Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
- Thread starter
-
- #141
Upo sahihi kabisa haujawahi kuniangusha katika matumizi ya akili.Siyo kila mhalifu unamkamata na arrest warrant kuna wahalifu wengine washakata kamba
Wao tYRi wana arrest warrant ya juu kwa juu wakamatwe hai au wakiwa wamekufa
Ova
hv kati ya yule boda na hao watekaj wenu nan muharifu ? wanaua wapinzan mf Ally Kibao , Soka etc , wanapambana kuua demokrasia kwa kuzuia mikutano ya vyama visivyabiana na ccmu kimawazo mf Chadema , wanazuia maandamano ya kupaza sauti ya umma dhidi ya idadi kubwa ya watu kupotea na wengine kuokotwa maiti , Mauaji ya hadharani mf uchaguzi mdogo mwaka 2024 huko Kigamboni na Gongo la mboto , Ubinyaji wa haki za binadamu kuanzia namna wanavyotumika kubambikizia kesi wapinzan wa ccmu , wanapora mali za watu hasa polisi wa barabarani , wanahusika kuwakinga waharifu dhidi ya mkono wa dola , wamekuwa machawa wa ccmu na sio walInz wa jamii etcAcha kuwatetea wahalifu na uhalifu.
Embu acha utoto wako hapa. Yaani wewe kila siku unaunga mkono uovu tu Utafikiri na wewe ni mhalifu. Kwanini usiulize sababu ya yule wa pikipiki aliyekuwa anakamatwa kutokutii Amri?
Kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, mtu anawezw kukamatwa bila warrant pale anapokua anatenda kosa muda huo, (mfano anaiba au anabaka) au pale inapoaminika kuwa kuna warranty imetolewa juu ya kukamatwa kwake lakini haipo mikononi mwa mtu anayemuona huyo mhalifu (mfano warrant imetolewa mbeya na mhalifu anaonekana Mitaa ya Dar). Au warrant iliyochapishwa gazetini.Siyo kila mhalifu unamkamata na arrest warrant kuna wahalifu wengine washakata kamba
Wao tYRi wana arrest warrant ya juu kwa juu wakamatwe hai au wakiwa wamekufa
Ova
Lazima jamii na taifa kujenga utamaduni wa kufuata akili ya kawaida na sheria katika kuishi.Saidia mtu unayemjua
Mfano huyo angesema natekwa halafu wananchi hawamjui wakawashambulia na kuua hao polisi unajua nini kingewapata hao wananchi baadaye huyo mtu wakiambiwa alikuwa jambazi wakimkimbiza
Wao watahesabika sehemu ya huyo jambazi na kupewa kesi ya mauaji ya kuua polisi
Njia nzuri kwenye hilo ni kupiga simu polisi au kuripoti kituo cha polisi cha karibu au kwa mjumbe au kiongozi wa mtas hsraka haraka sana kwa simu au bodaboda anakimbia haraka kuripoti
Usichukue sheria mkononi hata apige kelele anatekwa
Taarifa zilikuwa zipo Rasmi kituo cha polisi na hata ndugu walipewa taarifa na kufahamishwa juu ya ndugu yao kushikiliwa na Jeshi la polisi.Mwashambwa, siyo kila kitu kinahitaji mihemuko. Namna mbaya ya utendaji kazi wa polisi, unayaweka hatarini hata maisha ya askari wenyewe. Hivi kuna ugumu gani kwa askari baada ya kumkamata na kumdhibiti mtuhumiwa, kiongozi wa operation kujitambulisha rasmi kwa watu waliopo, kwa kutaja jina lake, kuonesha kitambulisho chake, sehemu ambayo mtuhumiwa anapelekwa, na mtuhumiwa kupewa nafasi ya kuwajulisha jamaa zake wa karibu, kama mwongozo wa jeshi la polisi, unavyotaka?
Namna hii mbaya ya utendaji kazi wa polisi, kuna siku italeta maafa. Miongozo ya utendaji kazi ipo, lakini wanaipuuza.
Acha uhalifu kama wewe ni mhalifu.Mtadanganya wajinga Toka Mbozi huko.
Ndomana nkasema huyo ana warrant ya juu kwa juu !Kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, mtu anawezw kukamatwa bila warrant pale anapokua anatenda kosa muda huo, (mfano anaiba au anabaka) au pale inapoaminika kuwa kuna warranty imetolewa juu ya kukamatwa kwake lakini haipo mikononi mwa mtu anayemuona huyo mhalifu (mfano warrant imetolewa mbeya na mhalifu anaonekana Mitaa ya Dar). Au warrant iliyochapishwa gazetini.
General rule, lazima kuwe na warrant - kwa mhalifu konki kama huyo lazima wangekuwa na warrant hao mapolisi
Kila kitu kina sababu hata yule wa kiluvya kwenda kumteka ukweli anaujua mwenyewe bw tarimoNilijua itakuwa kati ya haya mawili
1. Mhalifu au
2. Hapeleki hesabu ya boss. Halafu boss mwenyewe mafia.
Waambie polisi waako wavae uniform, nextime tutasshindwa kuwatofautishaNdugu zangu Watanzania,
Jeshi letu la Polisi Nchini limetoa ufafanuzi wa kina juu ya video mjongeo iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikionyesha dereva bodaboda au mtu mwenye pikipiki akikamatwa na watu waliovaa kiraia nakisha baadaye kupakizwa kwenye gari nyeusi na kuondoka naye.
