Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
- Thread starter
- #21
Ndugu yangu, rafiki yangu na mtani wangu Erythrocyte Mimi na Watanzania wote hakuna anaye pinga ukosoaji wenye afya kwa serikali mnapoona pana kasoro. Lakini kinachofanywa na viongozi wako pamoja na wanachama wenzako wa chadema siyo ukosoaji bali ni kupandikiza chuki,uhasama na Mbega ya ubaguzi unaoweza kuchochea vurugu,machafuko, kulilipua na kulipasua Taifa. Viongozi wako mara nyingi wamechochea machafuko na kutaka vurugu zitokee,kama watanzania wa wangewasikilza na kuwaunga mkono dhamira zao kwa hakika hapa tungekuwa tunaandika mambo mengine hapa.
Erythrocyte mbona wewe unajitahidi kupita humu kuandika na kuchangia mada mbalimbali lakini huwa hutukani wala kutumia lugha za uchochezi wala udhalilishaji? Mbona mara nyingi wewe unatumia lugha za heshima ,busara na upendo? Mimi sijawahi kuona andiko lako lolote ukimtukana mtu wala kumdhalilisha mtu humu,Ndio maana hata Mimi nakuheshimu sana michango yako ,kuisoma,kulifuatilia sana kwa kuwa umekuwa mhabarishaji mzuri na unayepigania chama chako pasipo kumjeruhi mtu kwa maneno.
Sasa akina mdude au Mwabukusi Boniface wanashindwa nini kuwasilisha hoja na kumkosoa mtu bila kumtukana wala kuzalisha na kumvunjia heshima? Kwani mtu ukikosoa kwa heshima kama ufanyavyo wewe ujumbe hauwezi kufika? Ni vipi matusi yanaongeza uzito wa hoja? Ni vipi kumdhalilisha mtu kunakuongezea ubora wa hoja? Kwanini tusikosoane kwa hoja bila matusi?
Wewe kweli ndugu yangu unaona lugha za akina Mdude na Mwabukusi ni sawa? Ni uungwana kwa wafanyayo? Ni haki kweli? Ni sahihi kweli? Ndio demokrasia hiyo ya kutukana watu? Hivi huoni kuwa Mdude na Mwabukusi wamekosa adabu na heshima Kwa wanaotofautiana nao mitizamo? Huoni wamekosa busara? Tangia lini matusi yakawa ushujaa?
Mbona akina Nelson mandera,Dr Martin Luther King Jr walikuwa wakosoaji lakini hakuna unapoona wakitukana wengine? Je hawakufikisha ujumbe wao kwa Dunia? Hawakuungwa mkono? Lakini mbona walitumia lugha za ustaarabu katika kukosoa na Dunia nzima inawaelewa mpaka leo?
Tusitake kulipasua Taifa letu kwa Tamaa na uroho wa madaraka au kwa kutumiwa na kutimiza ajenda za watu au wafadhili wasiolitakia mema Taifa letu.kuunga mkono yafanywayo na kutamkwa kutoka katika vinywa vya baadhi ya viongozi na wanachama wa chadema siyo haki wala uungwana kwa Taifa letu,siyo Afya wala busara kufanya hivyo,kwa kuwa inachochea chuki,uhasama ,ubaguzi, mgawanyiko na mpasuko kwa Taifa letu.