Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linawatafuta watu wawili ambao bado majina yao hayajafahamika baada ya kutoroka na kutelekeza boti ambayo ilibeba shehena ya dawa za kulevya aina ya mirungi kutoka nchini Kenya kuja Tanzania kupitia Bahari ya Hindi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Julai 22, 2025 mkoani humo na kueleza kuwa boti hiyo ilikamatwa na Kikosi cha Polisi Wanamaji katika eneo la Mawe Mawili Kijiji cha Kwale, mpakani mwa Wilaya ya Mkinga na Jiji la Tanga usiku wa kuamkia leo
Amesema kuwa watuhumiwa hao wametoroka baada ya kutelekeza boti yao aina ya fibre rangi nyeupe iliyokuwa ikisafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kutoka nchini Kenya kupitia Bahari ya Hindi katika operesheni maalumu iliyofanywa na jeshi hilo katika kuthibiti madawa ya kulevya
Kamanda Mchunguzi ameongeza kuwa watuhumiwa hao wawili waliokuwa kwenye boti walifanikiwa kutoroka baada ya kufika karibu na fukwe, lakini boti pamoja na shehena ya mirungi vilikamatwa na vipo chini ya ulinzi wa polisi
Amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga litaendelea kuimarisha doria na operesheni maalumu hususani katika maeneo ya baharini ambayo yamekuwa yakitumiwa na wahalifu kuvusha bidhaa haramu kutoka nchi jirani ikiwemo madawa ya kulevya
Chanzo: Mwananchi_official