Jeshi la Polisi limewakamata na kuwahoji waliovunja vioo Treni ya SGR, ni watoto wa miaka 12 na 16

Jeshi la Polisi limewakamata na kuwahoji waliovunja vioo Treni ya SGR, ni watoto wa miaka 12 na 16

Wakuu,

Hii taarifa mbona kama ya kutuzuga hivi? Hayo mawe yalikuwa ya ukubwa kiasi gani mpaka yavunje hivyo vioo? Au ni sababu ya mwendo? Wazee wa physics mje mtueleze.

Lakini pia kama walikuwa wanashindanisha kasi siyo kwamba yangerushwa kwenye uelekeo ule treni inakoenda kuona kipi kitawahi kufika, au ndio yalikata kona kama ile risasi iliopigwa juu karibu na kituo ikarudi chini hadi kumpata mwanafunzi aliyekuwa anajaribu joho, au risasi iliyppigwa juu ikakata kona hadi kumfikia Akwilina?

Mapovu yenu chawa myaache kwenye nguo, mwenye ana majibu ya kitaalamu kuelezea hilo atuambie tuelewe.

=====

Baada ya kufanya msako Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata watoto hao wawili ambao wote wakazi wa kijiji cha Manase Wilaya Chamwino.

Chanzo cha kufanya uharibifu huo ni baada ya kuona treni ikipita wakarusha mawe kwa pamoja ili kuona kama mawe waliyoyarusha yataweza kushindana na mwendo wa treni.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na njia hiyo ya treni kupeana elimu juu ya ulinzi wa miondombinu hiyo na kwa wazazi kutoa elimu kwenye familia hasa kwa watoto kuacha vitendo vitakavyosababisha uharibifu na hivyo kukinzana na sheria za nchi.

View attachment 3159991
Nipo impressed kujua walifanywa nn baada ya tukio!
 
Kipindi nakua mzazi wangu alinikuza kwa namna mbili na namshukuru sana na Mungu amrehemu huko alipo

Nazo ni utoto na Ujinga

Kuna vitu nilikuwa nikifanya alisema huu utoto basi hakuniadhibu alinionya
Mfano. Kuchora madaftari au kuta, kukataa kuoga, kupanda miti,kuzuga naumwa etc.

Lakini kuvunja vitu, kutukana sijui kuiba n.k hiyo ilikuwa haina muamana maana alisisitiza huo ni ujinga na sio utoto hivyo nilikuwa napokea dozi takatifu na ya kukata na shoka

Nachotaka kusema ni hiki hao watoto walichofanya ni ujinga sio utoto
 
Jeshi la Polisi limewakamata na kuwahoji Watuhumiwa wawili ambao ni Watoto wa miaka 16 na miaka 12 kwa tuhuma za kuvunja vioo viwili vya Treni ya Mwendokasi (SGR) kwa kutumia mawe katika Kijiji cha Manase, Wilaya ya Chamwino Dodoma.

Taarifa ya Polisi imesema Watoto hao ambao majina yao ni Erasto Michael Richard (16) na Hassan Ezekiel Ndahani ( 12) Wakazi wa Kijiji hicho cha Manase, walifanya tukio hilo wakati Treni hiyo ikiwa inapita eneo hilo ikitokea Dar es salaam kuelekea Dodoma.

Jeshi la Polisi limesema chanzo cha Watuhumiwa hao kufanya kitendo hicho ni kupima uwezo wa spidi ya mawe na spidi ya Treni hiyo kuona kama mawe hayo yangeweza kushindana na mwendo wa Treni ambapo Jeshi hilo limetoa wito kwa Wananchi hasa wanaoishi maeneo ambayo Treni inapita kuendelea kupeana elimu juu ya umuhimu wa kulinda miundombinu ya Treni kwani ni kwa manufaa ya Watanzania wote.

“Kila Mzazi/Mlezi anao wajibu wa kutoa elimu kwa Familia hasa Watoto kuacha vitendo ambavyo vitasababisha uharibifu kwa reli na Treni ya kisasa kwani itawasababisha kukinzana na sheria za Nchi” imeeleza taarifa ya Polisi..

Hawa wagogo wataelimika lini?
20241124_170018.jpg
 
Wakuu,

Hii taarifa mbona kama ya kutuzuga hivi? Hayo mawe yalikuwa ya ukubwa kiasi gani mpaka yavunje hivyo vioo? Au ni sababu ya mwendo? Wazee wa physics mje mtueleze.

Lakini pia kama walikuwa wanashindanisha kasi siyo kwamba yangerushwa kwenye uelekeo ule treni inakoenda kuona kipi kitawahi kufika, au ndio yalikata kona kama ile risasi iliopigwa juu karibu na kituo ikarudi chini hadi kumpata mwanafunzi aliyekuwa anajaribu joho, au risasi iliyppigwa juu ikakata kona hadi kumfikia Akwilina?

Mapovu yenu chawa myaache kwenye nguo, mwenye ana majibu ya kitaalamu kuelezea hilo atuambie tuelewe.

=====

Baada ya kufanya msako Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata watoto hao wawili ambao wote wakazi wa kijiji cha Manase Wilaya Chamwino.

Chanzo cha kufanya uharibifu huo ni baada ya kuona treni ikipita wakarusha mawe kwa pamoja ili kuona kama mawe waliyoyarusha yataweza kushindana na mwendo wa treni.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na njia hiyo ya treni kupeana elimu juu ya ulinzi wa miondombinu hiyo na kwa wazazi kutoa elimu kwenye familia hasa kwa watoto kuacha vitendo vitakavyosababisha uharibifu na hivyo kukinzana na sheria za nchi.

View attachment 3159991
Mbona hili jambo kwa watu waliosafiri kwa njia ya treni Dar korogwe moshi au Tanga korogwe moshi yalikuwa kawaida kurusha mawe ni vile habari zilikuwa hazitangazwi!
 
Back
Top Bottom