John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
1. Baada ya kuibuka kwa sakata la Kuwapa Uraia kiholela Wachezaji mpira wa Kigeni waliosajiliwa na timu ya Soka ya Singida United, Idara ya Uhamiaji walitoa taarifa yao ambayo wanadai kuwa inalenga kutoa ufafanuzi kuhusiana na suala hili. Taarifa husika imeambatishwa hapa kwenye uzi huu.
2. Kwenye taarifa yao hiyo, Uhamiaji wamenukuu Kifungu Na, 9 & 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357 ambavyo wanadai kwamba ndivyo vilivyotumika katika kuwaongoza Kuwapa Uraia hao Wachezaji wa Kigeni.
Nakala ya hiyo Sheria waliyonukuu kwenye taarifa yao pia nimeambatisha hapa kwenye uzi huu.
3. Ukisoma hiyo taarifa yao, Uhamiaji wanakiri kwamba wao ndio wamehusika katika mchakato wa Kuwapa Uraia hao Wachezaji wa Kigeni, na Taratibu zilifuatwa.
4. Mimi binafsi baada ya kusoma hiyo taarifa yao pamoja na hiyo Sheria ya Uraia waliyonukuu, naona kama kuna uvunjaji wa makusudi na wa wazi wazi kabisa wa hiyo Sheria.
5. Kwa kuwa, Idara ya Uhamiaji wamekiri kwamba utaratibu wa kisheria ullifuatwa kuhusiana na suala hili la Kuwapa Uraia hao Wachezaji wa Kigeni, hivyo Basi, ningependa Idara ya Uhamiaji ijibu Hoja hizi zifuatazo:-
5.1 Kwa kuwa Sheria hiyo ya Uraia inatamka Wazi kwamba kabla Raia wa Kigeni (Mwombaji wa uraia) hajapatiwa Uraia wa Tanzania, Mwombaji huyo anatakiwa awe ameishi ndani ya nchi hii kwa muda wa angalau minimum miaka saba (7).
Je, hao Wachezaji wa Kigeni waliingia hapa nchini Tanzania lini ili kuishi hapa na ili kutimiza hiyo miaka saba inayotakiwa Kisheria? Lini hasa (tarehe ngapi) ilikuwa siku ya hao Wachezaji waliyotimiza kipindi Cha kuishi hiyo miaka saba wakiwa Wakaazi hapa Tanzania?
Ufafanuzi wa kina kabisa unahitajika kwenye Hoja hizi kwa sababu Uhamiaji ndiyo Taasisi yenye Mamlaka yote kabisa ya kutunza kumbukumbu zote kabisa za Wageni au Wasafiri wote wa Kimataifa ambao wanaoingia na kutoka hapa nchini.
5.2 Tumekuwa tukiona Matangazo kwenye Magazeti mbalimbali yanayowahusu Raia wa Kigeni ambao wenye nia ya Kuomba Uraia wa Tanzania, Matangazo hayo yamekuwa yakiutaarifu umma wa waTanzania kuwasilisha Mapingamizi yao (endapo kama wanayo) dhidi ya hao Watu wanaoomba Uraia wa Tanzania.
Uhamiaji wanapaswa watueleze, Je, lini hasa hao Wachezaji wa Kigeni waliopatiwa uraia wa Tanzania walitoa Matangazo hayo ili kuutaarifu umma juu ya hilo suala lao la kuomba uraia wa nchi hii? Je, Matangazo hayo yalitolewa lini na yalitolewa kwenye Magazeti gani hasa ya hapa Tanzania?
6. Mwisho
Mimi binafsi sipingi hata kidogo Raia wa Kigeni kupatiwa uraia wa Tanzania, lakini pia sikubaliani hata kidogo na suala la Kutoa Uraia kwa Raia wa Kigeni kwa njia za kiholela. Kwa sababu kufanya hivyo ni jambo baya na la hatari sana kwa Usalama wa Umma na hata Usalama wa mtu mmoja mmoja ukiwa ndani ya nchi hii au ukiwa nje ya nchi.