Jeshi la Polisi: Hakuna ushahidi kuwa Freeman Mbowe alishambuliwa. Alikuwa ametoka kwa Joyce Mukya. Alikuwa amelewa chakari

Jeshi la Polisi: Hakuna ushahidi kuwa Freeman Mbowe alishambuliwa. Alikuwa ametoka kwa Joyce Mukya. Alikuwa amelewa chakari

Haya Sasa mambo wazi kabisa ni aibu hii kwa chadema kusema uongo sijui wataficha wapi sura zao chadema [emoji23][emoji1787][emoji2960]
Hata Balozi za USA, UK, na EU walipokimbilia kutoa matamko kumbe tatizo ni ulevi na ufusika. Sasa sijui wataficha wapi sura zao. Shame on them!!
 
Kwa taarifa yako CCTV footage zinasema ukweli kuliko Polisi, Mbowe, mtoto wake na mwingine awaye yote. Kwa hapa tulipo wote wenye akili timamu tunangoja tu ukweli wa CCTV footage, na sio maelezo ya polisi, Mbowe, mtoto wa Mbogwe, kimada Mbowe au nani.

NB: ukitaka kujua watu wamepuuza bajeti, angalia watakaichangia kwenye uzi huu, na wale waliochangia kwenye bajeti.

Cc:
Kamanda umepanic Hahahahahah
 
Umesahau pia kuwa kuna vipimo vya hospitali km X-Ray za kuthibitisha aina na kiwango cha majeraha alityopata Mbowe, Kamanda Mkuu, au navyo vitafichwa?

Mkuu huko kwenye ushahidi unaotegemewa utashi wa binadamu, ukweli unaweza kupindishwa, CCTV footage zikiwekwa wazi ukweli wote utakupatikana. Hilo ni rahisi sana.
 
Jijibu ni kwamba hana access na control room ya CCTV, zile zimewekwa na maafisa hivyo wenye access ni hao hao maafisa, sio kila mtu ndiyo maana cctv za kwa lissu 'zitolewa' jiulize nani aliyeondoa hizo cctv?
Haya ya kutoa CCTV nani aliyasema?
 
Bac ukijua polisi n kati ya chama kimoja ambacho kiafanya kazi na ccm ndio utajua kwenye tukio ili maana tundu lisu ushaidi wa awali ulikuwa cjui mago go go go nili
Serikali imeingia kwenye mtego ambao haujatambua maana kamili ya kuongelea kisa kilicho mpata mboe n bora wangekausha october aya maneno wanayo yasema yatawabeba upinzani bora wapigee kazii tu wakaushe maana ccm haina hoja ya kushindana wataonekana ni wajingaa wakiongea kuhusu maisha ya mtu...

Upinzan hawana akili za kilevi hamjawaelewa tu
 
Unadhani walishindwa kumuuguza kimya kimya bila mtu kujua kama kuna issues kama hizo? ? Nani angelijua hayo ya ulevi?
Ila wewe ni tofauti na wenzako Lumumba/Mataga, umejaribu kujenga hoja.
Kimya kimya bila PF3?
Kwa nini hakuripoti polisi apewe PF3 tusaidie wewe? Mbowe Aliendaje mbio mbio mbio bila PF3 Kama taratibu zinavyotaka kwa kesi Kama hiyo ya kuvamiwa? Mbowe na hawara yake Mukya Wana Cha kujibu
 
Suala hapa ni kudanganya umma kuwa alivamiwa,which everyone could have done that, first to protect his family and second to protect his image..ukiniquote uniambie what could you have done in this scenario??? otherwise kuchepuka wanaume wengi wanachepuka, wengine mmecomment kwenye hii thread na mnachepuka hata mkulu wenu wa pale magogoni anachepuka tena yeye its even worse kamzalisha mke wa mtu!!!!!
Ningebaki kimya.

Wanasiasa wetu hawana shida kabisa....sisi tuna shida kubwa tunaowashabikia.

