Jeshi la Polisi kuongea na Waandishi wa Habari Septemba 13, 2024 kuhusu tamko la CHADEMA la Septemba 11, 2024

Jeshi la Polisi kuongea na Waandishi wa Habari Septemba 13, 2024 kuhusu tamko la CHADEMA la Septemba 11, 2024

Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa ya jeshi la polisi Nchini View attachment 3094509

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Condom ilihitajika siku ile
 
Mungu hajawahi kushindwa na shetani..

Kaini alipo muua ndugu yake akaulizwa umempeleka wapi nduguyo akajibu kwa jeuri mimi nimekuwa mlinzi wake?.. Mungu akatoa adhabu wote tunajua....

Uzuri ni kwamba kabla Mungu hajatoa hukumu yake anakuuliza kwanza..
Mfano Walipopotea bensaa8 azori tuliwauliza polisi hawa watu wapo wapi wakatujibu kwa jeuri...

T.lissu alipopigwa risasi tukawauliza wasiojulikana akina nani na ni nani anawatuma wakatupuuza?

Nadhani sote tunajua kilichotokea Yalikuwa ni majonzi kwa Taifa zima.. Mungu sio John..

Leo tuna watu wengi wametekwa na wengine wameuawa kama mbuzi wa supu kwa kumwagiwa Tindikali. Tumeuliza sana Mbona polisi mnafanya hivyo? Wametujibu kwa jeuri..

mtu akiwa na cheo bana anadhani ni moyo atakufa nao kumbe unapata cheo kwa muda na unaondoka muda wowote!! Sijui kama wenye vyeo mnalijua hilo

Wabunge tena tuliowapa dhamana kukaa sehemu takatifu ambapo vitabu vitakatifuna dua zinaanza kabla ya vikao. Tukawataka wajadili kuhusu kutekwa!! Aisee Yule Mama sipiiiika akajibu kwa jeuri, hawana huo muda machafu.. angepotea mwanaye angejibu vile?

Tukasema poa ngoja twende kwa pilato huko nako wakatupuuza!!! Jamani sisi tumewakosea nini? Au hawa ndugu zetu waliopotea hawana damu miili yao ina maji tu.?

Tukajipa Tumaini Mama ni mama!!
Huwezi amini Mama akasema kauli tata et ni drama .. jamani tumekuwa wagriki kwamba tunaigiza movie za ukweli..huku familia zao wanaomboleza?

Mama hivi kweli wanafanya drama za kijumwagia Tindikali na kupigwa risasi za kichwa?

Mama hata kama wamekosea adhabu wanazopewa ni kali na nzito sana Mama. Mama gani unakuwa katili kiasi hiki kwa kauli zako wakati mama ni faraja na tumaini kwa watoto na mme!!! Umetukosea na umemkosea Mungu wako.

Watoto na familia zao zinawalilia ukishindwa kujali hilo basi ebu kumbuka ule uchungu wa Leba mama!!!

wazazi wao wanavyoumia kuwakosa watoto wao, basi warudishiwe hata miili yao wapate kuomboleza mara ya mwisho!!!!

HATA KAMA MTU AMEKUKOSEA NAMNA GANI!! USICHUKUE UAMUZI WA KUMWAGA DAMU YAKE N.A. KUTOKA UHAI WAKE..hilo ni jukumu la Muumba wetu.
Hao ndio wamama wa kizimkazi na mama supika wa akina mwakafyale
 
CHADEMA KUWAPA USHIRIKIANO POLISI NI USALITI NA MZAHA KWA ROHO ZA WALIOTEKWA, KUPOTEA NA KUUAWA.

1.Nimetaarifiwa kuwa Jana Jumanne 10 September 2024 jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kupitia RCO Kinondoni waliwapigia simu mawakili wa CHADEMA kwamba wanamuhitaji Katibu Mkuu John Mnyika kwa mahojiano.

2.Kama John Mnyika na CHADEMA watatoa Ushirikiano kwa Jeshi la Polisi Tanzania kufuatia kitu kinaitwa kamati ya uchunguzi watakuwa kuwa wamefanya mzaha mkubwa juu ya sisi wanachama wao tunotekwa, kuuawa na kupotea kwa kukubali kuwapa ushirikiano watuhumiwa namba moja wa matukio hayo.

3.Jeshi la Polisi halina uhalali wa Kimaadili Kufuatia kupotea kwa watu zaidi ya 100 na sita wakiwa ni wanachama wa CHADEMA huku mmoja akiokotwa akiwa ameuawa maeneo ya Ununio

4.Viongozi wa CHADEMA wakae vikaoni watoke na msimamo mmoja wa chama kuhusu wapi watapeleka ushahidi wao na maelezo wanayo yajua kuhusu watekaji na wauaji

•Taarifa ambazo CHADEMA wanazo na wana uhakika nazo isipokuwa hawana mamlaka inayoaminika na yenye nia ya dhati ya kushughukikia madai yao.

