Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Huyo ni mhalifu wa kupora watu vitu vyao.

Ukamataji wa namna ile mahakamani hauwezi kumshinda labda wamuue .

Hakua na silaha yoyote hivyo hawakuwa na sababu ya kumkamata kwa namna ile .

Kwa ushauri tu ni bora wangeenda na askari wawili waliovaa uniform wanaofahamika . Wakae ndani ya gari kama walivyoenda na gari la kiraia kama mbinu yao lakini baada ya wale manjagu waliovaa kiraia kumkamata na kuanda kusumbua na nao basi wale walivaa unifaomu wangeshuka na silaha zao na kumkamata na alikaidi wanauwezo wa kumpelekea moto na kumvunja miguu bila kuvunja sheria na ukamataji ungekuwa halali kabisa .

Lukas hii nchi ina sheria mkuu . Hata kama kuna watawala wasiotaka kuzifuata lakini zipo na kuna siku wasoozifuata wataitwa wahalifu.

Uhali unafanyika pale ambapo mtu yeyote hataki kufuata sheria .
Hata ukamataji usiofuata sheria ni uhalifu na ukiukwaji wa haki za binadamu .
Ule ukamataji ikitokea baadae wakagundua kuwa sio yeye waliokua wanamtafuta itakuaje kama sio kuleta hasara kwa mtu na kwa serikali .

Watuhumiwa Wauporaji wa mali za umma hawakamatwi na hata wakikamatwa wanakamatwa kwa heshima kubwa na hata kupongezwa kwa kuiba mali za umma na kujilimbikizia mali na mara nyingine wanasifiwa kwa kuambiwa kuwa wametulia vizuri urefu wa kama zao .

Hatukatai wahalifu kukamatwa lakini wakamatwe na askari wanaofahamika .
Mtu anaendesha bodaboda unasemaje kuwa anajifucha wakati yupo kijiweni na kijiwe chake kipo eno lenye utawala wa kituo cha polisi kinachokuwa jirani .
Akamatwe awekwe kizuiani na kufikishwa mahakamani .
Wazuie dhamani yake kama Dr.Slaa ili asilete taharuki ya kupora wetu.😂😂😂
 
Ulitaka akamatwaje mtu anayekaidi amri halali ?
Wewe ujinga ulionao ni beyond repair nilikuwekea link ya YouTube yenye clip ya huyo kijana akisimulia kuanzia mwanzo ilikuwaje, hujaisikiliza umedandia kureply hapa

Hopeless kabisa.
 
Kama wewe ni mhalifu nakusihi uache mara moja . Maana mkono wa serikali ni mrefu sana na utakufikia popote pale utakapokuwa.
Serikali ipi hiyo yenye mkono mrefu? Serikali hii hii ya Samia?
Mbona mpaka leo hawajawakamata wauwaji wa Mzee Kibao? Waliompiga risasi Lissu mpaka leo wana randa randa mjini!
 
Ujinga ni mzigo ndugu yangu. Kulikuwa na ubaya gani, polisi mmoja anawatangazia wananchi kuwa, "Ndugu wananchi sisi ni polisi msiwe na wasiwasi tunamkamata huyu ni mtuhumiwa" Halafu anatoa kitambulisho kuna ubaya gani?
muuguzi au daktari ambaye hana weled na ujuz huwa hajiamin na kaz yake na hutumia ukali kukueleza jambo.
 
Shida ya nchi yetu ni kwamba,
Polisi Wana magari yenye nembo ya POLICE sijui yanatumikaga wapi?
Wana uniform sijui zinatumikaga wapi?
Wana vitambulisho sijui vinatumikaga wapi?


Sasa wananchi wataacha kuwa na mashaka, tumeshuhudia vifo vingi kwa style za ajabu hivi hivi
📌huwezi elewa yasipokukuta haya
 
Serikali ipi hiyo yenye mkono mrefu? Serikali hii hii ya Samia?
Mbona mpaka leo hawajawakamata wauwaji wa Mzee Kibao? Waliompiga risasi Lissu mpaka leo wana randa randa mjini!
Yani Kuna machawa wanajifanya hawaoni haya brother.
Itabidi na machawa waanze kupotea aise nadhan itakuwa bomba
 
Back
Top Bottom