Jeshi la Polisi Morogoro lawakamata maofisa saba wa LBL kwa tuhuma za biashara haramu ya fedha

Jeshi la Polisi Morogoro lawakamata maofisa saba wa LBL kwa tuhuma za biashara haramu ya fedha

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata watu saba wanaodaiwa kuendesha biashara haramu ya fedha mtandaoni bila kibali cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Soma pia: Jeshi la polisi Mbeya limewakamata watu watano kwa kuhusika na mchezo wa upatu wa LBL

Watuhumiwa hao ni wawakilishi wa kampuni ya Leo Beneth London (LBL), wakifanya shughuli zao katika Manispaa ya Morogoro na Turiani, Mvomero.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama akizungumza leo Alhamisi, Februari 20, 2025 amesema waliwakamata watuhumiwa hao Februari 18, 2025, Kilakala, Manispaa ya Morogoro wakiwa na vifaa vinavyohusiana na biashara hiyo.

Watuhumiwa ni David Francis (35), Boazi Amboniye (42), Kundi Msalaba (31), Moses Dugomela (22), Isaya Paulo (25) na Baraka Sanga (32).

Msako huo umefanyika kwa kushirikiana na BoT, ikiwa ni sehemu ya kudhibiti utapeli wa fedha kupitia mitandao ya simu na teknolojia nyingine za kifedha.

Source: MwananchiDigital
Mbona hawa nao ni wawekezaji kama wale wa Dubai, wangewapa sapoti badala ya kuwakamata.
 
Sahihi kabisa, Kuna videos U- tubes zinaonesha hadi baadhi ya viongozi wa serikali wakiwahamasisha watu wajiunge , Tena ITV wametangaza
Je jeshi la police walikuwa wapi kuzuia hilo , watu wamejiunga na wanapokea Fidia zao bila shida kama hawakufata utaratib wa BoT tu ila lessen wanazozo za Biashara why wawafungie ili wananchi waasilike , mm nipo Dar Kuna office za LBL kibao na zingine zipo karibu na police jiran kabisa, KUNA MAMBO POLICE WANATUPA UKAKASI .
Wew ni muhanga wa hili jambo
 
Ndo tatizo la viongozi, yaani tatizo linashughulikiwa mwishoni kabisaa,haya ni maajabu ya Karne.
 
Back
Top Bottom