Jeshi la Polisi liendelee kuwakamata wote wenye kuleta maneno ya Uchochezi na kuwatupa Ndani kwa mahojiano

Ndugu yangu, rafiki yangu na mtani wangu Erythrocyte Mimi na Watanzania wote hakuna anaye pinga ukosoaji wenye afya kwa serikali mnapoona pana kasoro. Lakini kinachofanywa na viongozi wako pamoja na wanachama wenzako wa chadema siyo ukosoaji bali ni kupandikiza chuki,uhasama na Mbega ya ubaguzi unaoweza kuchochea vurugu,machafuko, kulilipua na kulipasua Taifa. Viongozi wako mara nyingi wamechochea machafuko na kutaka vurugu zitokee,kama watanzania wa wangewasikilza na kuwaunga mkono dhamira zao kwa hakika hapa tungekuwa tunaandika mambo mengine hapa.

Erythrocyte mbona wewe unajitahidi kupita humu kuandika na kuchangia mada mbalimbali lakini huwa hutukani wala kutumia lugha za uchochezi wala udhalilishaji? Mbona mara nyingi wewe unatumia lugha za heshima ,busara na upendo? Mimi sijawahi kuona andiko lako lolote ukimtukana mtu wala kumdhalilisha mtu humu,Ndio maana hata Mimi nakuheshimu sana michango yako ,kuisoma,kulifuatilia sana kwa kuwa umekuwa mhabarishaji mzuri na unayepigania chama chako pasipo kumjeruhi mtu kwa maneno.

Sasa akina mdude au Mwabukusi Boniface wanashindwa nini kuwasilisha hoja na kumkosoa mtu bila kumtukana wala kuzalisha na kumvunjia heshima? Kwani mtu ukikosoa kwa heshima kama ufanyavyo wewe ujumbe hauwezi kufika? Ni vipi matusi yanaongeza uzito wa hoja? Ni vipi kumdhalilisha mtu kunakuongezea ubora wa hoja? Kwanini tusikosoane kwa hoja bila matusi?

Wewe kweli ndugu yangu unaona lugha za akina Mdude na Mwabukusi ni sawa? Ni uungwana kwa wafanyayo? Ni haki kweli? Ni sahihi kweli? Ndio demokrasia hiyo ya kutukana watu? Hivi huoni kuwa Mdude na Mwabukusi wamekosa adabu na heshima Kwa wanaotofautiana nao mitizamo? Huoni wamekosa busara? Tangia lini matusi yakawa ushujaa?

Mbona akina Nelson mandera,Dr Martin Luther King Jr walikuwa wakosoaji lakini hakuna unapoona wakitukana wengine? Je hawakufikisha ujumbe wao kwa Dunia? Hawakuungwa mkono? Lakini mbona walitumia lugha za ustaarabu katika kukosoa na Dunia nzima inawaelewa mpaka leo?

Tusitake kulipasua Taifa letu kwa Tamaa na uroho wa madaraka au kwa kutumiwa na kutimiza ajenda za watu au wafadhili wasiolitakia mema Taifa letu.kuunga mkono yafanywayo na kutamkwa kutoka katika vinywa vya baadhi ya viongozi na wanachama wa chadema siyo haki wala uungwana kwa Taifa letu,siyo Afya wala busara kufanya hivyo,kwa kuwa inachochea chuki,uhasama ,ubaguzi, mgawanyiko na mpasuko kwa Taifa letu.
 
Wewe ndiye Wakumbozi, unaeaibisha Mkoa mzima, mpaka nashangaa hii Akili inayotoka tumboni badala ya kichwani.
 
Hakuna ambalo serikali inaweza kuogopa ,ndio maana ilikwenda mahakamani ikapangua hoja zote kishujaa na kihodari na kushinda kesi vizuri.
 
Wewe ndiye Wakumbozi, unaeaibisha Mkoa mzima, mpaka nashangaa hii Akili inayotoka tumboni badala ya kichwani.
Hoja hujibiwa kwa hoja na siyo Viroja.pinga na kosoa kwa hoja na siyo habari za ubaguzi wa kikanda au ukabila.maana hapa siandiki kwa niaba ya kabila au ukoo wala mkoa.mimi siyo muandishi wa mkoa wala ukoo wala kabila
 
Toa mifano ya matusi na uchochezi waliofanya .
 
Sifahamu una uelewa kiasi gani kuhusu haki ya kikatiba ya watu kutoa maoni yao na pia wajibu wa vyama vya upinzani, watu wa kada mbalimbali ikiwemo wanaharakati katika kuikosoa serikali iliyopo madarakani pale endapo inadhibitika inafanya maamuzi yenye madhara hasi kwa taifa letu. Watawala kamwe hawezi kukwepa kukosolewa pale wapotenda mambo ya hovyo kwa kificho ama kwa uwazi. Huwezi kutaka itumike lugha nyepesi dhidi ya kundi la watawala wachache walio wachoyo, wabinafsi, wasiowajibika ipasavyo, wezi, mafisadi, wabadhirifu wa mali za umma, n.k. eti tu kwa kisingizio cha uheshimiwa wao na haki yao batili na haramu yenye kuwahalalishia kutenda jinai na kisha kutokuweza kushtakiwa pale wafanyapo madudu yao. Madai yenye kusingizia watu "kutumia lugha za uchochezi, ubaguzi na zenye hatari ya kuligawa taifa na kuleta machafuko na mpasuko nchini" ni yale yatokayo kwa vibaraka na chawa wa hao watawala dhalimu na wenye kutaka kuhalalisha udhalimu.
 
