Jeshi la Polisi: Hakuna ushahidi kuwa Freeman Mbowe alishambuliwa. Alikuwa ametoka kwa Joyce Mukya. Alikuwa amelewa chakari

Jeshi la Polisi: Hakuna ushahidi kuwa Freeman Mbowe alishambuliwa. Alikuwa ametoka kwa Joyce Mukya. Alikuwa amelewa chakari

Polisi bana wamewahoji watu waliokuwa karibu hawakusikia kelele yoyote du. Je hao watu walimuona Mbowe akianguka peke yake na mbona hakumpa msaada? Inatia shaka sana tunakuwa na ubaguzi wa namna hii kwenye jeshi letu na polisi.yanayoendelea Marekani ni mambo kama haya unakuja na vitu havina mantiki kwenye maswala ya kiuchunguzi.
 
Ndugu wana jamvi habali za asubuhi?

Niingie kwenye mada,
Nionavyo mimi ni.kwamba hii ajari ya mh mbowe kwa sasa anaijutia na pengine kwa kuwapa mamlaka vijana wake amabao ni special kutoa na kufanya maamuzi juu ya chama kwa ruhusa yake.
Nasema hivyo kwa sababu gani? Kama mh mbowe angekuwa na utambuzi mzuri nadhani asingekubali hiyo ajali ihusishwe kisiasa kwa kuwa ni jamabo amabalo lingeripotiwa kawaida lisingempa wakati mgumu kama alionao sasa kujibu hoja nyingi ambazo zisinge kuwapo.

Kulingana na taarifa ya police kuwa alikuwa amelewa chakali na pia DR wa Ngugai kusema hivyo, inatosha kusema kauli za watu wasiojulikana ziliasisiwa na vijana wake bila kumshirikisha na kujua uzito wa maamuzi yao.
kwa hiyo baada ya kupata utambuzi tayari mambo yalikuwa yamerushwa hewani kwa hiyo hakuwa na namna.
Wangeripoti kuwa amepata ajari baada ya kuwa anatoka kunywa kinywaji wala pasingekuwa na challenge nyingi kwani hilo ni jambo la kawaida tu.
Nimuombe mbowe apunguze nguvu ya hawa vijana wake ili kutunza heshima yake na chama chake.
Maaana kwa sasa hata ambaye alikuwa hajui kuwa mbowe ana mchepuka sasa kajua, na hao mabalozi wake sasa watajua kuwa malalamiko ya wabunge kuombwa mapenzi ni ya ukweli maana tayali kianzio kipo.
Pole sana Mr F Mbowe.
Ungejifunza kwanza kuandika vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema ilijengwa kwa ghilba,uongo na uchonganishi
Mungu fundi sana,safari hii wamepata aibu ya mwaka
 
View attachment 1476358View attachment 1476359
USHAHIDI wa awali wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu madai ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe umeonesh kuwa siku hiyo ya tukio Mbowe alikuwa amelewa chakali na alizunguka kwenye kumbi mbalimbali za starehe zinazouza vileo ikiwemo ya Royal Village.

Pia ushahidi huo unaonesha mbali ya kuwa kwenye maeneo hayo ya starehe alikuwa nyumbani kwa mzazi mwenzake Joyce Nkya ambaye ni Mbunge wa Viti Maaluma Chadema na kwamba hata taarifa za kwamba ameshambuliwa zinatia shaka kwani mashahidi wote ambao wameojiwa hakuna anayethibitisha uwepo wa tukio hilo zaidi ya Mbowe mwenyewe na dereva wake.

Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Jeshi hilo David Misime amesema Juni 9 mwaka huu walitoa taarifa ya awali kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Mroto kuhusu tukio la lililoripotiwa kuwa Mbowe amelezwa jijini Dodoma kwa kile kilichodaiwa kushambuliwa wakati anaingia nyumbani kwake .

Misime amesema baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo ya awali wamekuwa wakipokea simu nyingi kutoka kwa waandishi wa habari wakitaka kufahamu matokeo ya uchunguzi kuhusu taarifa iliyofikishwa Kituo cha Polisi Kati Dodoma.

