Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Siyo kila mhalifu unamkamata na arrest warrant kuna wahalifu wengine washakata kamba
Wao tYRi wana arrest warrant ya juu kwa juu wakamatwe hai au wakiwa wamekufa

Ova
Upo sahihi kabisa haujawahi kuniangusha katika matumizi ya akili.
 
Acha kuwatetea wahalifu na uhalifu.
hv kati ya yule boda na hao watekaj wenu nan muharifu ? wanaua wapinzan mf Ally Kibao , Soka etc , wanapambana kuua demokrasia kwa kuzuia mikutano ya vyama visivyabiana na ccmu kimawazo mf Chadema , wanazuia maandamano ya kupaza sauti ya umma dhidi ya idadi kubwa ya watu kupotea na wengine kuokotwa maiti , Mauaji ya hadharani mf uchaguzi mdogo mwaka 2024 huko Kigamboni na Gongo la mboto , Ubinyaji wa haki za binadamu kuanzia namna wanavyotumika kubambikizia kesi wapinzan wa ccmu , wanapora mali za watu hasa polisi wa barabarani , wanahusika kuwakinga waharifu dhidi ya mkono wa dola , wamekuwa machawa wa ccmu na sio walInz wa jamii etc

JESHI LA POLIS NDIO WAHARIFU WAKUBWA KULIKO HUYO BODA BODA , TUMEONA NA KUSIKIA MENGI KUHUSU HILI JESHI
 
Embu acha utoto wako hapa. Yaani wewe kila siku unaunga mkono uovu tu Utafikiri na wewe ni mhalifu. Kwanini usiulize sababu ya yule wa pikipiki aliyekuwa anakamatwa kutokutii Amri?

Mwashambwa, siyo kila kitu kinahitaji mihemuko. Namna mbaya ya utendaji kazi wa polisi, unayaweka hatarini hata maisha ya askari wenyewe. Hivi kuna ugumu gani kwa askari baada ya kumkamata na kumdhibiti mtuhumiwa, kiongozi wa operation kujitambulisha rasmi kwa watu waliopo, kwa kutaja jina lake, kuonesha kitambulisho chake, sehemu ambayo mtuhumiwa anapelekwa, na mtuhumiwa kupewa nafasi ya kuwajulisha jamaa zake wa karibu, kama mwongozo wa jeshi la polisi, unavyotaka?

Namna hii mbaya ya utendaji kazi wa polisi, kuna siku italeta maafa. Miongozo ya utendaji kazi ipo, lakini wanaipuuza.
 
Siyo kila mhalifu unamkamata na arrest warrant kuna wahalifu wengine washakata kamba
Wao tYRi wana arrest warrant ya juu kwa juu wakamatwe hai au wakiwa wamekufa

Ova
Kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, mtu anawezw kukamatwa bila warrant pale anapokua anatenda kosa muda huo, (mfano anaiba au anabaka) au pale inapoaminika kuwa kuna warranty imetolewa juu ya kukamatwa kwake lakini haipo mikononi mwa mtu anayemuona huyo mhalifu (mfano warrant imetolewa mbeya na mhalifu anaonekana Mitaa ya Dar). Au warrant iliyochapishwa gazetini.

General rule, lazima kuwe na warrant - kwa mhalifu konki kama huyo lazima wangekuwa na warrant hao mapolisi
 
Hii nchi ngumu sana...........!
Narudia tena hii nchi ngumu sana............!
 
Saidia mtu unayemjua
Mfano huyo angesema natekwa halafu wananchi hawamjui wakawashambulia na kuua hao polisi unajua nini kingewapata hao wananchi baadaye huyo mtu wakiambiwa alikuwa jambazi wakimkimbiza

Wao watahesabika sehemu ya huyo jambazi na kupewa kesi ya mauaji ya kuua polisi

Njia nzuri kwenye hilo ni kupiga simu polisi au kuripoti kituo cha polisi cha karibu au kwa mjumbe au kiongozi wa mtas hsraka haraka sana kwa simu au bodaboda anakimbia haraka kuripoti

Usichukue sheria mkononi hata apige kelele anatekwa
Lazima jamii na taifa kujenga utamaduni wa kufuata akili ya kawaida na sheria katika kuishi.
Akili ya kawaida inahitaji mtu ujilinde ulinde wengine na ufuate sheria.
Sheria zimekataza maovu na kuweka taratibu za kufanya mambo au kudhibiti na kuwashghulikia waovu.
Kwa hiyo, katika kujilinda na kulinda wengine, wananchi wana haki ya k upambana hadi kuwadhibiti watekaji (ni muhimu wafundishwe hivyo, vinginevyo tutajenga taifa la majuha na makondoo).
Pia lazima sheria za ukamataji zifuatwe, ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu stahiki.
 
