Jeshi la Polisi Rukwa lakabidhiwa mbwa 3 kwa ajili ya kukabiliana na uhalifu pamoja na doria

Jeshi la Polisi Rukwa lakabidhiwa mbwa 3 kwa ajili ya kukabiliana na uhalifu pamoja na doria

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wafipa si wakorofi jamaani hadi kuwaletea mbwa ila ukizingua wanakupiga radi ya 200 kwenye jua kali

====================
Katika kuimarisha ulinzi na usalama mkoani Rukwa, Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha Mbwa na Farasi kinakabidhiwa mbwa watatu kwa ajili ya kukabiliana na uhalifu pamoja na doria.

Akizungumza na waandishi wa habari, Inspekta wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Kikosi cha Mbwa na Farasi mkoa wa Rukwa, Chenga Machota, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuboresha mazingira bora ya kufanyia kazi kwa askari nchini.

Ameongeza kuwa mbwa hao wanaenda kuongeza ufanisi kwa Jeshi la Polisi mkoani Rukwa pamoja na kuongeza uwajibikaji katika maeneo ambayo hayakuwa rahisi kufikika.

 
Nje ya mada ni kuwa moja ya somo ambalo mbwa wote duniani awe local, trained, untrained au imported mbwa hakatai kula nyama yenye simu na kufa tu.
 
Mambo mengine siyo hata ya kujadiliwa
 
Back
Top Bottom