Jeshi la Polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo
Kama wana umoja wao hao wafanyabiashara wa kkoo wasijichangishe?

Kwani serikali si kila bajeti huwa wanatenga fungu kwa ajili ya mfuko wa maafa sasa wanachangisha nini tena hela zilizotengwa ziko wapi mpk waanze kuwaonea wivu wengine wanaochangisha?

Mambo mengine ni aibu sana hasa yanapotendwa na kiongozi mkubwa hivyo
Kule Bukoba watu walichanga halafu serikali ikasepa nazo kwingine
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amesema hakuna mtu yeyote ambaye anaruhusiwa kuchangisha fedha kufuatia tukio la ajali ya kupomoka kwa grorofa la Kariakoo.

Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuzungumza katika eneo hilo akasema JENIFER JOVIN maarufu Niffer atafutwe ili aeleze nani ambaye alimpa mamlaka ya kuchangisha fedha kufuatia tukio hilo kwa sababu Serikali ina utaribu wake katika mafaa kama haya.

Pia, Soma: Maafa Kariakoo: Usichangishe fedha tumia akaunti ya Serikali

Aidha baada ya agizo hilo majibu yakatolewa eneo la Kariakoo wakati Waziri Mkuu anazungumza kwamba Mfanyabiashara Niffer ameshapatikana.
Interesting 🧐.....kama Serikali ina utaratibu wake katika maafa kama haya ya jengo kuporomoka Kariakoo, ina maana walioanza kuchangishana maji ile siku ya kwanza nao wakamatwe kwa kuwa hairuhusiwi?
Vipi vijana wasio kuwa na taaluma ya uokozi waliojitolea kuingia kwenye kifusi kutoa wale walioonekana kuhitaji msaada ile siku ya kwanza, nao watafutwe kwa kuwa hairusiwi?
Hizi siasa nadhani zina ukakasi kwa hakika 😡
 
Ujue serikali hii, unaona kabisa kuna watu ni zero brain, mtu akitumia umaarufu wake kuraise michango kuna shida gani, mie huyo niffer simjui, lakini mfano kama mwakinyo, akiraise michango kuna watu watapata msukumo sababu ya mwakinyo, kuna fans wa Diamond, simba sc ama yanga sc wakianzisha kuna watu watavutika kuchanga sababu ya simba ama yanga.

Huenda kukawa kuna kaupigaji kweli, mie sikatai mjini kila mtu anaweza tumia matatizo kama fursa, lakini jinsi walivyochukua hatua sio vizuri, kesho kutwa litatokea janga, mtu maarufu akaogopa kulivalia njuga.
Kati ya huyo binti niffer na serikali nani wa kwanza kuweka utaratibu wa kuchangia.
Kama ni huyo binti serikali ilikuwa wapi kutoa muongozo?
Watu kama wewe mnaenda jela kipuuzi sana. Unadhani kutojua sheria ndo kinga ya kutohukumiwa?
 
#UPDATES Wakati zoezi la kutoa misaada mbalimbali likiendelea Kariakoo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, na Uratibu. Dkt. Jim James Yonazi amewataka wananchi kuwa makini kuhusu michango inayoendeshwa ya kuwasaidia wahanga ambapo ameweka wazi kuwa akaunti inayokusanya michango ya fedha ni moja pekee na sio nyingine.

Dkt. Jim James amesema michango yote inayohusu tukio hilo inakwenda kwenye akaunti maalum ambayo ni ya serikali #EastAfricaTV
 
Yule Shangazi anaonesha wivu wa wazi kabisa kwa yule mtoto...
Siku zinavyokwenda anashindwa kuzuia wivu wake..
Riziki mwanzo wa chuki dear
Niffah ameonesha uwezo mkubwa wa beuty with brain ile division 1.7 yake ya halali,anajipambania mnoo
Hata kama anadanga ila anadanga kwa akili hawa wengine wameshtuka uzeeni ndo maana wanamchukia mnoo niffer amechelewa kuja mjini ila kawazidi parefuuu kiujanja
 
Viherehere kwenye mitandao sio kitu kizuri.

Hata hivyo hatua zimechelewa kuchukuliwa. Sijui jeshi letu ni wazee sana wamejazana huko hadi wanashindwa ku ‘catch up’ na mambo ya kwenye mitandao upesi?

Mtu ameshakusanya mamilioni ya pesa tokea jana na alitangaza kila hatua wao walikuwa wapi?
Kila kitu wanaitaji wapewe Maelelkezo!! Sio Watu wakujiongeza kama jeshi la Polisi
 
Halafu wewe hadi nimemiss umbea, sijui lini nichape kauzi tupeane ubuyu?
Watu wanatafuta umaarufu ili wapate masponsa wenye hela zao, tako kubwa bila sponsa ni hasara 🤣. Wengine wanatafuta umaarufu ili wapate ubunge mwakani 2025. Wengine wanataka umaarufu ili mwakani wapate tenda za kampeni kwenye uchaguzi 🤣🤣
 
Back
Top Bottom