Jeshi la Polisi: Tunachunguza taarifa za kikundi kukamata madereva Bajaj Mwanza

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Taarifa kwa Umma.webp

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limebaini uwepo wa ujumbe unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii (kama inavyoonekana kwenye picha) ukidai uwepo wa kikundi kinachokamata Bajaji kibabe kwa kigezo cha "Wrong Parking" na kutoza kiasi cha Tsh. 22,000 bila risiti, huku kukiwa na tuhuma kuwa baadhi ya askari Polisi wanashirikiana nao.

Hoja ya Mdau ~ Kuna kikundi Mwanza kinakamata Bajaj kibabe kwa kigezo cha 'wrong parking' kinatoza Sh 22,000 na hakitoi risiti

Jeshi la Polisi linapenda kuutaarifu umma kuwa, taarifa hiyo ipuuzwe kwani haina ukweli wowote. Majukumu ya Jeshi la Polisi yanafahamika kisheria na siyo kazi yake kukamata watu kiholela, kukusanya mapato wala kutoza faini kinyume cha sheria na taratibu zilizowekwa.

Aidha, Jeshi la Polisi linafuatilia kwa karibu na kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kitapeli huku wakilihusisha Jeshi la Polisi ili kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yao.

Tunatoa wito kwa mwananchi ama dereva wa Bajaj yeyote mwenye taarifa sahihi, ushahidi ama aliyekumbana na kadhia hiyo, kufika katika Kituo cha Polisi kilicho karibu yake ili kutoa taarifa zitakazosaidia wahusika kukamatwa.

Pia, Jeshi la Polisi linaendelea kuwahakikishia wananchi kuwa, lipo macho kulinda usalama wao na mali zao na halitamfumbia macho mtu ama kikundi chochote kinachovunja sheria za nchi.

Imetolewa na: -
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mwanza
 
Nchi inaelekea kubaya sana, Polisi wako Bize na CHADEMA kuliko kulinda usalama wa Raia wake, hakika inasikitisha sana
 
Kundi la kukamata bajaji linachunguzwa haraka,ila kundi la mbwa mwitu na tiger weusi mmmhh?
 
Hivi vikundi vikiachiwa vitakuja kushika hatamu
Kila mtu atakuwa anajikusanyia mapato anavyotaka

Ova
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limebaini uwepo wa ujumbe unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii (kama inavyoonekana kwenye picha) ukidai uwepo wa kikundi kinachokamata Bajaji kibabe kwa kigezo cha "Wrong Parking" na kutoza kiasi cha Tsh. 22,000 bila risiti, huku kukiwa na tuhuma kuwa baadhi ya askari Polisi wanashirikiana nao.

Hoja ya Mdau ~ Kuna kikundi Mwanza kinakamata Bajaj kibabe kwa kigezo cha 'wrong parking' kinatoza Sh 22,000 na hakitoi risiti

Jeshi la Polisi linapenda kuutaarifu umma kuwa, taarifa hiyo ipuuzwe kwani haina ukweli wowote. Majukumu ya Jeshi la Polisi yanafahamika kisheria na siyo kazi yake kukamata watu kiholela, kukusanya mapato wala kutoza faini kinyume cha sheria na taratibu zilizowekwa.

Aidha, Jeshi la Polisi linafuatilia kwa karibu na kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kitapeli huku wakilihusisha Jeshi la Polisi ili kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yao.

Tunatoa wito kwa mwananchi ama dereva wa Bajaj yeyote mwenye taarifa sahihi, ushahidi ama aliyekumbana na kadhia hiyo, kufika katika Kituo cha Polisi kilicho karibu yake ili kutoa taarifa zitakazosaidia wahusika kukamatwa.

Pia, Jeshi la Polisi linaendelea kuwahakikishia wananchi kuwa, lipo macho kulinda usalama wao na mali zao na halitamfumbia macho mtu ama kikundi chochote kinachovunja sheria za nchi.

Imetolewa na: -
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mwanza
Bajaji zinakamatwa mbele ya kituo cha polisi (pamba), ndiyo wanakuja na utetezi huu!? Walitakiwa wawajibike tu.
 
Back
Top Bottom