Jeshi la polisi mkiwa kama hivi mtakuwa mkipendwa sana

Polisi kama huyu anaonyesha uwajibikaji wake kulinda amani na kusaidia pale jambo linapo wezekana.

kumsaidia kusomesha mtoto ni jambo zuri

View: https://www.youtube.com/watch?v=jyoBjJv64fs

Waafrika mnapenda sana bure. Tunataka polisi wafanye kazi kwa kuzingatia sheria za nchi na haki, full stop. Itasaidia nini kama atachukuwa rushwa halafu anakwenda kusaidia? Au anaua leo kesho anatoa msaada? Au anambambikia kesi mtu halafu anatoa msaada? Tujaribu kutafakari kabla ya kusifia jambo.
 
Kuna ubinadamu nje ya kazi. Ulitaka afanane na moderetor wa JF ikifika usiku
 
Waafrika mnapenda sana bure. Tunataka polisi wafanye kazi kwa kuzingatia sheria za nchi na haki, full stop. Itasaidia nini kama atachukuwa rushwa halafu anakwenda kusaidia? Au anaua leo kesho anatoa msaada? Au anambambikia kesi mtu halafu anatoa msaada? Tujaribu kutafakari kabla ya kusifia jambo.
Hayo ya kuchukua rushwa na kumsaidia huyo kijana sioni kama yanatuhusu sana. Ukizingatia Afande massawe hatumjui maisha yake. Alafu ata huko nchi mnazoishi zilizoendelea kuna story kibao za police kusaidia raia wenye uhitaji. Hivyo tümpe pongezi Askari kwa alichojitolea. Atakako pata hela ni suala lake binafsi
 
Shida hajui Uafrika wala Uzungu! Huyo kijana hakuyachagua hayo maisha. Ndiyo maana anapambana kusoma ili asije kuwa ombaomba baadaye.

Si Afrika tu ndiyo kuna watu wenye uhitaji. Hata Marekani wapo. Utofauti tu ni kwamba kule Marekani kuna akina "Afande Massawe" wengi hivyo wahitaji wanasaidika kirahisi tofauti na huku ambako akina "Afande Massawe" wanaonekana watu wa ajabu kwa kuwa wanajitoa kutasaidia wengine.

Afande Massawe kafanya jambo jema. Ukiweza, mtafute umuunge mkono kwa hiyo kazi nzuri anayoifanya.
 
🔨📌
 
Umeelewa point yangu? Nimesema kipaumbele cha polisi kiwe ni kufuata sheria, maadili mazuri na haki kwenye kazi na hivi viwe ndiyo vigezo vya kwanza tutakavyotumia kuwapima. Kuna faida gani ya kutoa msaada kama polisi imeoza? Tumia akili kidogo!
 
Tumia ubongo wako ili uelewe nilichoelezea. Kusaidia bila maadili mazuri ni bure. Soma heading ya thread ilivyo ya kijinga!
 
Umeelewa point yangu? Nimesema kipaumbele cha polisi kiwe ni kufuata sheria, maadili mazuri na haki kwenye kazi na hivi viwe ndiyo vigezo vya kwanza tutakavyotumia kuwapima. Kuna faida gani ya kutoa msaada kama polisi imeoza? Tumia akili kidogo!
Polisi ni taasisi! Afande Massawe anaweza akawa ni mtu mdogo sana kwenye hiyo taasisi hivyo hana ushawishi wowote kwenye hiyo taasisi. Ni kumwonea kumuhusisha yeye na udhaifu au uimara wa taasisi. Lakini kwa kitendo chake cha kujitolea kumsaidia muhitaji, ameonesha kuwa ni mwaminifu kwa kile kilicho katika uwezo wake. Apongezwe kwa hilo.
 
Ndugu jaribu kuelewa ninachopigania hapa: Mwanzisha thread kaandika hivi kichwa cha habari yake: ''Jeshi la polisi mkiwa kama hivi mtakuwa mkipendwa sana''. Mimi nikampinga na kusema kupendwa kwa polisi ni lazima kuandamane na kufanya kazi kwa kuzingatia haki na sheria na siyo kutoa zawadi tu. Kipi kigumu hapa? Wewe unakubaliana naye kuwa polisi kutoa misaada tu bila kubadilika kiutendaji ni sahihi?
 
Ingawa sijawahi kutoka nje ya Tanzania lakini na siwezi kusema kuhusu police wa nchi nyingine. Lakini ni kweli hakuna nchi ambayo raia wake wanawapenda police asilimia 100. Wao wamewekwa kulinda sheria ifuatwe na binadamu kwa asili ni wavunja sheria ikiwemo ata hao Askari. KWa hiyo ni ngumu sana kua na police perfect 100% anapotokea mmoja kama massawe basi na apongezwe
 
Back
Top Bottom