"Napenda kujulisha kuwa Jeshi la Polisi limeendelea kufanya upelelezi wa kina kuanzia kwa mhanga mwenyewe wa tukio ambaye alidai kuwa muda wa saa saba hivi usiku akiwa kwenye ngazi ya kuingia nyumbani kwake akiwa na anatoka kwa mzazi mwenzake aitwaye Joyce Nkya ambaye ni Mbunge wa Viti Maaluma Chadema anayeishi eneo la Medeli Mjini Ddoma alishambuliwa na kuumia kwenye mguu wa kulia.

"Mhanga wa tukio hilo alidai wakati anashambuliwa alipiga kelele nyingi kuomba msaada ambao aliupata kutoka kwa dereva wake ambaye naye alipiga simu kwa Joyce Nkya kisha hospitali iliyoko takribani umbali wa kilometa tano nje ya Jiji la Dodoma pasipo umuhimu wa kutoa taarifa Polisi kabla ya kwenda kwa Joyce Nkya na Hospitali,"amesema Misime.

Ameongeza upelelezi wao umepata ushahidi kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa .

"Hata hivyo kwa mujibu wa wa mashahidi hawa hakuna hata mmoja aliyeweza kusikia kelele hizo au kuona mbowe akishambuliwa. Kwa mantikini hiyo ushahidi pekee unaozumngumzia kushambuliwa ni maelezo ya mhanga wa tukio(Mbowe) pamoja na dereva wake.

"Ambayo kwa hali ilivyo sasa yanatia shaka kuhusu ukweli wa tukio hili.Mashaka hayo yanaongezeka zaidi pale tulipobaini kuwa nyumbani kwa Mbowe alikuwepo kijana wake aitwaje James Mbowe ambaye hawakuona umuhimu wa kumjulisha kuhusu tukio lililotokea hapo nyumbani badala yake waliona umuhimu wa kumjulisha Jocye Nkya aliyekuwa mbali na eneo la tukio,"amesema.

Pia amesema uchunguzi wa Jeshi la Polisi nchini umethibitisha kuwa siku ya Juni 8 mwaka huu Mbowe alitembelea sehemu kadhaa za starehe zinazouza vileo ikiwepo ya Royal Village na kupata kinywaji.

"Hata hivyo alipofika hospitali alioneana akiwa katika hali ya ulevi chakari kiasi cha kushindwa kutamka maneno sawa sawa.Tunaendelea na uchunguzi kutafuta ukweli wa tukio hili, hivyo tunaomba wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia upelelezi huo wazilete kwetu. Tutaendelea kutoa taarifa kwenu kadri ushahidi utakavyopatikana,"amesema Misime kupitia taarifa ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari.

Pia soma

> News Alert: - Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

> Freeman Mbowe na Joyce Mukya wamtumia Mjomba wa Mtoto kupata cheti cha kuzaliwa

> Mhe. Mbowe na Mhe. Joyce Mukya mtafanya hili suala kuwa siri mpaka lini?

> Joyce Mukya ni nani? Pamoja na kutokuwa active kwenye Siasa bado anapeta ubunge CHADEMA zaidi ya miaka 10

Mnavyomtafuta mtatoa ripoti zaidi ya hiyo? Chuki ya wazi kwake mliyonayo hatuoni ajabu!
Lijamaa linakunywa vinywaji Vikali sana wakati umri wake umeenda sana.
Likishauliwa kupunguza mvinyo mkali nasikia linakuwa mbogho.
 
Mimi nimeandika kiswahili na hiyo ni typing error. Tofautisha na makosa ya mtoa mada. Naomba niishie hapo. Binadamu ndio nilimaanisha.
Hacha kujifanya mwalimu wa mwndiko pata concept sepa mwandiko fata nyumbani kwako kwa mkeo
 
Ile press conference haikuwa na mantiki hata kidogo maana hakuna la maana alilosema. ajathibitisha kama mbowe alianguka kwa ulevi, hajathibitisha kama alipigwa.
Assume ni kweli alikuwa kalewa, is it a crime kunywa pombe Tanzania? Assume alikuwa kumbi za starehe kama alivyosema is it a crime?
Yani ile alifanya makusudi kuwafurahisha akina Ndungai badala ya kutoa maelezo ya kujitosheleza. Sema ndiyo hivyo watanzania wengi wanaamini wanachokisikia.
Safi good analysis safi sanaAaa.
 
