Jeshi la Polisi lapewa siku 90 kuhakikisha mitambo ya LUGUMI inafanya kazi vituo vyote

Ishu ya mkataba kusainiwa siku moja baada ya zabuni kutangazwa sio hoja?? Mbona wanacheza na akili zetu hawa watu??
 
Sasa tumuamini nani, CAG anasema kazi haijafanyika, Rubber Stamp bunge linasema kila kitu kiko sawa.
 
Usishangilie upuuzi wewe .... hio ni pesa yetu sote. hivi watu wengine sijui akili zenu mnaweka wapi aiseee, shame on you, mnaleta siasa hata kwenye mambo ya muhimu....

Utawangwa na kichwa chagua watu wa kuwajibu. Ignore these Lumumba kids
 

Kali zaidi ni kuwa polisi wanenda kujichunguza wenyewe walete majibu kwa bunge. Hapo hapo vimeishatumwa vyombo viwili kufanya uchunguzi na hizi zote zimetumia rasilimali nyingi bila sababu ya maana. Yote hiyo tualipia kwa kodi zetu zilizooongezwa mara dufu. Hapa kazi tu!
 
Naibu Spika amepokea lini Ripoti ya Kamati na ripoti kujadiliwa? Ama kweli...

Mzee Tupatupa
Haya ndiyo yale yale mambo ya akina Jecha.

Utashangaa kwanini wanazungumza kijuujuu tu, badala ya kutupa details za kwamba vifaa vilifungwa lini, na kwanini havifanyi kazi?
 
"Siyo kila jipu ni la kutumbua tu!" Eti mtu anajidai mfia maslahi ya wananchi wa Tanzania, kwa mtindo huu???? Bora watu wanyamaze tu wasije wakamkasirisha MUNGU!!
 
Roho yangu ina maumivu makali sana kwa haya yanayotendeka, kama vile moto ulio fungwa ndani ya mifupa yangu. Nami nimechoka kwa maumivu.
 
Kwanini? wewe ulikuwa una imani na zile taarifa za magazeti uchwara walizokuwa wakilipuka nazo akina Lema?
Kwa aibu hii, ningekuwa nisinge thubutu hata kupost huu uzi hapa jukwaani.
 
Hongera Mh Kitwanga , Hongera Said .
 
hahahaha game over...

Maisha ya Tanzania sasa hivi nayalinganisha na TV series ya game of thrones.

Kila kitu drama drama, utendaji ni fairy tale.

Wacha movie iendeleeee: mie tukutane 2020 kwenye box la kupigia kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…