Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) latoa ufafanuzi kuhusu yanayoendelea mtandaoni

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) latoa ufafanuzi kuhusu yanayoendelea mtandaoni

Zingatia: Kiufupi ni kwamba hakuna sehemu barua imesema kuwa Kaptein Tesha siyo Mwanajeshi

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari​

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linautaarifu umma wa Watanzania kuwa kumejitokeza baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuweka maudhui yanayochochea kuingiza Jeshi katika mambo ya siasa.

Aidha, baadhi ya hoja hizo zinatolewa na watu waliopo katika mazingira ya kijeshi, kujinasibisha na Jeshi, walioachishwa Jeshi kwa tabia na mwenendo mbaya pamoja na kujihusisha na siasa na uanaharakati.

Kwa mantiki hiyo, JWTZ linapenda kuutaarifu Umma wa Watanzania kuwa linaendelea kutekeleza majukumu yake kikatiba kwa uaminifu, utiii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chetu.
Huyu mwamba si alikuaga mpambe wa Jiwe? Imekuwaje yeye sasa hivi ni afisa habari la jeshi letu? Hii imekaaje asee kiitifaki. Au wameona wakimtumia italeta uzito flani hiv.
 
Ukweli utabaki pale pale kuwa wapiganaji ambao no wengi kuliko senior officers wanawaunga mkono wananchi. Mtu kama huyu Bernard Mlunga ambaye alikuwa ADC wa Magufuli amekwisha compromise na wanamtandao hawezi akabadilisha mindset ya maelfu wa wapiganaji wa JWTZ.
Ndio ukweli huo..
Hawa high ranking officers ambao ni wanufaika , watajikuta peke yao.
 
Back
Top Bottom