Hapa tu ndio penye kila kitu. Sasa nazidi kupata shaka na huu ushahidi wa kuzunguka wakati kuna CCTV Cameras, na Bado hazitumiki kwenye ushahidi wa tukio hili!
Mkuu inaonekana umesoma na mihemuko hii taarifa ya uchunguzi,, Kama unajua kuchambua Mambo ya kiitelinjesia utagundua kuwa hata CCTV cameras zimetumika katika kukamilisha ushahidi.

Nanukuu aya kutoka kwenye hiyo ripot inayoosha Msaada wa CCTV cameras Kama ifuatavyo;
"Ameongeza upelelezi wao umepata ushahidi kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa" mwisho wa kunukuu.

Swali je hao wapepelezi Waliona vipi Kama kulikuwa na watu Kama siyo CCTV cameras??
Tujitahidi kusoma kwa utulivu na kuelewa.
 
Kwa kipindi kirefu jeshi la polisi limekuwa ni wazito wa kutoa ripoti zao kwa wakati na siku zote husema uchunguzi unaendelea,
Lakini hii kwa mara ya kwanza wameweza kutoa taarifa ya uchunguzi juu ya ya tukio la mwenyekiti wa chadema aliyekuwa ameumia mguu na kudaiwa kuvamiwa na watu wasiojulikana,
Lakini safari kwa muda mfupi na kutumia weledi wa kazi,wamekusanya ushahidi fasta na kutoa ripoti yao kuwa chairman alikuwa tilalila maji yalizidi unga.

Nina hakika hata tukio la lissu angetoa ushirikiano yeye na dereva wake ripoti ya uchunguzi ingekuwa imeshakamilika bila shinikizo wala mizengwe!
Kidogo kidogo wanaanza kubadilika wakifanya vizuri wapongezwe wakifanya vibaya wakosolewe!
 
Sasa watu wanaomtegemea meko awape mkate unategemea watakuwa na akili kichwani!? Bado kufungua kanisa na kumuabudu tu.
 
Umesoma taarifa yote ya uchunguzi ukakuta CCTV cameras hazijahusika kukamilisha uchunguzi? Au ndo kusoma habari kwa mihemuko ya kisiasa..
Kama unajua kuchambua taarifa za kiitelinjesia utaelewa kuwa CCTV kamara zilitumika Ila Kama kichwa chako nikwa ajili ya kufugia nywele pekee utaendelea kuuliza CCTV camera mpaka Mh Mbowe na Joyce wanapata mtoto.

"Ameongeza upelelezi wao umepata ushahidi kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa" Msemaji wa jeshi la polisi.
 
Just go with a technologies? Bora uwe unaandika kiswahili tu. Alafu kwa akili yako kati ya ushahidi wa binadamu na Cctv video footage upi una nguvu mahakani? Maana Cctv video footage lazima wataalamu waje wathibitishe kitalaamu kama kweli mlevi anadondoka. Binadamu mwenye akili timamu ana sense kwa sensory organs na anatoa direct evidence.Kama hawakusikia mtu akishambuliwa Cctv ndio zitarekodi?
Kama mahakama ni hizi za "kangaroo" hauna nguvu.G.Floyd kaliamusha dude duniani sabau ya ushahidi huo.
 
Just go with a technologies? Bora uwe unaandika kiswahili tu. Alafu kwa akili yako kati ya ushahidi wa binadamu na Cctv video footage upi una nguvu mahakani? Maana Cctv video footage lazima wataalamu waje wathibitishe kitalaamu kama kweli mlevi anadondoka. Binadamu mwenye akili timamu ana sense kwa sensory organs na anatoa direct evidence.Kama hawakusikia mtu akishambuliwa Cctv ndio zitarekodi?
Haiwezekani Siku moja moja mkawa na afya njema ya akili?
 
ni aibu sana kwa IGP
Maisha yanenda kasi sana, juzi inaonekana kama miaka 200 nyuma.
Unafiki unawaponza sana watu wa vyama.
Nakumbuka, baada ya kutokea tukio la kushambuliwa kwa Mwamba, wafuasi wa ccm kwenye mitandao walitamani sana footage za cctv zitolewe, hili lilikumbana na upinzani mkali kutoka waandamanaji wa mitandaoni wa cdm ukiwamo wewe mkuu. Leo, polisi wametoa taarifa ya uchunguzi wa awali na kuonyesha mwamba aliteleza, cdm wanataka cctv zitumike na waropokaji wa ccm hawataki.
Mkiacha umalaya wenu wa kisiasa hii nchi itaenda mbele.
Kwa utu wa kila mmoja hata km akiwa mlevi au muuaji, akishambuliwa au kajiumiza, kitu huruma ni muhimu sana. Uongo haujengi wala majivuno si uugwana.
Tujifunze kuwa wa kweli daima maana itatuweka huru. Na sio ushabiki maandazi km mnavyofanya nyie, wewe ukiwemo.
 
