Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Kuna tangazo Azam Tv linalohusu tamasha la watoto litakalofanyika mwezi wa 8 Oyterbay kwenye uwanja wa kijani zamani kulikuwa dipu ya kuogeshea mbwa, moja ya "mchezo" ni wa kulenga shabaha kwa kutumia bunduki bandia, huu kwa watoto wenye wazazi wanaomiliki bunduki ambao ni wengi kulingana na eneo unaweza usiishie hapo bali utafika nyumbani siku yoyote ile mtoto atakapojisikia kuiba bunduki ya baba na kulenga shabaha.
Hivi waliouandaa mchezo huo kwa watoto walifikiria nini, mtoto alenge shabaha kwa bunduki bandia ili iweje! Ninaliomba jeshi la polisi lisiuruhusu mchezo huo na mingine isiyofaa kwa watoto, pia iwe imakagua michezo yote ya watoto, ninakumbuka huko nyuma mjini Morogoro wakati wa sherehe za nanenane kuna mtoto alifariki baada ya kuanguka kwenye pembea ya kuzunguruka, hii ilitokana na kukosa ukaguzi wa kuona mnyororo unaotakiwa kumshika kama haupwai.