Jeshi la Polisi linamsaka aliyemfanyia Mtoto Kitendo cha Ukatili na Udhalilishaji kwa Kumning’iniza kwenye mti

Jeshi la Polisi linamsaka aliyemfanyia Mtoto Kitendo cha Ukatili na Udhalilishaji kwa Kumning’iniza kwenye mti

Unaweza kuta labda ni kwa jirani yetu, sasa sijui Jeshi litavuka mipaka kwenda kumkamata mhusika!

Nawaza tu.
 
View attachment 2754985
Jeshi la Polisi limeona video hii fupi (clip) ikimwonesha Mtoto aliyefanyiwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji na limeanza kuifanyia kazi kuanzia ilipoanza kusambaa ili aliyefanya kitendo hicho cha kinyama kisichokubalika aweze kukamatwa na hatua zingine za kisheria ziweze kufuata.

Mtoto huyu lazima atakuwa na Mama, Babu, Bibi, Shangazi, Mjomba, Majirani na Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Tunatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za nani alifanya kitendo hicho au kilifanyikia wapi asisite kutoa taarifa Polisi au kwa Kiongozi yeyote yule ili kufanikisha kukamatwa kwake.

Imetolewa na:
David A. Misime - SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu Ndogo ya Polisi
Dar es Salaam, Tanzania

Pia soma: Serikali imchukulie hatua kali za Kisheria huyu aliyemtesa Mtoto kwa staili hii
naunga mkonyo hoja
 
Hee!!! Yani wapo kwenye msako alafu tuwasaidie sisi?
Ukiangalia hiyo video na ukashindwa kutoa ushirikiano ikiwa unajua, basi huna tofauti na hao waliofanya hivyo.

Mimi ningewachoma mapema tu, ule ukatili ni wa jambazi aliekubuhu.
 
Mbona kitengo cha IT cha police wakishirikiana na TCRA ni rahisi kumjua mtu was Kwanza kurusha maudhui mtandaoni?
Wito wangu msimdhuru mtuma picha maana ndio kamafanya sote tukaona mateso ya mtoto Ila mshughulikieni vilivyo kijana anaeonekana akimpatia adhabu isiyo stahili mtoto mdogo kama yule
Sheria ifuate mkondo wake
 
Back
Top Bottom