Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Acha uhuni wewe. Yule mhalifu alionyeshwa vyote na alijua ni polisi lakini alikuwa akigoma kupanda kwa sababu alijua mwisho wake wa uhalifu umefikia tamati.
Polisi ndio wanakamata watu kwa mtindo huo siku hizi?

Mtu aonyeshwe kitambulisho agome?

Angalia hao askari[vibaka] walivyovaa kichekibobu kuna mtu atakubali kukamatwa nao kirahisi?
 
Huyo mhalifu alionyeshwa kila kitu na alikuwa amewakimbia polisi kabla ya kudakwa. Hata yeye anajua ni mhalifu na ndio maana alikuwa analeta ubishi. Si unaona alikuwa haweki hata namba ya usajili wa pikipiki yake kwa ajili ya kuficha uovu wake kutojulikana.
 
Polisi ndio wanakamata watu kwa mtindo huo siku hizi?

Mtu aonyeshwe kitambulisho agome?

Angalia hao askari[vibaka] walivyovaa kichekibobu kuna mtu atakubali kukamatwa nao kirahisi?
Tena huyo mhalifu wamemsamehe sana maana alikuwa anakimbia na kukataa kutii amri hata pale alipoonyeshwa vitambulisho vyote. Inatakiwa wamfinye sanaa ili ataje na wenzake na kurudisha vitu alivyoiba kwa watu.
 
Nimeishi brazil huko polisi wa bongo wanasubiri jnsi wanavyo deal na wahalifu
Maana polisi wenyewe nao wanafanyiwqga sana na wahalifu
Ndomana polisi nao wamebidi kuwa aggressive ku deal na wahalifu

Ova
Ni matokeo ya kuishi kwenye jamii ya Wakatiri......maana Unakita Polisi nao ni wahalifu sasa wahalifu kwa wahalifu wakikutana nini kinatokea?
 
Acha kuharisha hapa. Nenda Kibaha kamwekee dhamana.
 
Watu kila siku wanatekwa na kuokotwa wameuawawa.
Shida yako Lucas unafanya siasa kwa kila jambo.

Hakuna anayetetea uhalifu ndio maana tunajadili hili jambo.

Kwa mazingira ya sasa ambapo utekaji na mauwaji yamekithiri ni ngumu sana kumwamini huyu mtu ni Mamlaka ya Serikali eti kwa sababu ya makaratasi tu ya vitambulisho.

KInyume na hapo hakuna sababu ya sheria za ukamataji kuwekwa. Kama hazifatwi. Polisi walishakiri kwamba wakitumia taratibu za kisheria inashindikana?
 

Huo ni Utekaji Wala siyo Ukamataji.

Huyo Askari Polisi aliyetoa taarifa hii amefanya hivyo baada ya kuona kwamba Wananchi wamewashitukia
 
Huyo mhalifu alionyeshwa kila kituo na mbaya zaidi alikuwa amewakimbia. Huyo mhalifu anajua kila kitu anachokifanya
 


Sio uhalifu wa kimtandao kwa kuikosoa SERIKALI ya CCM ?
 
Mzee kibao alitii sheria bila shuruti yuko wapi??
 
Leo hili limepita salama watu wamepongeza, ila wale jamaa wasiojulikana mjue wamepata point ya kuendeleza ubaya ubwela. Watakuja wanasema wao ni police, na km kawaida yao wanakuchukua ndo inakuwa kwa heri.

Police wanatakiwa wawe na uelewa wa hali ya wakati husika. Kwa mtu aliosoma na hali ya tahadhari iliyopo kwa sasa huwezi kuvaa bukuta ukaja kimkamata mtu tena na gari la kiraia. Surely, ingekuwa usiku na huyo jamaa akapiga kelele kuwa anatekwa hawa police sasa hivi huenda tungekuwa tunaongea mengine. Km maofisa wa TRA hawakuacha kumbukumbu kwa watendaji wa serikali, basi yajayo yatafutahisha.
 
Weledi wa polisi ni zero kabisa.kama ni mhalifu wangesema kabisa kuwa wao ni polisi wa kituo Fulani ili kuondoa taharuki.Na wawe wanavaa ngua zao rasm.wanaukamataji wa kishamba sana
Polisi unavaaje pensi vile au inaruhusiwa na wanatumiaje gari ya aina ile maana magari yao yanafahamika
 
Siyo Polisi wote wanaokuwa katika unifom .wengine hawavai kwa ajili ya kuwezesha shughuli mbalimbali za kipolisi kufanyika kwa mafanikio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…