Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kufuatia majukumu ya Jeshi la Polisi kama yalivyoainishwa katika Ibara ya 147 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sura ya 322 ya Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi Katika kifungu cha 5 (1), Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatimiza wajibu wake kuhakikisha Usalama wa raia na mali zao,Kuzuia na kutanzua uhalifu, Kukamata watuhumiwa na kupeleleza, Kusimamia utekelezaji wa sheria na Kudumisha amani na utulivu.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linapenda kuujulisha umma kuhusu muendelezo wa upelelezi wa mgogoro wa ardhi uliotokea tarehe 06.05.2026 majira ya saa 11:10 alfajiri huko Vikawe, Wilaya ya Kibaha na kupelekea majeruhi 15 na mauaji ya watu watatu.
Katika upelelezi huo tarehe 14.05.2026 majira ya saa 10:00 alfajiri Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani lilifanya operesheni ya kuwakamata watu wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika kujeruhi na kusababisha mauaji ya watu watatu ambao walienda kuvunja nyumba zao.
Soma Pia: Kibaha: Wanaodaiwa kuwa ni Polisi wavamia usiku wa manane na kuwakamata wananchi, watatu hawajulikani walipo
Watuhumiwa hao ni :-
Watuhumiwa wote wanashikiliwa kwa mahojiano katika kituo cha Polisi Kibaha.

- Musa Chununu Tembo, Miaka 34, Kuli na Mkazi wa Vikawe
- Walter Elia Urassa, Miaka 33, Fundi ujenzi na Mkazi wa Vikawe
- Jackson Alfa Kilundwa, Miaka 31, Fundi Ujenzi ,Mkazi wa Vikawe
- David Erick Mayengo, Miaka 26,Mkulima na Mkazi wa Vikawe.