CCTV ndoushahidi uliokuwepo mbashara kuhoji majilani sijambo baya lakini ule niusiku huwenda kutokusikia kwao nisahihi labda walilala lakini mtu pekee ambaye hakulala ni CCTV labda Kama hakuwepo eneo la tukio huyu ndiye shahidi namba moja mbona hajahojiwa?
 
View attachment 1476358View attachment 1476359
USHAHIDI wa awali wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu madai ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe umeonesh kuwa siku hiyo ya tukio Mbowe alikuwa amelewa chakali na alizunguka kwenye kumbi mbalimbali za starehe zinazouza vileo ikiwemo ya Royal Village.

Pia ushahidi huo unaonesha mbali ya kuwa kwenye maeneo hayo ya starehe alikuwa nyumbani kwa mzazi mwenzake Joyce Nkya ambaye ni Mbunge wa Viti Maaluma Chadema na kwamba hata taarifa za kwamba ameshambuliwa zinatia shaka kwani mashahidi wote ambao wameojiwa hakuna anayethibitisha uwepo wa tukio hilo zaidi ya Mbowe mwenyewe na dereva wake.

Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Jeshi hilo David Misime amesema Juni 9 mwaka huu walitoa taarifa ya awali kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Mroto kuhusu tukio la lililoripotiwa kuwa Mbowe amelezwa jijini Dodoma kwa kile kilichodaiwa kushambuliwa wakati anaingia nyumbani kwake .

Misime amesema baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo ya awali wamekuwa wakipokea simu nyingi kutoka kwa waandishi wa habari wakitaka kufahamu matokeo ya uchunguzi kuhusu taarifa iliyofikishwa Kituo cha Polisi Kati Dodoma.

"Napenda kujulisha kuwa Jeshi la Polisi limeendelea kufanya upelelezi wa kina kuanzia kwa mhanga mwenyewe wa tukio ambaye alidai kuwa muda wa saa saba hivi usiku akiwa kwenye ngazi ya kuingia nyumbani kwake akiwa na anatoka kwa mzazi mwenzake aitwaye Joyce Nkya ambaye ni Mbunge wa Viti Maaluma Chadema anayeishi eneo la Medeli Mjini Ddoma alishambuliwa na kuumia kwenye mguu wa kulia.

"Mhanga wa tukio hilo alidai wakati anashambuliwa alipiga kelele nyingi kuomba msaada ambao aliupata kutoka kwa dereva wake ambaye naye alipiga simu kwa Joyce Nkya kisha hospitali iliyoko takribani umbali wa kilometa tano nje ya Jiji la Dodoma pasipo umuhimu wa kutoa taarifa Polisi kabla ya kwenda kwa Joyce Nkya na Hospitali,"amesema Misime.

Ameongeza upelelezi wao umepata ushahidi kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa .

"Hata hivyo kwa mujibu wa wa mashahidi hawa hakuna hata mmoja aliyeweza kusikia kelele hizo au kuona mbowe akishambuliwa. Kwa mantikini hiyo ushahidi pekee unaozumngumzia kushambuliwa ni maelezo ya mhanga wa tukio(Mbowe) pamoja na dereva wake.

"Ambayo kwa hali ilivyo sasa yanatia shaka kuhusu ukweli wa tukio hili.Mashaka hayo yanaongezeka zaidi pale tulipobaini kuwa nyumbani kwa Mbowe alikuwepo kijana wake aitwaje James Mbowe ambaye hawakuona umuhimu wa kumjulisha kuhusu tukio lililotokea hapo nyumbani badala yake waliona umuhimu wa kumjulisha Jocye Nkya aliyekuwa mbali na eneo la tukio,"amesema.

Pia amesema uchunguzi wa Jeshi la Polisi nchini umethibitisha kuwa siku ya Juni 8 mwaka huu Mbowe alitembelea sehemu kadhaa za starehe zinazouza vileo ikiwepo ya Royal Village na kupata kinywaji.

