Jeshi la Polisi lapewa siku 90 kuhakikisha mitambo ya LUGUMI inafanya kazi vituo vyote

Jeshi la Polisi lapewa siku 90 kuhakikisha mitambo ya LUGUMI inafanya kazi vituo vyote

Ñchi hii hata wezi wa fedha nyingi hadi billioni 37 wanapewa muda wa kuficha wizi wao kwa kuruhusiwa kupandikiza kompyuta mbovu hivi hivi kadamnasi. Nani alichota pesa ya Lugumi? Iweje mtu aliyefunga kompyuta 14 tu katika miaka mi 3 aweze kufunga mifumo madhubuti ya kompyuta 98 ndani ya siku 90? Aliyehamisha hela kupitia mradi wa Lugumi atajwe.
Mtumbua majipu anatumbua vidagaa ma papa kama lugumi yanapewa muda ila engineer manispaa anatumbuliwa mbele ya waandishi wa habari
 
Eeh Mungu wangu. Nimegundua kwa nini vikundi vya kigaidi hujitokeza, nimegundua ni kwanini yule kijana wa Kiarabu alijichoma Moto mbele ya ofisi za Serikali, nimegundua ni kwa nini mtiifu wa ccm anaweza kujiunga Chadema, nimegundua kwa nini anataka aombewe. Jamani issue ya Lugumi ndo imeisha hivi hivi bila mtu kutiwa hatiani!!!?? Kweli? Nchi inaenda wapi? Mbona sioni tofauti ya JK na JPM? Mungu bora uiangamize Taifa hili tujue moja. Izame kama gharika.
Sema aingamize tahasisi ya CCM
 
Naibu Spika amepokea lini Ripoti ya Kamati na ripoti kujadiliwa? Ama kweli...

Mzee Tupatupa

Nchi yetu imekuwa ya watu waongo tu. Kuanzia Rais, watendaji wakuu wa serikali, wabunge, wakurugenzi, wakuu wa mikoa n.k hakuna anayetwambia ukweli. Wabunge mpaka wamefikia hatua ya kutoa mpaka matusi ya nguo bungeni, yaani inasikitisha sana. Siku viongozi hawa nasi wananchi wa kawaida tukianza kuwaambia uongo na kuwatukana wasitushangae. Kama kiongozi mkuu ambaye ni kioo cha jamii unaamua kusema uongo na kutukana, unategemea nini kutoka kwa wananchi. Mifano ipo mingi, JK alitudanganya ESCROW siyo pesa za serikali, Waziri Mkuu wake naye vilevile. Serukamba katumia neno F.U.C.K YOU bungeni. Kubenea kadanganya kuhusu Dk. Hussen Mwinyi na Mikataba ya ujenzi wa nyumba za JWTZ. n.nk Waziri Mkuu Majaliwa naye kadanganya kuwa wananchi hawana mamlaka ya kuihoji serikali. Mhhhh, Mwingine anasema ni Rais wa Wanyonge ili hali wanyonge hao hao anawakamua mpaka watoke damu badala ya jasho kwa kuwapandishia kodi kila nyanga. Jamii yetu ni shida tu Mkuu.
 
Kwanini? wewe ulikuwa una imani na zile taarifa za magazeti uchwara walizokuwa wakilipuka nazo akina Lema?
Kuna baadhi ya vituo baada ya issue kubumbuluka jamaa wamekimbia kufunga dell mbovu haraka haraka!CAG alipokagua hali halisi ilikuwa hivyo!
Tunajua mchezo uliofanyika!
 
MKATABA tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara Said Lugumi, umezidi kuchukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kushindwa kuendelea na sakata hilo kutokana na kuhamishiwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Hatua hiyo inatokana na utata uliogubika mkataba huo ambao unawahusisha vigogo kadhaa wa Jeshi la Polisi pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, huku ikidaiwa kuwa huenda ikawa njia ya ‘kulindwa’.

Wiki iliyopita PAC ilipokutana na jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ilibainika kuwa mwaka 2011 liliingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37.
Lakini hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 pekee na kampuni hiyo kulipwa Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha za makubaliano ya mkataba.


Kutokana na hali hiyo, PAC ambayo ilibaini kuwapo viashiria vya ufisadi katika tenda hiyo, iliwaagiza watendaji wa jeshi hilo kuwasilisha taarifa za mkataba huo pamoja na vielelezo vyake ili wajumbe waweze kuupitia pamoja na kutoa maagizo.

Chanzo cha kuaminika kiliambia MTANZANIA kuwa katika sehemu ya mkataba huo kati ya Jeshi la Polisi na Lugumi, imebainika kampuni hiyo kufanya mafunzo kwa watu watano ambayo wametumia Sh bilioni 5, huku mshauri mwekelezi akilipwa Sh bilioni 46 nje ya fedha zilizopo kwenye mkataba.

Hatua ya mkataba huo kupelekwa mbele ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, inadaiwa kuwa njia ya kutaka kuwalinda baadhi ya vigogo ambao wanatajwa kuhusika na kashfa hiyo ambayo imelitia doa Jeshi la Polisi nchini.
“Hapa kuna kulindana tu, hakuna namna yoyote. Kama uchafu umebainika mbele ya Kamati ya PAC inakuwaje wengine wanadaka kitu ambacho hakikuanza kwao?