Mwashambwa, siyo kila kitu kinahitaji mihemuko. Namna mbaya ya utendaji kazi wa polisi, unayaweka hatarini hata maisha ya askari wenyewe. Hivi kuna ugumu gani kwa askari baada ya kumkamata na kumdhibiti mtuhumiwa, kiongozi wa operation kujitambulisha rasmi kwa watu waliopo, kwa kutaja jina lake, kuonesha kitambulisho chake, sehemu ambayo mtuhumiwa anapelekwa, na mtuhumiwa kupewa nafasi ya kuwajulisha jamaa zake wa karibu, kama mwongozo wa jeshi la polisi, unavyotaka?

Namna hii mbaya ya utendaji kazi wa polisi, kuna siku italeta maafa. Miongozo ya utendaji kazi ipo, lakini wanaipuuza.
Taarifa zilikuwa zipo Rasmi kituo cha polisi na hata ndugu walipewa taarifa na kufahamishwa juu ya ndugu yao kushikiliwa na Jeshi la polisi.
 
Nilijua itakuwa kati ya haya mawili
1. Mhalifu au
2. Hapeleki hesabu ya boss. Halafu boss mwenyewe mafia.
 
Kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, mtu anawezw kukamatwa bila warrant pale anapokua anatenda kosa muda huo, (mfano anaiba au anabaka) au pale inapoaminika kuwa kuna warranty imetolewa juu ya kukamatwa kwake lakini haipo mikononi mwa mtu anayemuona huyo mhalifu (mfano warrant imetolewa mbeya na mhalifu anaonekana Mitaa ya Dar). Au warrant iliyochapishwa gazetini.

General rule, lazima kuwe na warrant - kwa mhalifu konki kama huyo lazima wangekuwa na warrant hao mapolisi
Ndomana nkasema huyo ana warrant ya juu kwa juu !
Tena huyo anazali anatoka hai wangekuwa wengine wangemqlizana naye tu

Ova
 
Nilijua itakuwa kati ya haya mawili
1. Mhalifu au
2. Hapeleki hesabu ya boss. Halafu boss mwenyewe mafia.
Kila kitu kina sababu hata yule wa kiluvya kwenda kumteka ukweli anaujua mwenyewe bw tarimo

Ova
 
Ndugu zangu Watanzania,

Jeshi letu la Polisi Nchini limetoa ufafanuzi wa kina juu ya video mjongeo iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikionyesha dereva bodaboda au mtu mwenye pikipiki akikamatwa na watu waliovaa kiraia nakisha baadaye kupakizwa kwenye gari nyeusi na kuondoka naye.

Jeshi letu la polisi limesema tukio hilo lilifanywa na askari wetu kwa mtu huyo ambaye alikuwa ni mhalifu wa makosa mbalimbali ya uporaji kwa kutumia pikipiki.

Kwa hiyo watanzania tuache mihemuko na lawama na kutupa maneno yasiyo na ukweli. Tuwe watu wa subira na kushirikiana na vyombo vyetu vya ulinzi kupata taarifa rasmi.

View attachment 3245354

Soma: Video: Mtanzania adaiwa kutekwa mchana kweupe huko Kibaha
Waambie polisi waako wavae uniform, nextime tutasshindwa kuwatofautisha
 
Lazima jamii na taifa kujenga utamaduni wa kufuata akili ya kawaida na sheria katika kuishi.
Akili ya kawaida inahitaji mtu ujilinde ulinde wengine na ufuate sheria.
Sheria zimekataza maovu na kuweka taratibu za kufanya mambo au kudhibiti na kuwashghulikia waovu.
Kwa hiyo, katika kujilinda na kulinda wengine, wananchi wana haki ya k upambana hadi kuwadhibiti watekaji (ni muhimu wafundishwe hivyo, vinginevyo tutajenga taifa la majuha na makondoo).
Pia lazima sheria za ukamataji zifuatwe, ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu stahiki.
Syo kila mhalifu kumkamata inabidi ufate sheria, kuna wahalifu wengine watukutu haambiliki hawasikii sheria zenyewe zimedunda kwaooo
Mtu anafanya tukio kesho katoka na anaendelea na uhalifu,
Mpaka inafika wakati anapewa warning Acha sasa tutamalizana na wewe lakini bado hasikiii

