Mwashambwa, siyo kila kitu kinahitaji mihemuko. Namna mbaya ya utendaji kazi wa polisi, unayaweka hatarini hata maisha ya askari wenyewe. Hivi kuna ugumu gani kwa askari baada ya kumkamata na kumdhibiti mtuhumiwa, kiongozi wa operation kujitambulisha rasmi kwa watu waliopo, kwa kutaja jina lake, kuonesha kitambulisho chake, sehemu ambayo mtuhumiwa anapelekwa, na mtuhumiwa kupewa nafasi ya kuwajulisha jamaa zake wa karibu, kama mwongozo wa jeshi la polisi, unavyotaka?
Namna hii mbaya ya utendaji kazi wa polisi, kuna siku italeta maafa. Miongozo ya utendaji kazi ipo, lakini wanaipuuza.