5.Jeshi la Polisi Tanzania halina mpango wa kuchukua hatua wala kukomesha utekaji na mauaji ya wananchi au makada wa CHADEMA bali wanalenga kutaka kujua CHADEMA wanajua nini kuhusu tuhuma zao ili watumie nafasi hiyo kuficha ukweli na kuharibu ushahidi.

6.Jeshi la Polisi Tanzania lilimsikia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe 22 August 2024 kufuatia tuhuma kwa Jeshi la Polisi, akimtuhumu ZCO Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, ACP FAUSTINE MAFWELE kuhusika katika kuratibu na kusimamia vikundi vinavyoendesha utekaji ndani ya Jeshi la Polisi, wakiwa na makao yao nyuma ya Kituo cha polisi Chang'ombe maarufu kama Tembo 7.

7. Jeshi la Polisi pamoja na Kusikia tuhuma za Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe za 22 August 2024, Hawakuwahi kujitokeza hadharani kukanusha tuhuma hizo.

•Hawakuwahi kumuhitaji Freeman Mbowe kumuhoji na kutaka kujua ukweli wa tuhuma hizo.

•Hawakuwahi kumfungulia mashtaka Freeman Mbowe juu ya upotoshaji au uchochezi kama tulivyo wazoea.

•Hawakuwahi kuhabarisha umma kuwa tuhuma za Freeman Mbowe zilikuwa zinafanyiwa kazi

8.Jeshi la Polisi Tanzania walichofanya ni kwenda kuvunja maskani ya kikosi kazi kinachotuhumiwa na Freeman Mbowe, kuendesha shughuli za utekaji na mauaji nyuma ya kituo cha Polisi Chang'ombe maarufu kama "TEMBO 7" na sasa wamehamia sehemu mpya ya maeneo ya Mpingo House.

•Huku askari waliotajwa na Freeman Mbowe walifuta akaunti zao katika mitandao ya kijamii kama alivyofanya Afande Semageni Shabani mmoja wa watuhumiwa katika kikosi kazi cha Polisi Chang'ombe (Tembo 7)

9.Kama Jeshi la Polisi Tanzania wangekuwa wana nia ya dhati ya kushughulikiia tuhuma za Mwenyekiti wa CHADEMA huenda Kifo cha Kiongozi wake wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa Bwana Ali Muhammad Kibao kisingetokea.

10.Tarehe 07 September 2024 majira ya Saa 6: 00 mchana, Wakati Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika anafamya kikao na Waandishi wa Habari kulitaka Jeshi la Polisi lijitokeze kusema alipo Kiongozi wake Ali Muhammad Kibao

•Tayari Jeshi la Polisi lilikuwa limeshauchukua Mwili wa Ali Muhammad Kibao kutoka Ununio na kupeleka hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni ya Mwananyamala

•Siku hiyo tarehe 07 September 2024 Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David Misime akitoa taarifa yake kuhusu kufanyia kazi tuhuma za John Mnyika tayari Jeshi la Polisi ilikuwa limeshaokota Mwili wa Ali Muhammad Kibao kwa zaidi ya saa 8 zilizopita tangu saa 1:00 Asubuhi baada ya Wakulima wa mchicha wa Ununio kujulisha mamlaka kuhusu kukutwa kwa mwili wa binadamu eneo la jirani la vitalu vyao vya mchicha.

11.Wakati wote huo Jeshi la Polisi lilikuwa linajua Mwili huo uliookotwa eneo la Ununio ndiyo Mwili wa Kiongozi wa CHADEMA anayetafutwa

•Badala ya jeshi la Polisi Kuwajulisha CHADEMA wao waliwazunguka CHADEMA na kuwatafuta ndugu wa Marehemu Ali Muhammad Kibao na kuwataarifu wafike hospitali ya Mwananyamala siku hiyo hiyo ya Tarehe 07 September 2024 majira ya mchana

•Na hata ndugu walipoutambua mwili wa marehemu Ali Muhammad Kibao Jeshi la Polisi lilificha taarifa isiwafikie CHADEMA na kuwaomba Wanafamilia Msiba uwe siri na usiwe wa kisiasa kwa kuwaondoa CHADEMA wasiwe sehemu ya msiba.

Na hata CHADEMA na mawakili wao walipofika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni ya Mwananyamala sehemu ya kuhifadhia maiti polisi waliwazuia CHADEMA kuingia ndani ya chumba cha Autopsy

•Hii pia inathibitishwa na taarifa ya Jeshi la Polisi ya tarehe 07 September 2024 kupitia kwa Msemaji wake DCP David Misime ambapo alisema kuwa wapo tayari kushirikiana na familia tu huku wakikwepa kutaja CHADEMA katika taarifa yao pamoja na kujua marehemu ni Kiongozi wa CHADEMA

•Je, leo Jeshi la Polisi ndiyo limegundua linahitaji Ushirikiano na CHADEMA..? Huu kwa lugha rahisi tu, tunaweza kuita ni unafiki wa kiwango cha juu sana na hatutakiwi kuufumbia macho.