Mwanasiasa bora huchunga ulimi wake na pia huchagua maneno ya kuongea na ndio hekima na busara kama mkuu hapo uliyemnukuu maana kuvunja sheria ni maneno tu ukiyatamka umevunja tayari,ukijizuia uko salama.
Huwezi kamwe kutoa hukumu ya jumla kuhusu maudhui ya kitabu ama jarida lolote lile kwa kusoma tu kichwa chake cha babari. Ujumbe unaobeba ukweli ndani ya maudhui yake huwa na sura mbili zenye kukinzana.

Kwanza huwa mchungu kwa wale wenye mtazamo hasi dhidi yake. Na plili, huamsha faraja na kuchocjea furaha kwa wale wenye mtizamo chanya juu yake.
Hapo busara na hekima huwaendea wale wote wenye mtazamo chanya juu ya ukweli pale unapotolewa kwa maslahi mapana ya taifa letu.
 
Hakuna uhuru usio na mipaka, ukitumia uhuru wako vibaya lazima utashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Usitegemee kuachiliwa ukivuruga Amani na umoja wa taifa lazima ushughulikiwe.
 
Haki haiwezi kuwa kuwatukana watu na kuwadhalilisha,hiyo siyo haki wala demokrasia,kwa hiyo ni lazima waanze kukamatwa kwa nguvu zote
 
Haki haiwezi kuwa kuwatukana watu na kuwadhalilisha,hiyo siyo haki wala demokrasia,kwa hiyo ni lazima waanze kukamatwa kwa nguvu zote
Lucas mdogo wangu, ukweli na uongo kamwe haviwezi kupikika chungu kimoja. Kamwe huwezi kuhalalisha haramu kwa kilemba cha madai ya kutaka kuuficha uovu.

Pepo likimkumba mtu, mtumishi wa Mungu huwajibika kulikemea limtoke, hapo hakuna cha kubembeleza, matumizi ya lugha laini wala nini, ni, karipio, nguvu na mamlaka, toka pepo, mwache mtu huyu huru na kwenda katika makao yako.

Wale waliopewa dhamana ya uongozi wanapokengeuka hupaswa kuambiwa ukweli pasipo kupepesa macho. Wao ni zao la vyeo vya kikatiba, na majukumu yao ni kuhifadhi, kuitii na kuilinda katiba hiyo hiyo ambayo imewapa wajibu wa kutenda na kuenenda.

Hivi unaweza kutueleza nini hasa maana ya uchochezi unaofanywa, na maneno yapi hasa yanapaswa kumfanya mtu kubanwa na sheria kwa wale ambao hawaridhishwi katika sakata la mkataba wa DPW. Jeshi la Polisi lisitake kuwaondoa watu kwenye reli kwa kisingizio cha uchochezi na matendo ya kutaka kufanya uhaini kwa wale ambao wanaopinga baadhi ya vipengele vilivyomo katika mkataba.

Beleshi ni lazima liitwe hivyo kwa jina lake, na wala si kwa jina la kijiko kikubwa. Pepo limemkumba mama yetu Tanganyika, ni lazima likaripiwe kwa lugha ngumu, ili litii, na limtoke. Hapo hakuna mba mba mba.
 

Hilo jeshi la polisi ndio hutumika kusimamia wizi wa kura ili CCM iendelee kukaa madarakani kwa shuruti. Hivyo ni sahihi waendelee kukitetea chama walichokilinda kukaa madarakani kwa njia haramu.
 
Bado hujapewa cheo, maana unaboa mpaka basi.
 
Hilo jeshi la polisi ndio hutumika kusimamia wizi wa kura ili CCM iendelee kukaa madarakani kwa shuruti. Hivyo ni sahihi waendelee kukitetea chama walichokilinda kukaa madarakani kwa njia haramu.
CCM siku zote inashinda kwa haki kabisa kutokana na imani kubwa na uaminifu iliyojijengea kwa watanzania.
 
CCM siku zote inashinda kwa haki kabisa kutokana na imani kubwa na uaminifu iliyojijengea kwa watanzania.
Zamani wakati watu wamelala CCM iliweza kushinda kwa haki. Toka uchaguzi wa 2010 kizazi za CCM kilipoisha, wizi kwa kushirikiana na vyombo vya dola na tume isiyo huru ya uchaguzi ndio mbeleko ya CCM. Uchaguzi wa 2020 chini ya dhalimu Magufuli ndio tulishuhudia uchaguzi wa kishenzi kupita maelezo. Na ushahidi wa ushenzi ule upo wazi.

Kile kizazi cha waliolala wa kuichagua CCM kwa hiari kimeshapita, ndio maana tunashuhudia chaguzi za kishenzi mno ili CCM ibaki madarakani. Ifike mahali CCM mkubali kuwa wakati ukuta, na zama zenu zimeshapita. Vinginevyo jiandaeni kwa machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi na tutayaunga mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…