Jeshi la Polisi lapewa siku 90 kuhakikisha mitambo ya LUGUMI inafanya kazi vituo vyote

Jeshi la Polisi lapewa siku 90 kuhakikisha mitambo ya LUGUMI inafanya kazi vituo vyote

Ishu ya mkataba kusainiwa siku moja baada ya zabuni kutangazwa sio hoja?? Mbona wanacheza na akili zetu hawa watu??
 
Sasa tumuamini nani, CAG anasema kazi haijafanyika, Rubber Stamp bunge linasema kila kitu kiko sawa.
 
Usishangilie upuuzi wewe .... hio ni pesa yetu sote. hivi watu wengine sijui akili zenu mnaweka wapi aiseee, shame on you, mnaleta siasa hata kwenye mambo ya muhimu....

Utawangwa na kichwa chagua watu wa kuwajibu. Ignore these Lumumba kids
 
Ni pure siasa za usanii....

Sasa ndiyo naanza kuelewa alikuwa na maana gani huyo Lugumi alipotamba siyo kila jipu Magu ana uwezo wa kulitumbua.......

Hivi kwa mwendo huu wa Bunge la mfumo wa Chama kimoja la huyo mdada, ni nani atathibitisha kama mashine hizo zimefungwa?

Na Je ni sheria gani ya nchi hii inayoruhusu mwizi arejeshe mali akizoiba halafu ataachiwa huru?!

Kali zaidi ni kuwa polisi wanenda kujichunguza wenyewe walete majibu kwa bunge. Hapo hapo vimeishatumwa vyombo viwili kufanya uchunguzi na hizi zote zimetumia rasilimali nyingi bila sababu ya maana. Yote hiyo tualipia kwa kodi zetu zilizooongezwa mara dufu. Hapa kazi tu!
 
Naibu Spika amepokea lini Ripoti ya Kamati na ripoti kujadiliwa? Ama kweli...

Mzee Tupatupa
Haya ndiyo yale yale mambo ya akina Jecha.

Utashangaa kwanini wanazungumza kijuujuu tu, badala ya kutupa details za kwamba vifaa vilifungwa lini, na kwanini havifanyi kazi?
 
Sasa nadhani walioshindwa kumuelewa GADO kwenye hii cartoon sasa watapata mwanga...!

April.28.16.Magufuli.and_.the_.Boil_.jpg


Ni swala la aina ya jipu na mahali lilipo!​
 
"Siyo kila jipu ni la kutumbua tu!" Eti mtu anajidai mfia maslahi ya wananchi wa Tanzania, kwa mtindo huu???? Bora watu wanyamaze tu wasije wakamkasirisha MUNGU!!
 
Roho yangu ina maumivu makali sana kwa haya yanayotendeka, kama vile moto ulio fungwa ndani ya mifupa yangu. Nami nimechoka kwa maumivu.
 
Ni baada ya Kamati ya Bunge iliyopewa kazi ya kufuatilia Sakata la Lugumi kuthibitisha kuwa vifaa mashine hizo zimefungwa katika vituo vyote.

Agizo hilo limetolewa na Bunge kupitia kwa Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson wakati akiahirisha Bunge la 11 leo mjini Dodoma
==========



Habari wakuu,

Leo akihitimisha bunge, naibu spika ametolea ufafanuzi utekelezaji wa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa alama za vidole(AFIS), hoja iliyojengwa kutokana na mkaguzi wa hesabu za serikali(CAG) kwa kutokamilika kwa mradi huo.

Agizo la bunge lilimtaka afisa masuhuli wa jeshi la polisi kuhakikisha mfumo wa AFIS unafanya kazi ndani ya kipindi cha miezi sita. Ripoti ilieleza mfumo wa AFIS ulikuwa unafanya kazi katika vituo 14 pekee kati ya vituo 108 hivyo agizo la kamati halikuwa limetekelezwa kikamilifu.

Spika ametoa agizo kwa serikali kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi ndani ya miezi mitatu ili kuboresha uwezo wa jeshi la polisi kuwa na utambuzi wa haraka wa wahusika wa matukio ya kihalifu katika vituo vyote nchini. Pili masuala yote yaliyobainika kuwa na dosari za kiutendaji yapatiwe ufumbuzi haraka.

Spika anatarajia sasa suala hilo litafikia mwisho na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali atafunga hoja yake baada ya kujiridhisha na utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa.

Hongera Mh Kitwanga , Hongera Said .
 
hahahaha game over...

Maisha ya Tanzania sasa hivi nayalinganisha na TV series ya game of thrones.

Kila kitu drama drama, utendaji ni fairy tale.

Wacha movie iendeleeee: mie tukutane 2020 kwenye box la kupigia kura.
 
Back
Top Bottom