Hatujui kuchambua uongo au ukweli.

Labda hawa watu ninaowasoma humu kila siku wakitaka maendeleo ya kweli huwa nadhani ni familia za karibu za viongozi wa nchi(upinzani&serikali) wakiwatetea ndugu zao ili waendelee kuneemeka na wanayochuma.
 
Kimada Joyce Mukya ana nguvu kuliko hata mtoto wa kumzaa wa Mbowe.

Mke wa ndoa wa Mbowe Ni daktari Tena bingwa akaona taarifa hizo zimfikie kimada sio mkewe wa ndoa Wala mwanawe.

Maisha haya puuuui.

Pole Sana mke wa ndoa wa Mbowe
😂😂😂
 
Kamanda umepanic Hahahahahah

Cha kupanick ni kipi? Niko vizuri na wala sina shaka na ninachoongea.

Nje ya mada, naona ulipotea kidogo humu, au uko kitengo tofauti siku hizi? Karibu tena.
 
Mkuu huko kwenye ushahidi unaotegemewa utashi wa binadamu, ukweli unaweza kupindishwa, CCTV footage zikiwekwa wazi ukweli wote utakupatikana. Hilo ni rahisi sana.
Yaani vipimo vya hospitali navyo visiaminike? Ni suala la kuchukuliwa vipimo upya kuthibitisha, maana majeraha, km kuvunjika mguu, hayafutiki siku moja.
 


View attachment 1476358View attachment 1476359
USHAHIDI wa awali wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu madai ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe umeonesh kuwa siku hiyo ya tukio Mbowe alikuwa amelewa chakali na alizunguka kwenye kumbi mbalimbali za starehe zinazouza vileo ikiwemo ya Royal Village.

Pia ushahidi huo unaonesha mbali ya kuwa kwenye maeneo hayo ya starehe alikuwa nyumbani kwa mzazi mwenzake Joyce Nkya ambaye ni Mbunge wa Viti Maaluma Chadema na kwamba hata taarifa za kwamba ameshambuliwa zinatia shaka kwani mashahidi wote ambao wameojiwa hakuna anayethibitisha uwepo wa tukio hilo zaidi ya Mbowe mwenyewe na dereva wake.

Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Jeshi hilo David Misime amesema Juni 9 mwaka huu walitoa taarifa ya awali kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Mroto kuhusu tukio la lililoripotiwa kuwa Mbowe amelezwa jijini Dodoma kwa kile kilichodaiwa kushambuliwa wakati anaingia nyumbani kwake .

Misime amesema baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo ya awali wamekuwa wakipokea simu nyingi kutoka kwa waandishi wa habari wakitaka kufahamu matokeo ya uchunguzi kuhusu taarifa iliyofikishwa Kituo cha Polisi Kati Dodoma.

"Napenda kujulisha kuwa Jeshi la Polisi limeendelea kufanya upelelezi wa kina kuanzia kwa mhanga mwenyewe wa tukio ambaye alidai kuwa muda wa saa saba hivi usiku akiwa kwenye ngazi ya kuingia nyumbani kwake akiwa na anatoka kwa mzazi mwenzake aitwaye Joyce Nkya ambaye ni Mbunge wa Viti Maaluma Chadema anayeishi eneo la Medeli Mjini Ddoma alishambuliwa na kuumia kwenye mguu wa kulia.

"Mhanga wa tukio hilo alidai wakati anashambuliwa alipiga kelele nyingi kuomba msaada ambao aliupata kutoka kwa dereva wake ambaye naye alipiga simu kwa Joyce Nkya kisha hospitali iliyoko takribani umbali wa kilometa tano nje ya Jiji la Dodoma pasipo umuhimu wa kutoa taarifa Polisi kabla ya kwenda kwa Joyce Nkya na Hospitali,"amesema Misime.

Ameongeza upelelezi wao umepata ushahidi kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa .

