Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limemtia mbaroni Mtu mmoja aitwaye Emmanuel Sulwa Mapana (24) maarufu Mchambi Mkazi wa Mtaa wa Sima, Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu akiwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania zenye cheo cha Luteni.
Polisi Simiyu wamesema leo February 14,2025 saa 6:30 mchana Kikosi kazi cha kupambana na uhalifu na Wahalifu Mkoa wa Simiyu kilifanikiwa kumkamata Mtu huyo akiwa amevaa Kombati ya Jeshi la Wananchi Tanzania akiwa na gari aina ya Ractic lenye namba ya usajili T.560 DCS ambapo pia alikutwa na Mkanda wa Jeshi la Wananchi na Laptop moja.
“Emmanuel Sulwa Mapana alikuwa anatafutwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa kosa la kujifanya Mtumishi wa Serikali, Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu linatoa wito kwa Wananchi wote kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za uhalifu na Wahalifu” - imeeleza taarifa ya Polisi.
-------------------------------------------
Kuna mambo siyaelewi kwenye hili hii taarifa:
1. Je chombo cha polisi kwa maana hii Jeshi la Polisi lina haki ama wajibu wa kuwashika watuhumiwa wa namna hii?! Watu wanaovaa sare za Jeshi la Wananchi wanatiwa nguvuni na Jeshi la Polisi ama Jeshi la Wananchi?
2. Mwanzoni mwa taarifa, inasema kuwa Emmanuel amekutwa na sare za Jeshi zenye cheo cha Luteni, je kukutwa na sare ni sababu tosha ya Emmanuel kuwa ni Luteni? Je ni kazi ya Jeshi la Wananchi ama Jeshi la Polisi kujua kuwa Emmanuel ni luteni ama laah?!
3. Jeshi la Wananchi (JWTZ) kuna viongozi pamoja na MP Military Police je Jeshi la Polisi wanashindwa kushirikiana na JWTZ katika kutoa taarifa na MP wa Jeshi la Wananchi ndio waende kumkamata Luteni feki?
4. Taarifa ya sasa inadai kuwa Emmanuel Sulwa Mapana kuwa ni Luteni feki, je JWTZ wakisema kuwa Dogo Emma ni Luteni, Jeshi la Polisi wataondoa kauli yao au wataendelea kusema kuwa Emma ni Luteni feki?
Mpaka sasa hatujapata neno kutoka JWTZ kuwa Emmanuel ni luteni feki! Ila sidhani kama ni sahihi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu kuweka wazi kuwa Emmanuel ni Luteni Feki kwa kigezo cha kumkuta na sare za jeshi, bali ilikuwa ni kazi ya MP wa JWTZ waliopo sehemu husika.