Ni uozo wa hali juu. Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali anafanya kazi yake ya kukagua hesabu mbali mbali za taasisi za Serikali na kugundua ufisadi mkubwa sana wa shilingi bilioni 37. Halafu huyu jipu Tulia akishirikiana na Serikali dhalimu wanachakachua kazi ya CAG na kudai mashine zimefungwa katika vituo vyote 108 wakati CAG aligundua ni vituo 14 tu.
Ufisadi hautaisha Tanzania.
BAK soma hii
Utetezi wa Polisi sakata la Lugumi huu hapa
CAG ajiuzulu maana inaonekana kasema 'uongo'
Tenda ilitangazwa lini? Mzabuni alipataikanaje?
Miaka 3 mzabuni kalipwa 99%.
Kazi haijafanyika kwa mujibu wa Naibu Spika
a) Hao waliozemebea ni akina nani na wamechukuliwa hatua gani?
b)Pesa za kukamilisha zitatoka fungu gani,mzabuni keshamaliza kazi na kulipwa 99%
c)Kulikuwa na haja gani ya kuunda kamati kuchunguza kazi ambazo zipo chini ya wizara?
d)Kwanini taarifa haikujadiliwa na bunge?
e) Kulikuwa na sababu gani za kutupiana mpira ikiwa vituo vilikamilika?
f)Gazeti la Nipashe 22 April lilitoa taarifa ya Polisi ikisema vilivyofungwa ni 14 kati ya 108.
Gazeti kama lilisema uongo kwanini halichukuliwi hatua?
g) Kazi ya miaka 3 inakwishaje kwa miezi 3 na nini kilikwamisha
Tuliwambia danadana ilikuwa na mambo, mkadhani sisi ni wendawazimu
Hii ni kawaida ya CCM, na CCM ni ile ile. Huwezi kuzaa mtoto akakua na kubalehe kwa mila za Kingoni ukidhani siku moja atakuwa na mila za kibondei.
Lugumi kwisha, tuendelee kutumbua majipu na sasa mahakama ya mafisadi
Taarifa ya CAG inasema jambo moja
Taarifa ya Polisi (kwa mujibu wa gazeti hapo juu) inasema jingine
Taarifa ya Naibu Spika inazungumzia tukio tofauti kabisa
Hoja ni moja Lugumi, taarifa zinakinzana
CAG ajiuzulu maana katika hili sijui kama ana la kusema tena
''Yaliyopita si ndwele tugange yajayo''
Taratibu watatuelewa
The Boss Mag3 Nyani Ngabu BAK MsemajiUkweli Ngongo