Huyo ni mhalifu wa kupora watu vitu vyao.
Ukamataji wa namna ile mahakamani hauwezi kumshinda labda wamuue .
Hakua na silaha yoyote hivyo hawakuwa na sababu ya kumkamata kwa namna ile .
Kwa ushauri tu ni bora wangeenda na askari wawili waliovaa uniform wanaofahamika . Wakae ndani ya gari kama walivyoenda na gari la kiraia kama mbinu yao lakini baada ya wale manjagu waliovaa kiraia kumkamata na kuanda kusumbua na nao basi wale walivaa unifaomu wangeshuka na silaha zao na kumkamata na alikaidi wanauwezo wa kumpelekea moto na kumvunja miguu bila kuvunja sheria na ukamataji ungekuwa halali kabisa .
Lukas hii nchi ina sheria mkuu . Hata kama kuna watawala wasiotaka kuzifuata lakini zipo na kuna siku wasoozifuata wataitwa wahalifu.
Uhali unafanyika pale ambapo mtu yeyote hataki kufuata sheria .
Hata ukamataji usiofuata sheria ni uhalifu na ukiukwaji wa haki za binadamu .
Ule ukamataji ikitokea baadae wakagundua kuwa sio yeye waliokua wanamtafuta itakuaje kama sio kuleta hasara kwa mtu na kwa serikali .
Watuhumiwa Wauporaji wa mali za umma hawakamatwi na hata wakikamatwa wanakamatwa kwa heshima kubwa na hata kupongezwa kwa kuiba mali za umma na kujilimbikizia mali na mara nyingine wanasifiwa kwa kuambiwa kuwa wametulia vizuri urefu wa kama zao .
Hatukatai wahalifu kukamatwa lakini wakamatwe na askari wanaofahamika .
Mtu anaendesha bodaboda unasemaje kuwa anajifucha wakati yupo kijiweni na kijiwe chake kipo eno lenye utawala wa kituo cha polisi kinachokuwa jirani .
Akamatwe awekwe kizuiani na kufikishwa mahakamani .
Wazuie dhamani yake kama Dr.Slaa ili asilete taharuki ya kupora wetu.😂😂😂