Jeshi la Polisi: Hakuna ushahidi kuwa Freeman Mbowe alishambuliwa. Alikuwa ametoka kwa Joyce Mukya. Alikuwa amelewa chakari

Jeshi la Polisi: Hakuna ushahidi kuwa Freeman Mbowe alishambuliwa. Alikuwa ametoka kwa Joyce Mukya. Alikuwa amelewa chakari

Hili hustahili kuchekelea, kwahyo mtu hatakiw kulewa?
Kulewa kila mtu analewa. Ila tukiumia ulevini hatusemi uongo Wala kumsingizia mtu!! Lazima ni cheke hii ze comedy show ni shida [emoji23][emoji1787][emoji2960]
 


View attachment 1476358View attachment 1476359
USHAHIDI wa awali wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu madai ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe umeonesh kuwa siku hiyo ya tukio Mbowe alikuwa amelewa chakali na alizunguka kwenye kumbi mbalimbali za starehe zinazouza vileo ikiwemo ya Royal Village.

Pia ushahidi huo unaonesha mbali ya kuwa kwenye maeneo hayo ya starehe alikuwa nyumbani kwa mzazi mwenzake Joyce Nkya ambaye ni Mbunge wa Viti Maaluma Chadema na kwamba hata taarifa za kwamba ameshambuliwa zinatia shaka kwani mashahidi wote ambao wameojiwa hakuna anayethibitisha uwepo wa tukio hilo zaidi ya Mbowe mwenyewe na dereva wake.

Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Jeshi hilo David Misime amesema Juni 9 mwaka huu walitoa taarifa ya awali kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Mroto kuhusu tukio la lililoripotiwa kuwa Mbowe amelezwa jijini Dodoma kwa kile kilichodaiwa kushambuliwa wakati anaingia nyumbani kwake .

Misime amesema baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo ya awali wamekuwa wakipokea simu nyingi kutoka kwa waandishi wa habari wakitaka kufahamu matokeo ya uchunguzi kuhusu taarifa iliyofikishwa Kituo cha Polisi Kati Dodoma.

"Napenda kujulisha kuwa Jeshi la Polisi limeendelea kufanya upelelezi wa kina kuanzia kwa mhanga mwenyewe wa tukio ambaye alidai kuwa muda wa saa saba hivi usiku akiwa kwenye ngazi ya kuingia nyumbani kwake akiwa na anatoka kwa mzazi mwenzake aitwaye Joyce Nkya ambaye ni Mbunge wa Viti Maaluma Chadema anayeishi eneo la Medeli Mjini Ddoma alishambuliwa na kuumia kwenye mguu wa kulia.

"Mhanga wa tukio hilo alidai wakati anashambuliwa alipiga kelele nyingi kuomba msaada ambao aliupata kutoka kwa dereva wake ambaye naye alipiga simu kwa Joyce Nkya kisha hospitali iliyoko takribani umbali wa kilometa tano nje ya Jiji la Dodoma pasipo umuhimu wa kutoa taarifa Polisi kabla ya kwenda kwa Joyce Nkya na Hospitali,"amesema Misime.

Ameongeza upelelezi wao umepata ushahidi kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa .

"Hata hivyo kwa mujibu wa wa mashahidi hawa hakuna hata mmoja aliyeweza kusikia kelele hizo au kuona mbowe akishambuliwa. Kwa mantikini hiyo ushahidi pekee unaozumngumzia kushambuliwa ni maelezo ya mhanga wa tukio(Mbowe) pamoja na dereva wake.

"Ambayo kwa hali ilivyo sasa yanatia shaka kuhusu ukweli wa tukio hili.Mashaka hayo yanaongezeka zaidi pale tulipobaini kuwa nyumbani kwa Mbowe alikuwepo kijana wake aitwaje James Mbowe ambaye hawakuona umuhimu wa kumjulisha kuhusu tukio lililotokea hapo nyumbani badala yake waliona umuhimu wa kumjulisha Jocye Nkya aliyekuwa mbali na eneo la tukio,"amesema.

