Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Jeshi la Polisi nchini limejipa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyotokea kwenye daraja la selander, ambapo mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Hamza, aliwafyatulia risasi askari watatu na mlinzi mmoja wa kampuni ya SGA na kuwaua wote na askari wengine kadhaa kujeruhiwa na hatimaye yeye mwenyewe kuuawa na askari waliokuwa wakilinda doria eneo hilo
Kuna hadithi nyingi zinazosemwa semwa kuhusu nia ya huyo kijana aliyewafyatulia risasi askari hao.
Kuna wengine wanadai kuwa huyo kijana alikuwa analipiza kisasi kwa askari hao, baada ya kumdhulumu dhahabu zake ambazo alikuwa akiziuza.
Hebu tujiulize hivi hawa hawa Polisi watatoa ripoti bila kuuficha ukweli, hata kama ripoti hiyo itasema chanzo cha mauaji hayo ni wao Polisi kufanya dhuluma hiyo ya kumpora dhahabu zake huyo kijana??
Hata ukiangalia mazingira ya mauaji hayo, kwa huyo kijana kuwa-target maaskari watupu na kuwaacha raia, inadhibitisha tetesi hizo.
Ni kwanini basi isiundwe Tume huru ya kuchunguza chanzo cha mauaji hayo, Tume hiyo ihusishe na wataalam wengine kwa mfano majaji wastaafu, wanasiasa maarufu toka kwenye vyama vya siasa, na kadhalika na kadhalika.
Ninavyoona Mimi, kuunda Tume ya uchunguzi, ya maaskari watupu, ni sawaswa na kesi ya nyani kumpa ngedere!
Ni dhahiri hapo hata hayo matokeo ya uchunguzi wa Tume hiyo unaweza kuyabashiri