“Kuna kila dalili ya wingu na shaka, ila ukweli utajulikana tu, haiwezekani watu wanatumia fedha za walipakodi vibaya halafu inapokuja wanataka kushughulikiwa wanatafuta kivuli cha kujifichia,” kilisema chanzo chetu.
Mkataba huo uliibuliwa na PAC wiki iliyopita ambapo watendaji wa Jeshi la Polisi walishindwa kutoa maelezo ya kutosha ndipo ikawataka kuwasilisha taarifa juzi.
Pamoja na kutakiwa kufanya hivyo, hadi kufikia jana saa 10 jioni Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly, alisema kuwa kamati yao haijapokea taarifa yoyote kuhusu Kampuni ya Lugumi hivyo wameliandika barua Jeshi la Polisi liwasilishe mkataba huo ndani ya siku tatu.

Alisema barua hiyo wamemuomba Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, ili aweze kuwaandikia Polisi ili wawasilishe mkataba huo kwa mujibu wa utaratibu kama kamati ilivyoagiza.
“Hadi muda huu ninapozungumza nawe sijapata taarifa yoyote, kwa hali hiyo tumelazimika kumwandikia barua Katibu wa Bunge ili awaandikie barua polisi walete mkabata huo ndani ya siku tatu kutoka leo (jana) kama walivyotakiwa na kamati yetu,” alisema Hilaly.

BALOZI ADADI
Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu, alithibitisha mkataba huo kuwasilishwa mbele ya kamati yake.
“Mimi kama mwenyekiti wa kamati ninapenda kukiri kwamba tumepokea mkataba kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi na tutaufanyia kazi kwa kina.

“Tunahitaji kuona kama kuna wizara zilizohusika na mkataba huu na kama tutaukuta ni mbaya, tutatoa taarifa kwa umma. Kikubwa tunawaomba Watanzania wawe watulivu, hatuko kwa ajili ya kumlinda mtu wala kikundi cha watu, tunasimamia masilahi ya Watanzania wote,” alisema Balozi Adadi.

Source: Mtanzania
 
Mtoto lugumi anadekezwa kakosea kachelewesha maaendeleo. Kaambiwa tuuu afanye correction. Ila angekuwa mtoto mwingine kwa taritabu za shule yetu angekuwa kashapewa adhabu ya kutumbuliwa
 
Lugumi ni sawa na jiwe la mtoni....ukikanyaga lazma uteleze mtumbuaji nae kahanya kwa mwendokasi kabakia kimya tuli....hizi sample za wasukuma lugumi na chenge zinaogopwa sana
 
Tangia mwaka 2011 bado hawajamaliza installation? kampuni ya Lugumi ishitakiwe kwa kukiuka mkataba wa kazi.
 
Ni uozo wa hali juu. Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali anafanya kazi yake ya kukagua hesabu mbali mbali za taasisi za Serikali na kugundua ufisadi mkubwa sana wa shilingi bilioni 37. Halafu huyu jipu Tulia akishirikiana na Serikali dhalimu wanachakachua kazi ya CAG na kudai mashine zimefungwa katika vituo vyote 108 wakati CAG aligundua ni vituo 14 tu.

Ufisadi hautaisha Tanzania.

Hivi hiyo ripoti ilijadiliwa lini?

Bunge llimepwaya sana hili hadi kinyaa.
 
Ni kitu cha kustaajabisha sana Mkuu. Ilikuwa ni ufisadi tu hivyo wakatunga vituo 14 kati ya 108. Wakaingia mitini kwenda kutafuna mabilioni yao. Baada ya ripoti ya CAG ndiyo wakaenda kununua mashine nyingine mwaka huu ili kuchakachua ripoti ya CAG. Magufuli ni janga kubwa la Taifa.

Tangia mwaka 2011 bado hawajamaliza installation? kampuni ya Lugumi ishitakiwe kwa kukiuka mkataba wa kazi.
 
Wanastaajabisha sana hawa watu, labda wanadhani ni pesa ya CHADEMA/UKAWA.

Usishangilie upuuzi wewe .... hio ni pesa yetu sote. hivi watu wengine sijui akili zenu mnaweka wapi aiseee, shame on you, mnaleta siasa hata kwenye mambo ya muhimu....
 
“A thief is a man who steals in
ways that are not customary. He takes a loaf of
bread from a baker's window and, straight away,
we run him into jail. Another steals the bread
from the mouths of millions of women and
children he rigs votes to win parliament sit.
 
Iba kuku uone halafu analalamika dpp alichezea kesi ya samaki wakat wote ni wazee wa magoli ya mkono
 
Hivi hawa wanaitakia nini nchi hii? Haya majibu yasiyokidhi na kulandana na maswali yaliyoulizwa?

Walifanya vitimbwi vya kuudhi kipindi cha mchakato katiba mpya wawakilishi wa upinzani wakato...wamefanya tena hivyo wakati huu...now I know haya yote yanafanyika ile upuuzi huwe unapitishwa pasipo upinzani.

Huyu mtetea wanyonge akikaa kimya ujue ccm ni ile ile tu...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom