Jeshi la Polisi huu si mchezo wa watoto, ni janga kwa wazazi

Naunga mkono hoja, hii michezo si sahihi kwa watoto mimi binafsi hata bunduki au silaha za bandia huwa siwanunulii watoto.
Michezo hii ndiyo imewafikisha watoto wa marekani kufanya mauaji kwa kuchukua silaha za wazazi wao na kwenda nazo shule "kuzichezea" waone kama kweli zinaua.
 
Dogo acha kuning'iniza poumbou hapo sofani sebuleni kwa shemeji Yako. Katafute chumba uswaz ujitegemee.

Sasa tuseme dada Yako na watoto wote wamesafiri ukabaki na shemeji Yako tu itakuwaje na haka kapupwe mwezi huu kanavyopuliza.
 
Jikomboe kifikra na kimawazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi sioni ubaya wa kumfundisha mtoto kulenga shabaha.

Hiyo ya kusema atachukua bunduki ya mzazi wake hapo sasa kosa sio la mtoto ni la mzazi kwa kuacha bunduki mahali ambapo si salama.

Bunduki ikiachwa mahali ambapo si salama sio mtoto tu hata mtu mzima anaweza kuichukua na kufanyia uhalifu.

Halafu hao watoto ni wa umri gani, wasiojua kua hii ni halisi na hii ni fake, nadhani hata kwenye mafunzo watafundishwa na kuonywa kutumia bunduki halisi.

Wawafundishe tu aisee, sioni ubaya kwenye hilo. Wakimaliza hilo wazazi wawapeleke watoto wajifunze mapigano ya ana kwa ana.
 
hii ya shabaha ,nadhani iangaliwe upya. watt wetu wetu wa siku hz hawa,wasije wakatulenga bullets majumbani.kuna kupitiwa unajikuta umehifadhi silaha with little Care!!
 
Sasa hizo ndio sababu gani zisizo na mashiko

Watanzania tupo nyuma sana

Ulizani bunduki zinawekwa jikoni au kabatini
 
Kulenga shabaha hakujalishi halisi au feki, ukijifunzia chochote ukipewa halisi utaweza, na ukijifunzia chochote utakuwa na ujasiri na hamu ya kutumia halisi hivyo utaitafuta.
 
Kulenga shabaha hakujalishi halisi au feki, ukijifunzia chochote ukipewa halisi utaweza, na ukijifunzia chochote utakuwa na ujasiri na hamu ya kutumia halisi hivyo utaitafuta.
Amna icho kitu bna, achana na mawazo hayo.
Tukiwa watoto tulikua tunaendesha vile vigari vyetu wala hakukua na mtu anaewaza kua atafute gari halisi aendeshe.

Michezo ya bunduki, tushacheza sana wala hakuna tukio tumewahi kufanya.

Michezo ya kibaba na mama watoto wanaigiza kama kweli vile lakini haiathiri ukuaji wao wala heshima kwa wazazi wao zaidi ya kuwajengea kua waamuzi wazuri.
 
na watu wanaona sawa tu
 
Dogo acha kuning'iniza poumbou hapo sofani sebuleni kwa shemeji Yako. Katafute chumba uswaz ujitegemee.

Sasa tuseme dada Yako na watoto wote wamesafiri ukabaki na shemeji Yako tu itakuwaje na haka kapupwe mwezi huu kanavyopuliza.
Ndo akili zako zilipo ishia,, unatofauti gani na mbwa aliyenusa pheromone [emoji2369]
 
..hamjaona CHIPUKIZI wa Ccm wakichezea silaha?
Kama watoto wanazuiliwa wasitumie toys kwamba watakuja kuwa wauaji je majizi ya kura yalipokua bado madogo yalikemewa vipi kutojifunza wizi wa kura unaoleta madarakani viongozi vimeo ambao sio chaguo la wananchi.?
 
ukenikumbusha vile vibastola vya zamani vinatoa mlio na moshi ndani vinajazwa baruti aisee vile vina vibee mnoo
 
Naunga mkono hoja, kisa haya yafuatayo;

1. Mtoto, hana uwezo mkubwa wa kutofautisha kati ya bunduki toi na bunduki halisia. Kwa wazazi wenye bunduki, siku akiiweka mikononi mwake ataendelea kucheza, kumbe anauwa kweli.

2. Kumfunza shabaha mtoto hakuna faida yoyote inayopatikana kwa wazazi au taifa kwa ujumla

3. Kulenga shabaha, kwa mtoto kwake ni mchezo, lakini siku akiipata bunduki halisia inayofanana na ile aliyoitumia kwenye kulenga shabaha, anaweza akauwa huku hajui kwamba anauwa na hatajua madhara ya bunduki halisia.

4. Kwenye kulenga shabaha, mtoto hajifunzi kitu chenye faida kwake ukilinganisha na hasara mtoto anazoweza kuziweka kwa jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…