Una IQ ndogo sana. Alichofanya ni utapeli na utakatishaji pesa.
 
Umoja wa wafanya biashara hawana Magroup yao? hawana Account za vikundi? mpaka kwenye mitandao ya kijamii??
 
Kwani kuna shida gani mfano kama nifa ana mjomba na binamu wake wa Mikese huko na ni wahanga wa tukio la gorofa na wako hospital na uwezo wa kuwahudumia familia hawana kwahiyo nifa ameenda mtandaoni kuomba msaada wasamalia wema wamsaidie kuuguza ndugu zake .
Hapo amekanyagaje waya??
Nauliza tu wajemeni?
 
Mchi inaviingozi wa hovyo sana kiongozi haiwezekani atoe amri eti mkamateni huyo halafu ndio uchunguzi ufanyike ili kujua nani amempa kibali.
Ilitakiwa aagize jeshi lichunguze kwanza na likigundua kuna makosa ndio akamatwe.
Hii inanikumbusha PM Lowasa (Mungu aendelee kumpumzisha alipojichaguli)
Lilipoanguka ghorofa la changombe village keko mwaka 2006
Alipofika eneo la tukio lowasa alipiga sana mkwara halafu akauliza Injinia wa manispaa kama yupo.
Wakati jengo linaangu Injinia wa manispaa kulikuwa hakuna na kwa wakati huo kulikuwa na uhaba sana wa mainjinia huko kwenye halmashauri.
Brother angu Ayub ndio alikuwa ameajiriwa na amepangiwa manispaa ya temeke hana muda mrefu.
Hilo jengo la changombe village lilijengwa na kukamilika wakati huyo injinia ayubu bado hajaajiriwa temeke.
Kwa hiyo Marehemu Lowasa alivyouliza Injinia wa Manispaa yupo wapi Injinia Ayub akajitokeza akasema nipo hapa PM.
Marehemu Lowasa alivyomuana akatoa maelekezo kwa RPC Injinia Ayubu awekwe ndani kwani amekuwa mzembe na kusababisha jengo kuanguka.
Jamaa akakamatwa akawekwa ndani gerezani keko Miezi 6 ndipo upelelezi ukakamilika ikaonekana Injinia Ayub Bahati hausiki na utoaji wa kibali wa ujenzi wa hilo ghorofa kwani aliajiriwa wakati jengo limeshajengwa ndipo akajakuachiwa na kuendelea na ajira yake.
Embu angalie Marehemu Lowasa alivyomkerehesha huyo Injinia Ayubu kwa maagizo yake tu yasiyo na busara na yakukurupuka.
Viongozi wanatakiwa wajiepushe kutoa maagizo ya WEKA NDANI HUYO, KAMATA HUYO badala yake watoe maagizo ya kufanyika uchunguzi kwanza kabla ya kukamata na kuweka ndani.
Unamkamata mtu ,unakuja kufanya uchunguzi inagundulika aliyekamatwa hana hatia inasikitisha sana
 
 
We unaambiwa PM katoa maagizo unaleta mambo ya wakili.
Kwani PM ni Sheria au Mahakama? Ikijulikana kwamba Wana Umoja wao wa wafanyabishara kama social group ulizo nazo kwenye whatsap za kusaidiana wakati wa shida na Raha na wamekubaliana hivyo,? Utakuja kujibu nini
 
When the rule of law is only on papers
 
Dada apewe maua yake inaonyesha ni jinsi gani jamii ya wafanyabiashara wenzie wanavyo muamini sana angekuwa haaminiki asingeweza kukusanya pesa nyingi namna hiyo kwa muda mfupi wanao mfahamu angekuwa haaminiki hata elfu kumi asinge pata na kwa kiasi kikubwa walio changa ni wafanyabiashara wenzie wanao mfahamu
 

Kuna matapeli wengi sana nchi. na wamevamia fani.
 
Huyo Niffer kafanywa Tu kama mbuzi WA kafara ili ku divert mjadala
 
Hakuna haja ya kutoa muongozo sheria ipo. Ukitaka kuchangisha pesa kutoka kwa umma ni lazima uwe na kibali.
 
Hakuna kitu kinaitwa kudanga kwa akili dhambi ni dhambi tu na ni chukizo kwa Mungu
 
Aibu kubwa sana Hilo lilikuwa la caharamila hata yeye ni basi tu kazi ya police hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…