Ushauri wangu kwa CHADEMA.
CHADEMA iandae na ije na Mkakati wa ndani kuwalinda na kuwatoa kwenye risk "Internal front line activists, critics and human rights defenders" kwa kuwapa ulinzi wa aina mbalimbali kulingana na mazingira, psychological support and mentorship kulingana na hali halisi iliyopo.
Toka 2015, dola imejipa mkakati wa kuteka, kuua na kuumiza wanaharakati, wakosoaji na wapigania haki wa kisiasa hasa ambao ni "aggressive" mifano ni mingi tuu. Sina hakika mpaka sasa ni watu wangapi wametekwa, kuumizwa au kuuwawa ambao ni CHADEMA affiliates.
Ni wengi sana, lakini kuna mazingira mengine ni wazi yanatokana na uzembe, kujisahau au kutokuwa na intelijensia nzuri na support kwa watu wao.
Nitatoa Mfano mdogo, Mdude kwa alipofikia, level yake ya mapambano, historia yake ya kuteswa na kupigwa hakutakiwa kukaa Iwambi, porini huko hana back-up, hafuatiliwi, hana alerts wala lolote, hana ulinzi wa namna, vifaa vya kiteknolojia wala lolote.
Chadema wanaweza fanya kitu kwa watu wake zama hizi za teknolojia na utandawazi.
Ni wengi sana, na Chadema haijajua kwamba mkakati wa dola ni kuwadumaza kwa kuteka, kuua na kuumiza watu wao.
Kwenye mazingira kama haya, kuna takiwa kuwepo na mkakati wa kujihami na kupunguza madhara.
Mtu kama Ben Saanane na Mdude (kwa kutaja wachache) kwa level ya ukosoaji wao walitakiwa waingizwe kwenye mpango kama huu. Kipindi cha kupigania ukoloni, ukisikia Mandela yupo safe house za ANC nje au ndani ya South Africa usifikiri ulikuwa uoga, ilikuwa ni namna ya kukwepa mkono wa serikali dhalimu.
Huko mbele, watu hawatakua wanafanya harakati, maana mpango huu wa dola ni kupandikiza uoga na kudumaza harakati. Na watafanikiwa kama wahanga hawatakuwa na mikakati ya kujihami.