Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limemtia mbaroni Emmanuel Sulwa Mapana akiwa na sare za Jeshi zenye cheo cha Luteni

Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limemtia mbaroni Emmanuel Sulwa Mapana akiwa na sare za Jeshi zenye cheo cha Luteni

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limemtia mbaroni Mtu mmoja aitwaye Emmanuel Sulwa Mapana (24) maarufu Mchambi Mkazi wa Mtaa wa Sima, Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu akiwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania zenye cheo cha Luteni.
Screenshot_20250214_213045_Lite.jpg

Polisi Simiyu wamesema leo February 14,2025 saa 6:30 mchana Kikosi kazi cha kupambana na uhalifu na Wahalifu Mkoa wa Simiyu kilifanikiwa kumkamata Mtu huyo akiwa amevaa Kombati ya Jeshi la Wananchi Tanzania akiwa na gari aina ya Ractic lenye namba ya usajili T.560 DCS ambapo pia alikutwa na Mkanda wa Jeshi la Wananchi na Laptop moja.
images (98).jpeg

Emmanuel Sulwa Mapana alikuwa anatafutwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa kosa la kujifanya Mtumishi wa Serikali, Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu linatoa wito kwa Wananchi wote kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za uhalifu na Wahalifu” - imeeleza taarifa ya Polisi.

-------------------------------------------
Kuna mambo siyaelewi kwenye hili hii taarifa:

1. Je chombo cha polisi kwa maana hii Jeshi la Polisi lina haki ama wajibu wa kuwashika watuhumiwa wa namna hii?! Watu wanaovaa sare za Jeshi la Wananchi wanatiwa nguvuni na Jeshi la Polisi ama Jeshi la Wananchi?
Screenshot_20250214_213045_Lite.jpg

2. Mwanzoni mwa taarifa, inasema kuwa Emmanuel amekutwa na sare za Jeshi zenye cheo cha Luteni, je kukutwa na sare ni sababu tosha ya Emmanuel kuwa ni Luteni? Je ni kazi ya Jeshi la Wananchi ama Jeshi la Polisi kujua kuwa Emmanuel ni luteni ama laah?!

3. Jeshi la Wananchi (JWTZ) kuna viongozi pamoja na MP Military Police je Jeshi la Polisi wanashindwa kushirikiana na JWTZ katika kutoa taarifa na MP wa Jeshi la Wananchi ndio waende kumkamata Luteni feki?

4. Taarifa ya sasa inadai kuwa Emmanuel Sulwa Mapana kuwa ni Luteni feki, je JWTZ wakisema kuwa Dogo Emma ni Luteni, Jeshi la Polisi wataondoa kauli yao au wataendelea kusema kuwa Emma ni Luteni feki?
images (98).jpeg

Mpaka sasa hatujapata neno kutoka JWTZ kuwa Emmanuel ni luteni feki! Ila sidhani kama ni sahihi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu kuweka wazi kuwa Emmanuel ni Luteni Feki kwa kigezo cha kumkuta na sare za jeshi, bali ilikuwa ni kazi ya MP wa JWTZ waliopo sehemu husika.
 
Aisee ni bora ungetoa habari bila kuweka maswali yako. Kuvaa sare za jeshi ni uhalifu na jeshi lenye kazi ya ku deal na uhalifu ni polisi na siyo jeshi. Hata ukifanya uhalifu na kuharibu mali ya jeshi au kuibia mwanajeshi, polisi ndiyo inatakiwa ichukuwe hatua za kukushika na kukushtaki. Wanajeshi hawana mamlaka ya ku deal na uhalifu wa raia. MP wa jeshi siyo kwa ajili ya kukamata wananchi wahalifu mitaani.
 
Madogo kama hawa wanaotaka kazi ya jeshi, peleka Goma huko wakapambane na M23. Wakifanikiwa kurudi, watakuwa wamenyooka.
 
Aisee ni bora ungetoa habari bila kuweka maswali yako. Kuvaa sare za jeshi ni uhalifu na jeshi lenye kazi ya ku deal na uhalifu ni polisi na siyo jeshi. Hata ukifanya uhalifu na kuharibu mali ya jeshi au kuibia mwanajeshi, polisi ndiyo inatakiwa ichukuwe hatua za kukushika na kukushtaki. Wanajeshi hawana mamlaka ya ku deal na uhalifu wa raia. MP wa jeshi siyo kwa ajili ya kukamata wananchi wahalifu mitaani.
Umemuelewesha vizuri sana huyo 'layman'.
 
Kwanza kwa kukamatwa tu ina maana jeshi la Polisi limejiridhisha kuwa ni feki
Wanajeshi wangapi wanapita mitaani wakiwa wamevaa magwanda na hawakamatwi?
Huyu walikuwa wana taarifa zake na alikuwa anatafutwa na wamemdaka
Huyu sio wale vijana wanaovaa bandana au t-shirt ya jeshi na kukamatwa na wajeda na kurushwa kichura
Huyu ameweka na nyota mbili kabisa kuonekana ni afisa wa ngazi ya juu jeshini
Hayo maswali yako utajijibu wewe
 
Ww nae ni andazi kabisha kaz na majukumu ya JWTZ Ni kulinda mipaka na kaz ya polisi ni kulinda wananchi na mali zao

Sasa km kashikwa iyo ni kazi ya polisi na ata mahakama atapelekwa mahakama za kiraia km wezi au matapeli wengne

Jwtz hawana haki na wala sio jukumu lao kusika wezi na matapeli
 
Ngoja tusubili JWTZ nao watoe taarifa..ila dogo anasura ya kilembo napata mashaka.
Nenda Korea utawakuta ma general very soft Ila huwezi ku battle nae.

Binafsi mimi nina mwonekano mzur..mweupe na unaweza zania mtoto wa mama..watu ustaajabu wakijichanganya kuanzia udogo mpaka nakua mfano kwenye mpira nikiwa uwanjani nilikua nakiwasha mpaka wanashangaa

Urembo au ukakamavu hauonekanagi kwa macho

Bagoshaaa,
Nyinyi ndio mmezoea mtu mpaka awe na sura ya mzee WASSIRA Ama MIZENGO PINDA ndie awe kanali ☺️😊☺️😂😂🤣🤣
 
Nenda Korea utawakuta ma general very soft Ila huwezi ku battle nae.

Binafsi mimi nina mwonekano mzur..mweupe na unaweza zania mtoto wa mama..watu ustaajabu wakijichanganya kuanzia udogo mpaka nakua mfano kwenye mpira nikiwa uwanjani nilikua nakiwasha mpaka wanashangaa

Urembo au ukakamavu hauonekanagi kwa macho

Bagoshaaa,
Nyinyi ndio mmezoea mtu mpaka awe na sura ya mzee WASSIRA Ama MIZENGO PINDA ndie awe kanali ☺️
 
Back
Top Bottom