Pre GE2025 Jeshi la Polisi: Tumemkamata Dkt. Slaa, tunamhoji na kuangalia mifumo ya Sheria inatuelekeza nini cha kufanya

Pre GE2025 Jeshi la Polisi: Tumemkamata Dkt. Slaa, tunamhoji na kuangalia mifumo ya Sheria inatuelekeza nini cha kufanya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Saa chache baada ya kutolewa taarifa ya kukamatwa kwa mwanasiasa mkongwe, Dk Willibrod Slaa, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia kwa mahojiano.

Taarifa ya kukamatwa kwa Dk Slaa imesambaa kupitia mitandao ya kijamii, ikisikika sauti ya mwanasiasa huyo akizungumza kuhusu kukamatwa na Jeshi la Polisi akieleza anapelekwa kituo cha Mbweni, Dar es Salaam.

“Nawajulisha tu kwamba kuna polisi wamenifuata, nitawajulisha kitakachotokea. Napelekwa Mbweni kituoni,” alisikika Dk Slaa katika sauti inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Zaidi soma Dkt. Slaa akamatwa usiku huu nyumbani kwake Mbweni

Alipozungumza na Kituo cha Redio cha Wasafi FM leo Januari 10, 2025 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amethibitisha kukamatwa na kushikiliwa Dk Slaa kwa mahojiano.

“Ni sahihi daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na mahojiano yetu yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza nini cha kufanya naamini taarifa zaidi zitatolewa baadaye,” amesema.

Pia soma - Balozi Dkt. Wilbroad Slaa afichua siri mpya ya mikakati ya Mbowe kushinda uenyekiti. Apewa mapesa zaidi na Rais Samia na M/kiti CCM kummaliza Lissu..

Bila shaka Ile michadema uchwara itakuwa inashangilia
 
Kwa nini wasiangalie kwanza hiyo mifumo ya sheria kabla hawajamkamata pana watu ni kutafuta Kiki tu kwani huyo Slaa akipigiwa simu aende kituo cha polisi kuhojiwa atakataa au kwa kuwa mafuta wanazoa bure ndio maana wanaona watumie tu huku Nchi ikiendelea kutangaza misaada ya mabilioni kila kukicha..
 
Tahadhari ya usalama wa Dkt. Slaa ni muhimu wakati huu wasije waka Mben Saanane.
Damu za watu hawa siku zikinena hapo Ikulu hapatakalika.
ikulu gani?
muulizeni m/kiti wenu wa kudumu mboye
kawafanya nini kina saanane
sio kusingizia wasiohusika
 
Tàtizo àkili yako inafikiri kila mtu mzee àmezaliwa kucheza na wajukuu. Hayo ni ya ukoo wenu acha Dr. Slaa acheze na haki za raia siyo acheze na wajukuu.
Hata kama ni wajukuu,majukumu mengine lazima yafanyike.
 
Kiusalama ni lazima ahojiwe. Mbaya zaidi alisemea Clubhouse ambamo watu wa usalama wa taifa lazima wamo. Na wanaweza kukurekodi kirahisi tu. Amejitakia mwenyewe
Iko public na amekua akitaja sana usalama

Sasa athibitishe
 
Kwa nini wasijipange kwanza ndio wamkamate?
Na je, walimuita kwa njia ya kawaida akakaidi kwenda?.
Jamani polisi badilikeni.
si huwa mnaenda nchi za wenzenu kujifunza?
Huwa mnajifunza kweli?Au kuharibu fedha zetu.
Ndio utawala wa sheria unadakwa kwanza kama mwizi ukisubiriwa ushahidi mahakamani ambako hakimu.pekee ndie hujua akuhukumu kwa kipengele gani?
 
Umesoma kitabu cha Erick kuhusu Ben Saanane kutwangwa risasi za kichwa hapo ikulu na mwandazake?
erick kachanganyikiwa
kwanini neno lake lichukiliwe kama sheria?
ameweka vielelezo vya ushahidi asemayo?
erick akisema leo ni jumatatu tumuamini?
 
Ushakulaga za CCM afu leo badala ya kukaa kwa kutulia wewe ni mwendo wa kubwabwaja kila kukicha - kazi kwako.
 
Saa chache baada ya kutolewa taarifa ya kukamatwa kwa mwanasiasa mkongwe, Dk Willibrod Slaa, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia kwa mahojiano.

Taarifa ya kukamatwa kwa Dk Slaa imesambaa kupitia mitandao ya kijamii, ikisikika sauti ya mwanasiasa huyo akizungumza kuhusu kukamatwa na Jeshi la Polisi akieleza anapelekwa kituo cha Mbweni, Dar es Salaam.

“Nawajulisha tu kwamba kuna polisi wamenifuata, nitawajulisha kitakachotokea. Napelekwa Mbweni kituoni,” alisikika Dk Slaa katika sauti inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Zaidi soma Dkt. Slaa akamatwa usiku huu nyumbani kwake Mbweni

Alipozungumza na Kituo cha Redio cha Wasafi FM leo Januari 10, 2025 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amethibitisha kukamatwa na kushikiliwa Dk Slaa kwa mahojiano.

“Ni sahihi daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na mahojiano yetu yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza nini cha kufanya naamini taarifa zaidi zitatolewa baadaye,” amesema.

Pia soma - Balozi Dkt. Wilbroad Slaa afichua siri mpya ya mikakati ya Mbowe kushinda uenyekiti. Apewa mapesa zaidi na Rais Samia na M/kiti CCM kummaliza Lissu..
Huwa nashangaa sana kuona watu walioishia form four na kupata four ya 27 wanajua sheria kuliko dkt wa sheria

Hii Nchi ina vituko sana aisee ayaa
 
Ndio maana wananchi wanapigwa za uso na kina mwamposa wakisubia miujiza huku wao wakipalilia vitambi tu
Ukiona Nchi vyombo vya Serikali vipo busy na maneno ya kwenye mitandao yaani wanakosa usingizi kwa ajili hiyo jua hao watu wamedumaa sana hakuna kitu kitakachowabadili mpaka wanazikwa..
 
Back
Top Bottom