DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Jeshi la Polisi limewashikilia Vijana 8 kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya uhalifu ikiwemo unyang'anyaji kwa kutumia nguvu na silaha za jadi katika operesheni maalum iliyofanywa na Jeshi hilo hivi karibuni
Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa vijana hao Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi SACP Richard Thadei Mchomvu amesema miongoni mwa hao 8, Watatu ni Vijana waliohusika katika tukio liloripotiwa Mei 27, 2025 majira ya saa tano usiku na Nassor Suleiman Nassor aliyeripoti katika kituo cha Polisi Mazizini Zanzibar
Aidha, amesema kumekuwepo kwa video ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha vijana ambao wamejivisha mabaibui kufanya wizi ambapo amesema video hiyo haikuwa Zanzibar ila Operesheni iliyofanywa ilibaini pia njia ya kuvaa kwa mabaibui hutumika pia kwa vijana wanaofanya uhalifu huo hapa Zanzibar
Akiwataja Vijana watatu waliokamata katika operesheni hiyo ambayo walihusika na tukio la kushambuliwa kwa Ndugu Nassor ni pamoja na Mohamed Saha Khamis miaka 17, Fahad Ali miaka 16 na Ali Sufiani Rashid miaka 22 wote wakazi wa Kisauni Zanzibar