Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) latoa ufafanuzi kuhusu yanayoendelea mtandaoni

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) latoa ufafanuzi kuhusu yanayoendelea mtandaoni

Nishasema kwenye hili hamuwezi kuja na excuse yeyote itayofanya nimuone captain ni muongo

Huyo msemaji wa JWTZ ni Msigwa wa Jeshini ni ass kisser tu wala siwezi kumuamini.

Na nilisema majarabio yeyote watayofanya kutaka kuwaaminisha watu kuwa hali ni shwari na kwamba jeshi linaunga mkono serikali basi matokeo yake hayawezi kuwa mazuri kwao.

Walianza kusema ni AI na saizi wanakuja kusema ni wanajeshi waliofukuzwa.

Tutaona
 
Wakuuuu
Amkeni

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari​


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linautaarifu umma wa Watanzania kuwa kumejitokeza baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuweka maudhui yanayochochea kuingiza Jeshi katika mambo ya siasa.

Aidha, baadhi ya hoja hizo zinatolewa na watu waliopo katika mazingira ya kijeshi, kujinasibisha na Jeshi, walioachishwa Jeshi kwa tabia na mwenendo mbaya pamoja na kujihusisha na siasa na uanaharakati.

Kwa mantiki hiyo, JWTZ linapenda kuutaarifu Umma wa Watanzania kuwa linaendelea kutekeleza majukumu yake kikatiba kwa uaminifu, utiii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chetu.
Hmm…..things that make you go hmmm🤔

I didn’t hear an outright denial or acknowledgement of so called Captain Tesha.
 
Ndugu zangu Watanzania,

VIDEO:

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeutaarifu umma kuwa limebaini uwepo wa baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kusambaza maudhui yenye lengo la kulihusisha Jeshi na mambo ya siasa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 4, 2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Bernard Masala Mlunga, baadhi ya watu hao wanajitambulisha kwa jina la Jeshi licha ya kuachishwa kutokana na tabia na mwenendo usiofaa, huku wengine wakijihusisha na siasa na uanaharakati.

Jeshi limesisitiza kuwa halitishiki na majaribio hayo na litaendelea kulinda amani, uhuru na mipaka ya Taifa kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na misingi ya uadilifu wake.
Screenshot_20251004-212828_1.jpg
 
Back
Top Bottom