Pia amesema uchunguzi wa Jeshi la Polisi nchini umethibitisha kuwa siku ya Juni 8 mwaka huu Mbowe alitembelea sehemu kadhaa za starehe zinazouza vileo ikiwepo ya Royal Village na kupata kinywaji.

"Hata hivyo alipofika hospitali alioneana akiwa katika hali ya ulevi chakari kiasi cha kushindwa kutamka maneno sawa sawa.Tunaendelea na uchunguzi kutafuta ukweli wa tukio hili, hivyo tunaomba wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia upelelezi huo wazilete kwetu. Tutaendelea kutoa taarifa kwenu kadri ushahidi utakavyopatikana,"amesema Misime kupitia taarifa ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari.

Pia soma
Kwa hiyo Moroto alidanganya siyo mbowe hakukanyagwa na yeyote. Makao makuu Dar wanaelewa mazingira ya tukio kuliko Dodoma. Tell this to birds. EU and US beware of this fallacy. There were no investigation during Tundu Lisus attack. And where were the security guards this time. What about the cCTv cameras? Tell the nonsense to birds!!Tell these fallacy to birds. Between the Dodoma RPC and the shelf seaters of the Car headquarters who is giving the truth? By the way where the 24hour security guards this time? And the cameras? Tell your stories to birds.
There were cameras there were 24 hours security guards. Get u
> News Alert: - Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

> Freeman Mbowe na Joyce Mukya wamtumia Mjomba wa Mtoto kupata cheti cha kuzaliwa

> Mhe. Mbowe na Mhe. Joyce Mukya mtafanya hili suala kuwa siri mpaka lini?

> Joyce Mukya ni nani? Pamoja na kutokuwa active kwenye Siasa bado anapeta ubunge CHADEMA zaidi ya miaka 10
 
Kwa mtazamo wangu,naamini mpaka sasa CHADEMA wameshakusanya taarifa za nini kilitpokea ila waliona kueleza kila kitu ingekuwa ni kuingilia uchunguzi wa Jeshi la Polisi, hivyo waliona ni busara watoe nafasi kwa Polisi kufanya kazi yao na kama maelezo ya Polisi yatakuwa tofauti na kilichotokea, basi watajitokeza kueleza kwa undani nini kilitokea na hiki ndicho binafsi nakitarajia kitatokea wakati wowote kuanzia kesho.

Kama kumbukumbu zangu ziko sahii, Mnyika alisema wakati tukio linatokea,Mbowe hakuwa peke yake bali kulikuwa na watu wengine ambao hawakuwataja hivyo naamini katika kujibu taarifa ya Jeshi la Polisi, CHADEMA watawataja waliokuwepo na pia na kama kuna ushahidi wa ziada,basi watautoa hadharani.

Naamini hata Mbowe mwenyewe atatoa maelezo ya nini hasa kilitokea.

Tusubiri.
Lazima ataeleza. Kwani ndio matumizi ya bilioni 7
FB_IMG_15918103613000337.jpg
 
Inaonekana Joyce Mkuya ni mtamu sana kuliko mke wa ndoa Lilian Mbowe, maana kila janga lazima ahusishwe
Shetani kakutawala wewe na maisha yako.Piga magoti sali uweze kumrudia Mungu
 
Sina tatizo na maelezo yako ya kuchukua maelezo kwa wahusika kwanza, hilo nakubali kabisa. Lakini ni mwendawazimu tu ataacha kuchukua kilichonaswa na CCTV wakati zipo, huku kukiwa na utata kwenye maelezo. Maelezo haya hayaingii akilini.

