hiyo ripot inayoosha Msaada wa CCTV cameras Kama ifuatavyo;
"Ameongeza upelelezi wao umepata ushahidi kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa" mwisho wa kunukuu.

Swali je hao wapepelezi Waliona vipi Kama kulikuwa na watu Kama siyo CCTV cameras??
Tujitahidi kusoma kwa utulivu na kuelewa.
 
Kwa kipindi kirefu jeshi la polisi limekuwa ni wazito wa kutoa ripoti zao kwa wakati na siku zote husema uchunguzi unaendelea,
Lakini hii kwa mara ya kwanza wameweza kutoa taarifa ya uchunguzi juu ya ya tukio la mwenyekiti wa chadema aliyekuwa ameumia mguu na kudaiwa kuvamiwa na watu wasiojulikana,
Lakini safari kwa muda mfupi na kutumia weledi wa kazi,wamekusanya ushahidi fasta na kutoa ripoti yao kuwa chairman alikuwa tilalila maji yalizidi unga.

Nina hakika hata tukio la lissu angetoa ushirikiano yeye na dereva wake ripoti ya uchunguzi ingekuwa imeshakamilika bila shinikizo wala mizengwe!
Kidogo kidogo wanaanza kubadilika wakifanya vizuri wapongezwe wakifanya vibaya wakosolewe!
 
Sasa watu wanaomtegemea meko awape mkate unategemea watakuwa na akili kichwani!? Bado kufungua kanisa na kumuabudu tu.
 
Umesoma taarifa yote ya uchunguzi ukakuta CCTV cameras hazijahusika kukamilisha uchunguzi? Au ndo kusoma habari kwa mihemuko ya kisiasa..
Kama unajua kuchambua taarifa za kiitelinjesia utaelewa kuwa CCTV kamara zilitumika Ila Kama kichwa chako nikwa ajili ya kufugia nywele pekee utaendelea kuuliza CCTV camera mpaka Mh Mbowe na Joyce wanapata mtoto.

"Ameongeza upelelezi wao umepata ushahidi kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa" Msemaji wa jeshi la polisi.
 
Kama mahakama ni hizi za "kangaroo" hauna nguvu.G.Floyd kaliamusha dude duniani sabau ya ushahidi huo.
 
Haiwezekani Siku moja moja mkawa na afya njema ya akili?
 
ni aibu sana kwa IGP
Maisha yanenda kasi sana, juzi inaonekana kama miaka 200 nyuma.
Unafiki unawaponza sana watu wa vyama.
Nakumbuka, baada ya kutokea tukio la kushambuliwa kwa Mwamba, wafuasi wa ccm kwenye mitandao walitamani sana footage za cctv zitolewe, hili lilikumbana na upinzani mkali kutoka waandamanaji wa mitandaoni wa cdm ukiwamo wewe mkuu. Leo, polisi wametoa taarifa ya uchunguzi wa awali na kuonyesha mwamba aliteleza, cdm wanataka cctv zitumike na waropokaji wa ccm hawataki.
Mkiacha umalaya wenu wa kisiasa hii nchi itaenda mbele.
Kwa utu wa kila mmoja hata km akiwa mlevi au muuaji, akishambuliwa au kajiumiza, kitu huruma ni muhimu sana. Uongo haujengi wala majivuno si uugwana.
Tujifunze kuwa wa kweli daima maana itatuweka huru. Na sio ushabiki maandazi km mnavyofanya nyie, wewe ukiwemo.
 
CCTV ndoushahidi uliokuwepo mbashara kuhoji majilani sijambo baya lakini ule niusiku huwenda kutokusikia kwao nisahihi labda walilala lakini mtu pekee ambaye hakulala ni CCTV labda Kama hakuwepo eneo la tukio huyu ndiye shahidi namba moja mbona hajahojiwa?
 
Kwa hiyo huyu aliyetoa hii taarifa naye ni afisa wa jeshi? Amesoma? Au alipewa tu hiyo kazi? Kwa nini afisa mzima atolee taarifa kitu asicho na uhakika nacho? Unaposema alionekana amelewa una maana gani? Si useme tu kwamba vipimo vilionyesha amelewa. Maana aliyelewa akipimwa vipimo huthibitisha hivyo. Taarifa rasmi haipaswi kuwa ya kudhani kama hii. Kitaalamu kama una dhanio (Hypothesis) hutolei dhania kwenye taarifa rasmi, bali unalifanyia utafiti dhanio hilo kuona kama lina uthibitisho wowote wa kitaalamu. Kama mtu kauawa ukawa una dhanio kwamba ni mtu X kahusika, huendi hadharani kusema tunadhani aliyemuua ni X, bali unachunguza kuona kama dhanio lako lina ukweli. Sasa unasemaje kwa umma kwamba alionekana amelewa maana alikuwa anashindwa hata kutamka baadhi ya maneno. Kwani kila mgonjwa au hata asiye mgonjwa akiwa anashindwa kutamka maneno anakuwa amelewa?

Hii taarifa ni kama imeandikwa na mtu aliyeishia chakechea ya kijijini.

Angalia AYA ya mwisho inavyopingana na yote yaliyotolewa taarifa mwanzo wa taarifa. Eti anamalizia kwa kusema "tunaendelea na uchunguzi kutafuta ukweli wa tukio hili". Ina maana ulichokitolea taarifa hakina ukweli? Ukisha upate huo ukweli utakuja kukanusha ulichokitolea taarifa mwanzo? Ni Afisa gani wa serikali hii ana huo ujasiri wa kuja kukanusa au kusahihisha alichokisema mwanzo?

Hii inanikumbusha kwenye sakata la mapapai ya korona. Mtu mmoja alishatoa majibu na kuwatumbua watu kwamba wamekosea, halafu mtu mwingine anaunda tume akafanye utafiti kama alichokisema mkubwa ni cha kweli. Walituletea matokeo ambayo tayari tulikuwa nayo. Huwezi kwenda kinyume na alichokisema mkubwa. Spika alishasema Mbowe hakuvamiwa ila alianguka baada ya kulewa. Nani alikuwa na matumaini ya Polisi kuleta taarifa tofauti na spika ambaye alikuwa ni Spika tu wa Jiwe. Yale aliyoyasema Spika alipata toka kwa Jiwe. Wote lao moja.
 
Sasa hiyo AYA ya mwisho wewe umeielewaje?
 
Sasa tushike lipi? Sasa huyu Joyce Nkya ni nani tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…