Ova
 
Siyo kila mhalifu unamkamata na arrest warrant kuna wahalifu wengine washakata kamba
Wao tYRi wana arrest warrant ya juu kwa juu wakamatwe hai au wakiwa wamekufa

Ova
hv kwa matukio ya miaka hii 2 bado unakamata mtu namna ile ? hv ni kwel huyu boda boda ni tishio kias cha kumshika na mitutu ? mtu anaeomba msaada kwa raia ? Mzee kibao walimshika na mitutu tulipokaa kimya alikutwa wap ? hv hawa unawatetea wameua zaid ya watu 100 kweny mwaka uliopita ,unapata wap uhalali wa kushabikia namna hiyo ya ukamataj ? hv chuo cha polisi wanafundishwa nn ? mbona ukamataj huu haufanan na mtu aliyeend kozi za kijeshi , uvaaji pia ni kama panya road , watu wanafika 200 tangu mwaka 2023 hawajulikan walipo , Mdude wa chadema alishikwa hv hv na hatukujuwa alipo na hata kituo waliwekwa wenzio hadi kituo cha mkoa hakwepo , walienda mficha walipoona watu wamechachamaa ndo wakamuachia

TUTATETEA UTEKAJI NA MAUAJI MPK LINI ? AU MPK WW UWE MUHANGA NDO UTAELEWA TUNACHOPIGIA KELELE ?
 
Alphard nyeusi Noah nyeusi mbona wasitumie magari yenye namba na nembo za Polisi kwanini wanatumia gari za raia zisizokuwa na nembo.
 
Kila kitu kina sababu hata yule wa kiluvya kwenda kumteka ukweli anaujua mwenyewe bw tarimo

Ova
Tuna vyombo vya dola kwann umteke mtu ? je unaona sawa tuache vyomb vya dola na tuanze tekana? kikubwa tupambane na vyombo ambavyo vinakiuka misingi yao ya kiutumishi , tukicheka cheka soon tunakuwa HAITI , TABIA NI MAZOEA

ANGALIA HUU MWAKA WA UCHAGUZ WALA HAWAJALI KAMA ZAMAN , WANAKATA UMEME MPK MARA 20 kwa siku moja , wameweka kodi ya maji hadi kweny umeme na ukilipia maji wanakata pia kodi yao ya maji , yaan UMEME WA REA tunalipia hata tusiohusika , yaan ccmu kwa sasa hawajali lolote wanaipeleka nchi shimoni na wajinga wachache wakipewa sembe kg 5 wanasahau kesho wanakingia kifua udhalifu wa ccmu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Jeshi letu la Polisi Nchini limetoa ufafanuzi wa kina juu ya video mjongeo iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikionyesha dereva bodaboda au mtu mwenye pikipiki akikamatwa na watu waliovaa kiraia nakisha baadaye kupakizwa kwenye gari nyeusi na kuondoka naye.

Jeshi letu la polisi limesema tukio hilo lilifanywa na askari wetu kwa mtu huyo ambaye alikuwa ni mhalifu wa makosa mbalimbali ya uporaji kwa kutumia pikipiki.

Kwa hiyo watanzania tuache mihemuko na lawama na kutupa maneno yasiyo na ukweli. Tuwe watu wa subira na kushirikiana na vyombo vyetu vya ulinzi kupata taarifa rasmi.

View attachment 3245354

Soma: Video: Mtanzania adaiwa kutekwa mchana kweupe huko Kibaha
Kwa ukamataji huu basi mafunzo kwa polisi wetu ni zero! Mitaala ya mafunzo ya polisi yapitiwe upya na wakufunzi wachunguzwe elimu zao!
 
Alphard nyeusi Noah nyeusi mbona wasitumie magari yenye namba na nembo za Polisi kwanini wanatumia gari za raia zisizokuwa na nembo.
Kwani makachelo hutembea na gari za aina gani?
 
Huyo Kibaka ulitaka akamatwe je? Wewe utakuwa ni kibaka pia unamtetea kibaka mwenzako.
kwann jeshi litumie gari la kiraia ? huo ulikuwa utekaj , kemea utekaj kabla hujawa muhanga , hiz tabia zikishamili hatutaweza tena kuzitokomeza , hata Libyia walianzia huku huku
 
Back
Top Bottom