Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) latoa ufafanuzi kuhusu yanayoendelea mtandaoni

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) latoa ufafanuzi kuhusu yanayoendelea mtandaoni

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Zingatia: "Hoja hizo zinatolewa na watu waliopo mazingira ya kijeshi"


​

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari​

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linautaarifu umma wa Watanzania kuwa kumejitokeza baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuweka maudhui yanayochochea kuingiza Jeshi katika mambo ya siasa.

Aidha, baadhi ya hoja hizo zinatolewa na watu waliopo katika mazingira ya kijeshi, kujinasibisha na Jeshi, walioachishwa Jeshi kwa tabia na mwenendo mbaya pamoja na kujihusisha na siasa na uanaharakati.

Kwa mantiki hiyo, JWTZ linapenda kuutaarifu Umma wa Watanzania kuwa linaendelea kutekeleza majukumu yake kikatiba kwa uaminifu, utiii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chetu.
-490428889.jpg
Pia Soma: Mwanajeshi, Kapteni Tesha ajitoa muhanga kuongea hatari ya Taifa linapoelekea
 
Washamaliza kila kitu maana hawajakanusha wala kumkataa Tesha kuwa sio mwanajeshi wala kukanusha kuwa tesha hawajamtuma na wala hajashikiliwa na MP kwa mahojiano zaidi

Kwahy kicheko kiko mbioni kuja. Soon tutakuwa na katiba huru
 
Back
Top Bottom