11.kuanza kutafutwa leo na Jeshi la Polisi ni unafiki mkubwa. Jeshi la Polisi liliwapuuza CHADEMA likaziba masikio na kuacha kufanyia kazi tuhuma za CHADEMA kwa askari wake wanaotajwa kuendesha Operesheni za kuteka na kuua watu. Badala yake watuhumiwa hao wapo maofisini wanaendelea na kazi chafu wanazotuhumiwa nazo.

Baada ya kuona Rais Samia anatoa pole kwa familia na CHADEMA na Kulaani mauaji ndiyo Jeshi la Polisi likaanza kujifanya linafanya uchunguzi au kuongeza Polisi Wengine kuchunguza tukio la kutekwa Ali Kibao na kuuwawa.

12.CHADEMA wasiingie katika mtego huo wa kuhojiwa na Polisi tena na RCO ambaye yupo chini ya Usimamizi wa Boss wake ZCO Faustine Mafwele ambaye CHADEMA wamemtuhumu hadharani kuhusika na mutekwa na Kupotea kwa watu Dar es saalam ikiwemo Godwin Mlay, Deusdedith Soka na Frank Mbise.

Badala yake CHADEMA waandae ushahidi na mashahidi wao kwenda kutoa taarifa na maelezo kwa tume huru ya kijaji kama ilivyokuwa kwa Jaji Kipenka Mussa katika mauaji ya Wafanyabiashara wa Mahenge, Morogoro itakayokuwa huru kukusanya taarifa, kuhoji wahusika na mashahidi pamoja na kutoa mapendekezo juu ya kila tuhuma za mtuhumiwa.

Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595
The voice of the silenced Majority
 
HATA KAMA MTU AMEKUKOSEA NAMNA GANI!! USICHUKUE UAMUZI WA KUMWAGA DAMU YAKE N.A. KUTOKA UHAI WAKE..hilo ni jukumu la Muumba wetu.
Inawezekana pia kwamba hii ndiyo njia "Muumba wtuy" ameamua kuitumia kutuponya tulio baki? Hili ni swali tu mkuu wangu!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa ya jeshi la polisi Nchini View attachment 3094509

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wewe Lucas Mwashambwa ni kibaraka wa Mafwele, na nyie ni wamwagaji wakubwa wa damu isiyo na hatia
GXSjdPnWUAAzb2j.jpg
 
Yaani mpaka sasa hakuns hata mtu mmoja aliyekamatwa?😁😁
 
Chadema wakiweka ugoko, jesho linaweka jiwe.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa ya jeshi la polisi Nchini View attachment 3094509

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Kazi ya kuua.
Lucas Hebel Mwashambwa,
Hatoshi, labda kuongoza familia yake na kina Abdul
Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wanatoa taarifa gani kama wanashindwa kukamata wauaji ?
 
Vyombo vya ulinzi na usalama ni taswira ya Serikali iliyopo madarakani:

Ukiwa na serikali ya hovyo, unakuwa na vyombo vya ulinzi na usalama vya hovyo.

Ukiwa na Serikali inayoamini survival yake ni kwa kudhulumu haki, vyombo vya ulinzi na usalama kazi yake kubwa ni kuua wananchi wanaotetea haki. NA HAPA NDIPO TULIPO KWA SASA.
 
Si wangeacha tu! Maana tayari wananchi tunafahamu watazungumzia kuhusu kupiga marufuku kitu chochote kitakachofanywa na hao Chadema!

Lakini pia watatoa maneno ya vitisho kwa watu wote watakaoshiriki aidha kwenye maandamano, au kitu chochote kitakachofanywa na Chadema!!

Na mwisho wa siku watu wenye akili tutaendelea kuamini ya kwamba hilo jeshi limeundwa kwa madhumuni ya kuilinda CCM, na siyo kuwalinda raia na mali zao.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa ya jeshi la polisi Nchini View attachment 3094509

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Haya sasa ni malumbano kama ya vigodoro.
Kisa mna bunduki.
Toeni taarifa za walipo kina Soka.
Toeni taarifa kuhusu walio tajwa na Mbowe je? Kweli ni watumishi wa taski force au sio kweli.
Kanusheni maelezo ya Sativa je alifikishwa Ostabay polisi au ni uzushi.
Je alifikishwa Arusha au ni propa ganda?
Kombo mlikataa hamko nae baada ya siku 29 mkawa nae. Je ni nani alimleta kwenu? Au alikuwa ame jiteka baadae aka jisalimisha kwenu?
Sio kupambana na Chadema kwa nguvu ya dola..
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa ya jeshi la polisi Nchini View attachment 3094509

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Haya sasa ni malumbano kama ya vigodoro.
Kisa mna bunduki.
Toeni taarifa za walipo kina Soka.
Toeni taarifa kuhusu walio tajwa na Mbowe je? Kweli ni watumishi wa taski force au sio kweli.
Kanusheni maelezo ya Sativa je alifikishwa Ostabay polisi au ni uzushi.
Je alifikishwa Arusha au ni propa ganda?
Kombo mlikataa hamko nae baada ya siku 29 mkawa nae. Je ni nani alimleta kwenu? Au alikuwa ame jiteka baadae aka jisalimisha kwenu?
Sio kupambana na Chadema kwa nguvu ya dola..
 
Back
Top Bottom