Kama ushahidi unapatikana kwa watu tu, CCTV camera Ni za nini? Maana nijuavyo CCTV hazizuii wezi, bali hurekodi matukio kwenye eneo husika, ili kusaidia uchunguzi. Hilo liko wazi. Huoni kuendelea kukwepa hilo, ndio kukwepa ukweli ulipo zaidi ya huu upotoshaji wa pande zote?
Watetezi wa Mbowe angalia moo wangapi humu kwenye Hili hamzidi watatu !!!! Mliokomaa Tena nadhani ni wewe mwenyewe una ID tofauti Mbowe kabwagiwa Hili zigo . Chadema wamejitambua wewe ndio unatoka mijasho peke yako na wenzio wawili tu humu toka mada ianze
 
Kulewa kila mtu analewa. Ila tukiumia ulevini hatusemi uongo Wala kumsingizia mtu!! Lazima ni cheke hii ze comedy show ni shida [emoji23][emoji1787][emoji2960]
Iwapo wangemjeruhi kama Lisu isingekuwa stori ya kulewa, muulize aliyesema hili akujbu la Lisu alikuwaje
 
Aya ya PILI ya Taarifa ya Misime inamtaja mtu anaeitwa JOYCE MUKYA wakati Aya ya Tatu ya taarifa hiyo hiyo inamtaja mtu anaeitwa JOYCE NKYA, so which is which wakuu
naona huu uandishi katika report ya upelelezi kama imemkazia sana Joyce ukiingia deep inajipambanua wazi kuwa ilitaka kumvua nguo mtu flaani tu!
 
Hapa unaongelea mtu anayefaa kuongoza chama, au unaongelea mtu anayefaa kuongoza chama hawezi kuwa muongo? Mimi hapa najua watu wote ni waongo, ili wanatofautiana viwango. Na kwa kulitambua hilo ndio maana nataka cctv footage ukweli uwe wazi. Sasa naona we tayari umeshaamini taarifa ya polisi na kuanza kumwaga matusi, huku maelezo ya Mbowe na polisi yakiwa ni utata mtupu.
We jamaa bwana!
 
Sijui ni comment nini!, eti Mbowe hivi hii taarifa ni ya kweli au uongo?.
 
"Tulikuwa na shaka kuanzia siku ya kwanza juu ya Polisi kutumika kupotosha ukweli kuhusu tukio la Mwenyekiti Freeamn Mbowe. Mashaka hayo yamedhihirika kwa kutekeleza maelekezo aliyotoa Spika Ndugai kwao Bungeni kwa kusema uongo uleule uliosemwa na CCM Bungeni," Jon Mrema

"Kama ilivyokuwa tukio la kushambuliwa Tundu Lissu "hadi tukataka wachunguzi wa kimataifa, wamerudia tena utaratibu huo wa kusema uongo. Imekuwa ni kawaida yao kuficha ukweli na kuzusha mambo kama walivyofanya kwa mauaji ya Mwanahabari Daud Mwangosi na Aqulina Aquline "Jon Mrema

"Tunalitaka jeshi la polisi lifanye majukumu yake kwa weledi na sio kujiingiza kwenye propaganda za kisiasa ambazo zitalifanya lisiaminike kwa wananchi.l," Mkurugenzi wa Uenezi, Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje
 
Wao wamefanya uchunguzi, kafanye na wew alafu uje na ushahidi kama huo wa polisi, usiendeshwe na hisia kwa ujeuri utaishia kufeli, neno zuri kwako litakuwa halina ukweli na lenye ukweli litakuwa sio zuri kama hii ripoti ya jeshi la polisi
Yeye ajibuye kabla hajajua ni upumbavu na aibu kwake.

Uchunguzi upi wamefanya? Pale kuna CCTV camera kwanini wasituoneshe kilichofanyika? Mtu aliyeanguka anasagikaje mguu pasipokuumia sehemu nyingine yoyote? Mbona Rpc wa Dodoma alithibitisha kuwa alikanyagwakanyagwa?

Usipende kutoa majibu mepesi kwenye hoja/maswali magumu.
tapatalk_1591795235259.jpg
 
Ndugu zangu polisi just simple and cleal fungueni CCTV camera ZA nyumba ya Mbowe over.

Ni jambo la aibu polisi unatoa matokeao ya uchunguzi wako alafu unasema kama kuna mtu Ana taarifa akupe ulizo toa wewe nu USHUZI?.
Ni aibu wewe mtaalamu wetu unasema tukio bado mnalichuguza unachunguza nini wakti umeisha toa taarifa?
 
Back
Top Bottom