"Hata hivyo kwa mujibu wa wa mashahidi hawa hakuna hata mmoja aliyeweza kusikia kelele hizo au kuona mbowe akishambuliwa. Kwa mantikini hiyo ushahidi pekee unaozumngumzia kushambuliwa ni maelezo ya mhanga wa tukio(Mbowe) pamoja na dereva wake.

"Ambayo kwa hali ilivyo sasa yanatia shaka kuhusu ukweli wa tukio hili.Mashaka hayo yanaongezeka zaidi pale tulipobaini kuwa nyumbani kwa Mbowe alikuwepo kijana wake aitwaje James Mbowe ambaye hawakuona umuhimu wa kumjulisha kuhusu tukio lililotokea hapo nyumbani badala yake waliona umuhimu wa kumjulisha Jocye Nkya aliyekuwa mbali na eneo la tukio,"amesema.

Pia amesema uchunguzi wa Jeshi la Polisi nchini umethibitisha kuwa siku ya Juni 8 mwaka huu Mbowe alitembelea sehemu kadhaa za starehe zinazouza vileo ikiwepo ya Royal Village na kupata kinywaji.

"Hata hivyo alipofika hospitali alioneana akiwa katika hali ya ulevi chakari kiasi cha kushindwa kutamka maneno sawa sawa.Tunaendelea na uchunguzi kutafuta ukweli wa tukio hili, hivyo tunaomba wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia upelelezi huo wazilete kwetu. Tutaendelea kutoa taarifa kwenu kadri ushahidi utakavyopatikana,"amesema Misime kupitia taarifa ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari.

Pia soma

> News Alert: - Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

> Freeman Mbowe na Joyce Mukya wamtumia Mjomba wa Mtoto kupata cheti cha kuzaliwa

> Mhe. Mbowe na Mhe. Joyce Mukya mtafanya hili suala kuwa siri mpaka lini?

> Joyce Mukya ni nani? Pamoja na kutokuwa active kwenye Siasa bado anapeta ubunge CHADEMA zaidi ya miaka 10
[/QUO


Wanadanganya mpaka wanasahau...Juzi kamanda wa Polisi Dodoma kasema kuwa Mbowe alikanyagwa na watu kama watatu hivi...mbona hili hatujaliona kwenye ripoti yao....Job karekebishe tena hii statement uloowaandikia geshi la polith
 
Hii taarifa niya mtaani.na aliyeiandaa kwenye swala la propaganda bado uwezo wake uko chini sana.na kuiamini uwe una akili pungufu.wanasema wamefanya uchunguzi wa kina na wamejiridhisha mbowe alikua kalewa chakari kwahiyo hapo wanataka tuamini mbowe aliumia mwenyewe.

Sasa hiyo taarifa inaonyesha nikama wameshahitimisha uchunguzi wao alafu tena mwishoni wanasema wanaendelea na uchunguzi nakutoa rai kwa mtu yoyote mwenye taarifa za ilo tukio wakati huo huo wanasema kelele alizopiga mbowe hata majirani hawakuzisikia.Sasa wanaendelea kuchunguza nini.Mimi sio mwerevu ila hii taarifa ni ubabaishaji full.
Wamesema mwananchi mwenye taarifa anaombwa alisaidie jeshi la polisi.

Kama una taarifa wasaidie...utatusaidia na sisi tunaotaka haki itendeke bila kujali ccm na chadema.
 
Chadema jana walijaribu kuja na ka statement eti hawana imani na uchuzi wa polisi, nadhani baada ya kugundua mwamba amewaingiza chaka

Unajua shida ni kuwa matokeo ya uchunguzi huu wa polisi umefuata talking points zote zilizokuwa zinatolewa Bungeni. Huwezi kuwalaumu Chadema kwa kutilia shaka uchunguzi wenyewe. Kutoka alikanyagwa na kupigwa mateke hadi ameteleza mwenyewe ni parefu kidogo.

Amandla...
 
Back
Top Bottom