Jeshi la Polisi lazuia mkutano wa Mbowe, atakiwa kuripoti Polisi Kinondoni

Jeshi la Polisi lazuia mkutano wa Mbowe, atakiwa kuripoti Polisi Kinondoni

JM3

Senior Member
Joined
Dec 13, 2019
Posts
157
Reaction score
328
Mkutano wa M/kiti wa Chadema, Freeman Mbowe uliokuwa ufanyike mubashara hii leo Mei 14, 2020 kwa lengo la kuzungumza na umma, hautafanyika kwa kuwa Mbowe ametakiwa kuripoti katika kituo cha Polisi cha Oyster Bay.

Mkutano huu umehairishwa baada ya M/ kiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe wakati akijiandaa kuelekea kuanza mkutano huo, alipokea wito wa Jeshi la Polisi nchini kumtaka akaripoti Kituo cha Polisi, Polisi hawakusema sababu ya wito huo. Mhe. Mbowe ameambatana na wakili.


makene.JPG
 
Mbowe ni msanii tu.......alishajua atakamatwa na polisi kufuatia lile agizo la RC Makonda.

Kama kweli angekuwa na hoja za kuongea mkutano angeufanyia Dodoma!

Mbowe anaihujumu Chadema ili ipoteze ushawishi na yeye aendelee kuimiliki kama chama cha " mfukoni" namna ilivyo UDP na TLP!
 
Back
Top Bottom