Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) latoa ufafanuzi kuhusu yanayoendelea mtandaoni

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) latoa ufafanuzi kuhusu yanayoendelea mtandaoni

Washamaliza kila kitu hawaja kanusha wala kumkataa tesha kuwa sio mwanajeshi wala kukanusha kuwa tesha hawaja mtuma na wala haja shikiliwa na MP kwa mahojiano zaidi kwahy kicheko kiko mbioni kuja soon tutakuwa na katiba huru elewa kauli yao ya mwisho lina endelea kutimiza majukumj yao ya kikatiba
Wala hata MP hashughuliki na huyu Captain wa Jeshi La Anga, MP ni kwa wanajeshi wa nchi KAVU, nakupa hii huyu mkuu wake wa kumshughulikia anaitwa Air Police, Security Police au Security Forces ndiyo wanahusika na hawa wanajeshi wa Anga endapo ikibainika ka MESS UP na taratibu zao.. Angekua ni mwanajeshi wa majini kuna Masters-At-Arms au Shore Patrol ndiyo mkuu wao wa nidhamu..
 
Kilicho andikwa kwenye hiyo barua ni kichekesho cha Karne
Tesha kaongea mambo mazito sana, ni hekima imesaidia kuyajibu vinginevyo; maji huwa mafuta ukizima moto.
Tuhuma za kuuliwa rais na wahuni kuchukua nchi..>.....
sasa hv kuna uchunguzi wa kijeshi kisiri siri ndio hiyo barua ilivoonyesha, ndio mana hawajamkana Tesha, wanafuata katiBa
 
CPt Tesha hajafukuzwa jeshini. Huwezi kufukuzwa au kuachishwa jeshini ukabaki na uniform. Hii ni ujanja kama ujanja mwingine tu. Kama ana akili mama mwambieni akae kando hali ni mbaya mno . Jeshini Kuna mpasuko.
Are you saying, it's all over !!!?
 
Zingatia: "Hoja hizo zinatolewa na watu waliopo mazingira ya kijeshi"

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari​

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linautaarifu umma wa Watanzania kuwa kumejitokeza baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuweka maudhui yanayochochea kuingiza Jeshi katika mambo ya siasa.

Aidha, baadhi ya hoja hizo zinatolewa na watu waliopo katika mazingira ya kijeshi, kujinasibisha na Jeshi, walioachishwa Jeshi kwa tabia na mwenendo mbaya pamoja na kujihusisha na siasa na uanaharakati.

Kwa mantiki hiyo, JWTZ linapenda kuutaarifu Umma wa Watanzania kuwa linaendelea kutekeleza majukumu yake kikatiba kwa uaminifu, utiii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chetu.
Pia Soma: Mwanajeshi, Kapteni Tesha ajitoa muhanga kuongea hatari ya Taifa linapoelekea

Well and good Jeshi limesema. Lakini waangalie pia watu wamepokeaje msg ya Captain Tesha.
 
Ufafanuzi akili yangu imegoma kuuelewa.. Watu wanaochukua nchi au kufanya mapinduzi miaka yote ni makapteni.. Sio mageneral wala macoloneli..

Makapteni nawaheshimu sana.
 
Ni aibu sana kwa Samia kuifikisha nchi huku. Hatukuwahi kufikiria tutafikia kwenye haya mambo ya jeshi. Aibu zao wote wana mtandao. Sasa Bi Mkubwa si aachie kiti tu, kwa nini anatung’ang’ania? Yani hafikirii mpaka tunafika huku ni kwa sababu yake!! Nchi imemshinda jamani. Wenye kuweza kuokoa yanayokuja kulitia doa taifa waokoe, ila tunakokwenda siko.
Wana mtandao bado wanamtia ujasiri kuwa watamlinda dhidi ya hatari yoyote itakayotokea mbeleni..

Ngoja tuone mpaka mwisho.
 
Kwanini mnaenda kukimbia mchaka mchaka kama njia ya kutishia watu?
Wanapaswa kujibu hili swali.
Lakini pia inawezekana kukawa na mamluki miongoni mwao wanaotumiwa kisiasa

Tutaangalia kama watafanya mazoezi kama hayo tena baada ya Capt. Tesha kutoa tamko.
 
Back
Top Bottom