GE2025 Jeshi la Polisi: Tunawahakikishia hakuna tishio lolote la kiusalama kuelekea kesho Oktoba 29

GE2025 Jeshi la Polisi: Tunawahakikishia hakuna tishio lolote la kiusalama kuelekea kesho Oktoba 29

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722


TAARIFA KWA UMMA​

Jeshi la Polisi linaendelea kuwahakikishia kuwa kuna usalama wa kutosha tunapoelekea kesho tarehe 29.10.2025 siku ya kupiga kura, kwani hakuna tishio lolote la kiusalama kama tulivyowahakikishia Oktoba 26, 2025.

Aidha, lingependa kuwa tahadharisha kuwa, kuna kikundi cha watu baada ya kuona wameshindwa kuvuruga amani ya nchi yetu wameunda kikundi cha vijana ambao wanaandaa picha mjongeo na taarifa mbalimbali za matukio yaliyotokea siku za nyuma ambayo yalishashughulikiwa na mengine ya kutunga ili wayasambaze kwenye mitandao ya kijamii yaonekane yametokea kipindi hiki au muda mfupi uliopita.

Mkiona taarifa kama hizo kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vingine vya habari vilivyo andaliwa na watu hao wenye nia ovu na amani ya taifa letu mtambue kuwa, ni za uongo, uzushi na za kutaka kutuchonganisha na kutugombanisha.

Wapo pia walioandaliwa kama ambavyo baadhi wamesha jitokeza kuzungumza na kutoa taarifa zenye tungo tata, zenye kutaka kuleta taharuki. Pia wanakusanya matukio ambayo yalitokea nchi zingine na kuyatengeneza kwa kuyawekea sauti zenye lafudhi ya kiswahili ili yaonekane yametokea nchini mwetu na wakati huu muhimu tunapoelekea kupiga kura kesho.

Pia, wamepanga kuchukuwa picha za baadhi ya viongozi na kuziwekea maneno na sauti zenye matamko ya upotoshaji ili ionekane wao ndiyo wanayazungumza au wanayatamka wakati si kweli.

Jeshi la Polisi wakati linaendelea kuwafuatilia ili wawatie nguvuni kwa mujibu wa sheria, linatoa rai kwa wananchi mtakapo ona au kutumiwa picha mjongeo na taarifa kama hizo au vipeperushi na mengine yanayofanana na hayo myapuuze kwani yameandaliwa kwa nia ovu ya kihalifu kwa lengo la kutaka kuleta taharuki kwa wananchi.

Aidha, mkitumiwa taarifa kama hizo msisambaze kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria ya makosa ya kimtandao badala yake mzifute. Mkumbuke taarifa sahihi zinazohusu jambo lolote zitatolewa na mamlaka zenye wajibu wa kufanya hivyo.

Imetolewa na:
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania​


IMG_8559.JPG

IMG_8560.JPG
 

​

TAARIFA KWA UMMA​

Jeshi la Polisi linaendelea kuwahakikishia kuwa kuna usalama wa kutosha tunapoelekea kesho tarehe 29.10.2025 siku ya kupiga kura, kwani hakuna tishio lolote la kiusalama kama tulivyowahakikishia Oktoba 26, 2025.

Aidha, linge pendakuwatahadharisha kuwa, kuna vikundi vya watu baada ya kuona wameshindwa kuvuruga amani ya nchi yetu wameunda kikundi cha vijana ambao wanaandaa picha mjongeo na taarifa mbalimbali za matukio yaliyotokea siku za nyuma ambazo zilishashughulikiwa, na nyingine wakitunga ili wazisambaze kwenye mitandao ya kijamii zionekane zimetokea kipindi hiki au muda mfupi uliopita.

Mkiiona taarifa kama hizo kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vingine vya habari vilivyoandaliwa na watu hao wenye nia ovu na amani ya taifa letu, mtambue kuwa ni za uongo, uzushi na zenye nia ya kutuchonganisha na kutugombanisha.

Wapo pia walioandaliwa kama ambavyo baadhi wameshajitokeza kuzungumza na kutoa taarifa zenye tungo tata, zenye kutaka kuleta taharuki. Pia wanakusanya matukio ambayo yalitokea nchi zingine na kuyatengeneza kwa kuyawekea sauti zenye lafudhi ya Kiswahili ili yaonekane yametokea nchini mwetu na wakati huu muhimu tunapoelekea kupiga kura kesho.

Pia, wamepanga kuchukua picha za baadhi ya viongozi na kuziweka maneno au sauti zenye matamko ya upotoshaji ili ionekane wao ndiyo wanayazungumza au wanayatamka wakati si kweli.

Jeshi la Polisi watakieni watanzania wote uchaguzi wenye utulivu, amani na upendo, likiwahakikishia kuwa limejipanga kwa nguvu kubwa kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo katika maeneo yote nchini.

1761646628063.png


1761646666342.png
 

Attachments

  • MWANZA- KADA wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM), Paul Makonda amesema licha ya uwepo wa watu wanaolit.mp4
    3.6 MB
Jeshi la Polisi nchini limesema hali ya usalama inaendelea kuwa shwari kote nchini kuelekea siku ya kupiga kura kesho, Oktoba 29, 2025, huku likitoa tahadhari dhidi ya taarifa za uongo na uchochezi zinazosambazwa mitandaoni.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, David Misime, akizungumza leo Jumanne, Oktoba 28, 2025 jijini Dodoma amesema jeshi hilo limejipanga kuhakikisha wananchi wote wanapiga kura katika mazingira ya amani na utulivu, likifuatilia kwa karibu mitandao ya kijamii ili kudhibiti taarifa potofu.

Soma pia: Msemaji wa Polisi David Misime: Hatutawavumilia waliojipanga kuvuruga amani wakati wa uchaguzi mkuu 2025



Amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitengeneza picha, video na taarifa bandia kuhusu matukio yanayodaiwa kutokea nchini, ili kuonesha kana kwamba ni halisi na kuleta taharuki kwa wananchi.

“Wananchi wanapaswa kuwa makini na taarifa wanazoziona mitandaoni. Zingine ni za uongo na zenye nia ovu ya kuvuruga amani,” amesema Misime.

Jeshi hilo limewahimiza wananchi kutozisambaza taarifa hizo, na badala yake kusubiri taarifa rasmi kutoka mamlaka husika, likisisitiza kuwa lipo tayari kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na usalama kote nchini.
 
Hiyo kauli ya mwisho "KURA YAKO HAKI YAKO JITOKEZE " inahusiana vipi na kazi za kipolisi?

Polisi wanakumbusha/kuhamasisha watu kwa kutumia mwongozo gani??

Polisi sio chama cha siasa hivyo hakipaswi kujiendesha kisiasa waache wanasiasa ndio wajadili mambo ya kwenda au kutokwenda kupiga kura.
 
Back
Top Bottom