Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Hilo tukio la kutekwa Kwa Mzee Kibao halikufanywa sirini, limefanywa mchana kweupe na hao watekaji Wala hawakuwa na hofu, kwa kuwa walimshusha toka Kwenye Bus la Tashriff, lililokuwa linaelekea Tanga, eneo la Tegeta Kibo complex.
Mashuhuda wa tukio Hilo la kutekwa Kwa Mzee Kibao na hatimaye kuteswa na kuuawa kinyama, walijitambulisha kama ni askari Polisi waliovaa kiraia.
Sasa kama kweli Jeshi letu la Polisi litakuwa "serious" kabla ya jioni ya leo, litakuwa limewakamata watu wote waliohusika na unyama wa hali ya juu wa kumteka Mzee wetu Kibao na baadaye kumpiga sana Hadi kumuua na kummwagia tindikali usoni Iii asitambulike.
- CHADEMA: Mzee Ally Kibao ametekwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa kwenye basi. Usalama wa Taifa waeleze alipo
Hao watekaji walikuwa na machine gun, pingu, vitu ambavyo ni katika vyombo vya usalama nchini, ambavyo wanavimiliki.
Bila shaka yoyote, mashuhuda waliziona hizo gari za watekaji, Kwa kuwa tukio lenyewe lilifanyika mchana kweupe Kwa hiyo wapo baadhi ya mashuhuda walizikopi "number plate" za magari hayo, Kwa hiyo itakuwa kazi rahisi kufuatilia ni nani mmiliki wa gari hizo.
Hata hivyo Ili uchunguzi huo usivurugwe tunamuomba Rais Samia, achukue hatua ya dharula ya kuwafuta kazi mara moja, IGP Wambura na Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Dar, afande Muliro, kwa kuwa kuendelea kuwepo kazini kwa maafandec hao kutavuruga uchunguzi wa tukio Hilo baya kabisa, Kwa kuwa wao Police ni "main suspects" wa huo utekaji.
Mungu ibariki Tanzania