Jeshi letu la polisi limesema tukio hilo lilifanywa na askari wetu kwa mtu huyo ambaye alikuwa ni mhalifu wa makosa mbalimbali ya uporaji kwa kutumia pikipiki.
Kwa hiyo watanzania tuache mihemuko na lawama na kutupa maneno yasiyo na ukweli. Tuwe watu wa subira na kushirikiana na vyombo vyetu vya ulinzi kupata taarifa rasmi.
View attachment 3245354
Soma: Video: Mtanzania adaiwa kutekwa mchana kweupe huko Kibaha
Syo kila mhalifu kumkamata inabidi ufate sheria, kuna wahalifu wengine watukutu haambiliki hawasikii sheria zenyewe zimedunda kwaoooLazima jamii na taifa kujenga utamaduni wa kufuata akili ya kawaida na sheria katika kuishi.
Akili ya kawaida inahitaji mtu ujilinde ulinde wengine na ufuate sheria.
Sheria zimekataza maovu na kuweka taratibu za kufanya mambo au kudhibiti na kuwashghulikia waovu.
Kwa hiyo, katika kujilinda na kulinda wengine, wananchi wana haki ya k upambana hadi kuwadhibiti watekaji (ni muhimu wafundishwe hivyo, vinginevyo tutajenga taifa la majuha na makondoo).
Pia lazima sheria za ukamataji zifuatwe, ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu stahiki.
hv kwa matukio ya miaka hii 2 bado unakamata mtu namna ile ? hv ni kwel huyu boda boda ni tishio kias cha kumshika na mitutu ? mtu anaeomba msaada kwa raia ? Mzee kibao walimshika na mitutu tulipokaa kimya alikutwa wap ? hv hawa unawatetea wameua zaid ya watu 100 kweny mwaka uliopita ,unapata wap uhalali wa kushabikia namna hiyo ya ukamataj ? hv chuo cha polisi wanafundishwa nn ? mbona ukamataj huu haufanan na mtu aliyeend kozi za kijeshi , uvaaji pia ni kama panya road , watu wanafika 200 tangu mwaka 2023 hawajulikan walipo , Mdude wa chadema alishikwa hv hv na hatukujuwa alipo na hata kituo waliwekwa wenzio hadi kituo cha mkoa hakwepo , walienda mficha walipoona watu wamechachamaa ndo wakamuachiaSiyo kila mhalifu unamkamata na arrest warrant kuna wahalifu wengine washakata kamba
Wao tYRi wana arrest warrant ya juu kwa juu wakamatwe hai au wakiwa wamekufa
Ova
Huyo Kibaka ulitaka akamatwe je? Wewe utakuwa ni kibaka pia unamtetea kibaka mwenzako.Jeshi halina credibility ya kuaminika. Kwa nini wasingewatuliza wananchi kisha wakawatoa wasiwasi pamoja na kudhibitisha kwamba ni polisi na tunampeleka kituo fulani?
Tuna vyombo vya dola kwann umteke mtu ? je unaona sawa tuache vyomb vya dola na tuanze tekana? kikubwa tupambane na vyombo ambavyo vinakiuka misingi yao ya kiutumishi , tukicheka cheka soon tunakuwa HAITI , TABIA NI MAZOEAKila kitu kina sababu hata yule wa kiluvya kwenda kumteka ukweli anaujua mwenyewe bw tarimo
Ova
Kwa ukamataji huu basi mafunzo kwa polisi wetu ni zero! Mitaala ya mafunzo ya polisi yapitiwe upya na wakufunzi wachunguzwe elimu zao!Ndugu zangu Watanzania,
Jeshi letu la Polisi Nchini limetoa ufafanuzi wa kina juu ya video mjongeo iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikionyesha dereva bodaboda au mtu mwenye pikipiki akikamatwa na watu waliovaa kiraia nakisha baadaye kupakizwa kwenye gari nyeusi na kuondoka naye.
Jeshi letu la polisi limesema tukio hilo lilifanywa na askari wetu kwa mtu huyo ambaye alikuwa ni mhalifu wa makosa mbalimbali ya uporaji kwa kutumia pikipiki.
Kwa hiyo watanzania tuache mihemuko na lawama na kutupa maneno yasiyo na ukweli. Tuwe watu wa subira na kushirikiana na vyombo vyetu vya ulinzi kupata taarifa rasmi.
View attachment 3245354
Soma: Video: Mtanzania adaiwa kutekwa mchana kweupe huko Kibaha
Kwani makachelo hutembea na gari za aina gani?Alphard nyeusi Noah nyeusi mbona wasitumie magari yenye namba na nembo za Polisi kwanini wanatumia gari za raia zisizokuwa na nembo.
kwann jeshi litumie gari la kiraia ? huo ulikuwa utekaj , kemea utekaj kabla hujawa muhanga , hiz tabia zikishamili hatutaweza tena kuzitokomeza , hata Libyia walianzia huku hukuHuyo Kibaka ulitaka akamatwe je? Wewe utakuwa ni kibaka pia unamtetea kibaka mwenzako.