Jeshi la Polisi lapewa siku 90 kuhakikisha mitambo ya LUGUMI inafanya kazi vituo vyote

Jeshi la Polisi lapewa siku 90 kuhakikisha mitambo ya LUGUMI inafanya kazi vituo vyote

Naibu Spika amepokea lini Ripoti ya Kamati na ripoti kujadiliwa? Ama kweli...

Mzee Tupatupa
Mkuu VUTA-NKUVUTE, huyo ni mwanasheria nguli aliyesaidia serikali kushinda kesi ya mita 100 kutoka kituo cha kupiga kura, atashindwaje kujua yaliyomo kwenye ripoti hata kama hajaipokea!? Tanzania ina vichwa we acha tu.
 
Ni pure siasa za usanii....

Sasa ndiyo naanza kuelewa alikuwa na maana gani huyo Lugumi alipotamba siyo kila jipu Magu ana uwezo wa kulitumbua.......

Hivi kwa mwendo huu wa Bunge la mfumo wa Chama kimoja la huyo mdada, ni nani atathibitisha kama mashine hizo zimefungwa?

Na Je ni sheria gani ya nchi hii inayoruhusu mwizi arejeshe mali akizoiba halafu ataachiwa huru?!
Ni pure siasa za usanii....

Sasa ndiyo naanza kuelewa alikuwa na maana gani huyo Lugumi alipotamba siyo kila jipu Magu ana uwezo wa kulitumbua.......

Hivi kwa mwendo huu wa Bunge la mfumo wa Chama kimoja la huyo mdada, ni nani atathibitisha kama mashine hizo zimefungwa?

Na Je ni sheria gani ya nchi hii inayoruhusu mwizi arejeshe mali akizoiba halafu ataachiwa huru?!

Sasa nimeamini bunge letu tukufu
sio la wananchi tena, wala sio mihimili unaojitegemea!!
Haiwezekani watu wachezee fedha zetu kama LUGUMI
eti wanapewa siku tisini wafunge mashine!!
Ndio maana wabunge wa upinzani hawaruhusiwi kutoa hoja, bunge limetekwa kazi kwisha!!
Watanzania hakuna pa kusemea, nasikia hata wezi wa IPTL (ESCROW) wametengewa fedha wazalishe umeme wa gesi!!
 
Issue ya kutumbua majipu imekufa rasmi sasa. Inabidi kila "mtuhumiwa" sasa awe anapewa miezi mitatu kurekebisha madudu yake kwanza kabla ya kuwekwa pembeni.

Wabunge badala ya kuomba miongozo kwa issue zenye maslahi mapana kwa taifa, wanakomaa na trivial issues kama kulitaka Bunge lijadili kwa nini aliyemwita bwege mtu flani amechangisha fedha mbele ya camera za waandishi wa habari.
 
Hii ni sawa na kumsihi mwenye dhambi atubu kabla ya kifo chake.Sasa ninaanza kuamini kwamba LUGUMI zi zaidi ya tunavyomzungumzia na kumfahamu.
 
Nani amguse lugumi ...ameongezewa muda aendelee kumalizia pesa zake....
 
Usishangilie upuuzi wewe .... hio ni pesa yetu sote. hivi watu wengine sijui akili zenu mnaweka wapi aiseee, shame on you, mnaleta siasa hata kwenye mambo ya muhimu....

Nimeupenda mno mchango wako ila ungependeza zaidi ungewashauri wanaokimbia bungeni kusisitiza hoja yako ndani ya bunge ili kuwa na tija ya uwepo wa wapinzani.Dr.Tulia amefanya kilichopaswa kufanywa na upande wa pili wanaopendekeza aondolewe.Akiondolewa na wao wapo mitaani wanatafuta idhini ya kuandamana nani atatutetea?
 
Tarehe 23 April 2016, PAC iliomba Kuunda kamati ndogo kwa mujibu wa Kanuni ya 117 fasili 18 ili kufuatilia utekelezaji wa Agizo la PAC la bunge la 10 lililotolewa tarehe 23.10.2014 kwa Jeshi la Polisi Kuhusu utekelezaji wa Mradi wa kielektroniki wa utambuzi wa alama za vidole AFPIS

Msingi wa Agizo ni Ripoti ya CAG 2012/2013 kutokana na kutokukamilika na kutokufanya kazi ipasavyo kwa mradi huo.

Kazi ya Mradi huo ilikuwa ni kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya LUGUMI ENTERPRISES LIMITED.
Polisi waliagizwa Mitambo ifanye kazi ndani ya miezi sita.
CAG aliripoti tena utekelezaji kuwa AFPIS inafanya kazi katika vituo 14 tu kati ya vituo 108

Kamati ilimtaka katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani alete taarifa ya utekelezaji. Katibu mkuu taarifa yake ikaonyesha mitambo imefungwa vituo 153 pamoja na makao makuu ya polisi tofauti na taarifa ya CAG ilivyosema. Kamati ikaomba kuhakiki kujiridhisha na kujionea, na kamati ndogo ikaundwa kuhakiki.

HADIDU REJEA – kamati ifanye uhakiki iwapo vilinunuliwa na kufungwa
kamati imemaliza kazi yake, Imeiwasilisha PAC na PAC imeijadili na kuikabidhi kwa Spika kama Kanuni zinavyotaka.

MATOKEO YA TAARIFA YA KAMATI
i. Kamati imejiridhisha kwamba VIFAA VIPO Vituo vyote 153 na makao makuu ukiacha kasoro zilizojitokeza.

ii. Kilichobaki ni vifaa hivyo kufanya kazi

iii.Nimekabidhi matokeo (maoni, Ushauri na mapendekezo) yote ya kamati kwa serikali
AGIZO

i. Serikali ihakikishe mfumo huu unafanya kazi ndani ya Miezi mitatu kutoka leo hii ili kuboresha uwezo wa jeshi la polisi.

ii. Maswala yote yaliyobainika kuwa na dosari za kiutendaji yapatiwe ufumbuzi haraka.


iii. PAC ihakiki maelekezo niliyoyatoa na baada ya uhakiki kamati itoe taarifa bungeni wakati wa uwasilishaji wa taarifa yake ya mwaka.

iv. Ninatarajia sasa swala hili litafika mwisho na CAG atafunga hoja yake baada ya kujiridhisha utekelezaji wa maagizo niliyoyatoa.
 
mhhhh! haya bhana, sisi wengine tulishaufyata mkia kitambo.Tunaogopa kuwa wachochezi, hvyo no comments from me.
 
Ccm ni ileile ooh ni ileile tumejipanga mwaka huu wataisoma.........
 
Huu ni upuuzi wa hali ya juu sana!! Kinachoonekana kipo wazi na mambo haya yanafanyika katika nchi ya watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri!!.Ipo siku Mungu atatujalia kuwa na ufahamu mkubwa ndio tutagundua na kutambua ubaya wa haya yote yanayoendelea nchini.
 
Tatizo la wana chadema ni kujifanya mnajua kila kitu.

Ila naomba mbakize akiba ya maneno maana 2020, LUGUMI anaweza kugombea urais kupitia chadema baada ya gia kubadilishwa angani na mfalme Mbowe.
 
Back
Top Bottom