Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Jeshi la Polisi Zanzibar limewatahadharisha na kuwaonya baadhi ya viongozi wa siasa kuacha kutumia uhuru wa kujieleza kwa kutoa kauli za kebeghi kwa viongozi jambo ambalo linaingilia faragha ya mtu na kuhatarisha uvunjifu wa amani visiwani Zanzibar
Kamishna wa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad ametoa onyo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ziwani Mjini Unguja
CP. Hamad amesema kushamiri kwa kauli hizo kwa viongozi wa siasa kunapelekea kuvunja sheria za nchi na uvunjifu wa amani hivyo Jeshi la Polisi halitosita kumchukulia hatua mtu yoyote atakayefanya makosa hayo.
Soma Pia: Dk. Nchimbi: Wana CCM na Wanasiasa wa Vyama vingine tuchunge ndimi zetu
Aidha amesema tayari Jeshi hilo limeshaanza kuchukua hatua huku akisisitiza kuwa wameshaandaa jopo la wataalamu wa kisheria ili kupitia video zote za mikutano ya kisiasa yanayofanyika ili kubaini kama kuna ukiukwaji wowote wa kisheria.