"Hata hivyo alipofika hospitali alioneana akiwa katika hali ya ulevi chakari kiasi cha kushindwa kutamka maneno sawa sawa.Tunaendelea na uchunguzi kutafuta ukweli wa tukio hili, hivyo tunaomba wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia upelelezi huo wazilete kwetu. Tutaendelea kutoa taarifa kwenu kadri ushahidi utakavyopatikana,"amesema Misime kupitia taarifa ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari.

Pia soma

> News Alert: - Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

> Freeman Mbowe na Joyce Mukya wamtumia Mjomba wa Mtoto kupata cheti cha kuzaliwa

> Mhe. Mbowe na Mhe. Joyce Mukya mtafanya hili suala kuwa siri mpaka lini?

> Joyce Mukya ni nani? Pamoja na kutokuwa active kwenye Siasa bado anapeta ubunge CHADEMA zaidi ya miaka 10

Kwa hiyo huyu aliyetoa hii taarifa naye ni afisa wa jeshi? Amesoma? Au alipewa tu hiyo kazi? Kwa nini afisa mzima atolee taarifa kitu asicho na uhakika nacho? Unaposema alionekana amelewa una maana gani? Si useme tu kwamba vipimo vilionyesha amelewa. Maana aliyelewa akipimwa vipimo huthibitisha hivyo. Taarifa rasmi haipaswi kuwa ya kudhani kama hii. Kitaalamu kama una dhanio (Hypothesis) hutolei dhania kwenye taarifa rasmi, bali unalifanyia utafiti dhanio hilo kuona kama lina uthibitisho wowote wa kitaalamu. Kama mtu kauawa ukawa una dhanio kwamba ni mtu X kahusika, huendi hadharani kusema tunadhani aliyemuua ni X, bali unachunguza kuona kama dhanio lako lina ukweli. Sasa unasemaje kwa umma kwamba alionekana amelewa maana alikuwa anashindwa hata kutamka baadhi ya maneno. Kwani kila mgonjwa au hata asiye mgonjwa akiwa anashindwa kutamka maneno anakuwa amelewa?

Hii taarifa ni kama imeandikwa na mtu aliyeishia chakechea ya kijijini.

Angalia AYA ya mwisho inavyopingana na yote yaliyotolewa taarifa mwanzo wa taarifa. Eti anamalizia kwa kusema "tunaendelea na uchunguzi kutafuta ukweli wa tukio hili". Ina maana ulichokitolea taarifa hakina ukweli? Ukisha upate huo ukweli utakuja kukanusha ulichokitolea taarifa mwanzo? Ni Afisa gani wa serikali hii ana huo ujasiri wa kuja kukanusa au kusahihisha alichokisema mwanzo?

Hii inanikumbusha kwenye sakata la mapapai ya korona. Mtu mmoja alishatoa majibu na kuwatumbua watu kwamba wamekosea, halafu mtu mwingine anaunda tume akafanye utafiti kama alichokisema mkubwa ni cha kweli. Walituletea matokeo ambayo tayari tulikuwa nayo. Huwezi kwenda kinyume na alichokisema mkubwa. Spika alishasema Mbowe hakuvamiwa ila alianguka baada ya kulewa. Nani alikuwa na matumaini ya Polisi kuleta taarifa tofauti na spika ambaye alikuwa ni Spika tu wa Jiwe. Yale aliyoyasema Spika alipata toka kwa Jiwe. Wote lao moja.
 
Umesoma taarifa yote ya uchunguzi ukakuta CCTV cameras hazijahusika kukamilisha uchunguzi? Au ndo kusoma habari kwa mihemuko ya kisiasa..
Kama unajua kuchambua taarifa za kiitelinjesia utaelewa kuwa CCTV kamara zilitumika Ila Kama kichwa chako nikwa ajili ya kufugia nywele pekee utaendelea kuuliza CCTV camera mpaka Mh Mbowe na Joyce wanapata mtoto.

"Ameongeza upelelezi wao umepata ushahidi kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa" Msemaji wa jeshi la polisi.
Sasa hiyo AYA ya mwisho wewe umeielewaje?
 
Sasa tushike lipi? Sasa huyu Joyce Nkya ni nani tena?
 
Back
Top Bottom