Jeshi la Polisi lakanusha kumshikilia Sheikh Zuberi Nkokoo Mkoani Singida

Jeshi la Polisi lakanusha kumshikilia Sheikh Zuberi Nkokoo Mkoani Singida

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida lakanusha taarifa zinazozambaa kuwa limemkamata na kumshikilia Shekhe Zuberi Nkokoo (53) mwalimu wa dini ya Kiislam kutoka Taasisi ya Islamic Foundation ambaye aliripotiwa kupotea Juni 02, 2025 majira ya saa 5:30 usiku akiwa karibu na Sheli ya Lake Oil iliyopo Mtaa wa Misuna, Manispaa ya Singida.

Jeshi la Polisi Singida linaendelea kufanya uchunguzi wa kubaini mahali alipo mtu huyo ili kujua kama amekamatwa au ameshikiliwa, mhusika ni nani na sababu za kushikiliwa kwake.

Aidha, Jeshi la Polisi Singida linawashikilia watu watatu kwa mahojiano ambao ni Abdul Ally (58), Mfanyabiashara na Mkazi wa Muriet mkoani Arusha, Shabani Ramadhani Ikenga (54), Mfanyabiashara na Mkazi wa Kisaki Manispaa ya Singida, na Maulid Mussa (52), Mfanyabiashara na Mkazi wa Muriet mkoani Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linawataka wananchi kupuuza taarifa za uzushi na za uongo zinazozenezwa kwa nia ya kuleta taharuki kwa jamii na badala yake watoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kubaini wapi alipo kiongozi huyo wa dini.

View attachment 3358145
Waislam nao wamefikiwa?
 
Yaani jeshi la polisi kabisa wanaandika "sheli" ! Kweli "ukanjanja" bado hatua ndefu kufutika.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida limekanusha vikali madai yanayosambaa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa linamshikilia Sheikh Zuberi Nkokoo (53), mwalimu wa dini ya Kiislamu kutoka taasisi ya Islamic Foundation, ambaye ameripotiwa kupotea tangu Juni 2, 2025 usiku.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida Amon Kakwale, Sheikh Nkokoo alionekana mara ya mwisho majira ya saa 5:30 usiku akiwa karibu na Sheli ya Lake Oil, iliyopo Mtaa wa Misuna, Manispaa ya Singida. Taarifa za kupotea kwake zimezua mjadala mpana mitandaoni, huku baadhi ya watu wakidai kuwa anashikiliwa na vyombo vya dola — jambo ambalo sasa limekanushwa na polisi.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linakanusha taarifa zinazoenezwa kuwa limemkamata na kumshikilia Shekhe Zuberi Nkokoo. Tunaendelea kufanya uchunguzi kubaini alipo, kama amekamatwa, na iwapo ameshikiliwa, ni nani aliyefanya hivyo na kwa sababu gani,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Katika hatua za awali za uchunguzi, Jeshi la Polisi limewakamata na kuwaweka chini ya ulinzi watu watatu kwa mahojiano, wanaotajwa kuwa na taarifa au uhusiano wa karibu na mazingira ya kupotea kwa Shekhe huyo.

Walioshikiliwa ni Abdul Ally (58), mfanyabiashara kutoka Muriet, Arusha, Shabani Ramadhani Ikenga (54), mfanyabiashara na mkazi wa Kisaki, Singida na Maulid Mussa (52), mfanyabiashara kutoka Muriet, Arusha.

Jeshi la Polisi pia limetoa onyo kwa wananchi wanaosambaza taarifa zisizo rasmi au za upotoshaji kupitia mitandao ya kijamii, likisema hatua hizo zinachochea hofu na taharuki isiyo ya lazima.

“Tunawaomba wananchi kupuuza taarifa za uzushi na badala yake watoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kufanikisha kupatikana kwa kiongozi huyo wa dini,” aliongeza Kamanda huyo.

=

Kila siku watu wanapotezwa, pamoja na hayo jeshi la polisi kazi yao ni kukanusha tu, nchi sio salama tena kwa raia wake?
 
Kila siku watu wanapotezwa, pamoja na hayo jeshi la polisi kazi yao ni kukanusha tu, nchi sio salama tena kwa raia wake?

Kama Raia tukiendelea kuwa kimya basi tutapoteza maelfu na maelfu ya watanganyika, na tusipokuwa na uchungu na wenzetu wanaotekwa na kupotezwa, basi ni wazi kuwa hili halitakuwa Taifa tena
Amewahi kuikosoa serikali ya bibi ..?
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida lakanusha taarifa zinazozambaa kuwa limemkamata na kumshikilia Shekhe Zuberi Nkokoo (53) mwalimu wa dini ya Kiislam kutoka Taasisi ya Islamic Foundation ambaye aliripotiwa kupotea Juni 02, 2025 majira ya saa 5:30 usiku akiwa karibu na Sheli ya Lake Oil iliyopo Mtaa wa Misuna, Manispaa ya Singida.

Jeshi la Polisi Singida linaendelea kufanya uchunguzi wa kubaini mahali alipo mtu huyo ili kujua kama amekamatwa au ameshikiliwa, mhusika ni nani na sababu za kushikiliwa kwake.

Aidha, Jeshi la Polisi Singida linawashikilia watu watatu kwa mahojiano ambao ni Abdul Ally (58), Mfanyabiashara na Mkazi wa Muriet mkoani Arusha, Shabani Ramadhani Ikenga (54), Mfanyabiashara na Mkazi wa Kisaki Manispaa ya Singida, na Maulid Mussa (52), Mfanyabiashara na Mkazi wa Muriet mkoani Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linawataka wananchi kupuuza taarifa za uzushi na za uongo zinazozenezwa kwa nia ya kuleta taharuki kwa jamii na badala yake watoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kubaini wapi alipo kiongozi huyo wa dini.

View attachment 3358145
Tatizo jeshi la police haliaminiki tena
 
Tumezidi useng£ ,watu muanze kumiliki silaha aisee ,haya mambo ya kubebwa kikondoo ni ufala ,hawa mbwa wa ccm bado wana njaa kali na damu zenu
 
Watu wawe kama zakaria , wakija ******* kuteka ,we tengua viuno vyao kamama£ zao waende wakasimulie vizazi vyao
 
Ifike hatua jeshi lijishtukie. Haiwezekani kila siku wao hawaelewi nini kinaendelea
 
Back
Top Bottom