Jeshi letu lijifunze kutokana na vita ya Ukraine na sasa huko Israel/Hamas

Jeshi letu lijifunze kutokana na vita ya Ukraine na sasa huko Israel/Hamas

Nakubaliana nawe 100%. Ukiwaona Ijumaa wanapokimbia mchakamchaka utashangaa kama unaowaona kweli ni askari wanaoweza kupigana vita.

Their only area of competence is at harassing innocent civilians.
Jeshi letu bado nidhamu yake hairidhishi.
Sio wabunifu.
Wananenepeana tu.
Ni aibu pia ufisadi kutajwa jeshini.

Kwa ujumla jwtz yetu ni polisi iliyochangamka.

Ninaongea kwa uxoefu...mengine niishie hapa tu....hatujawekeza jeshini.

Mkapa ndiye alianza kuja vizuri basi tu
 
Ni kweli! Nadhani Jeshi letu liko vizuri tu, maana kama linashika namba 6 duniani kwa ubora, ni swala la kuwekeza tu katika Technology ya zana za kivita.
Lakini hata hivyo bajeti ni changamoto, na sijui Serikali inatenga kiasi gani kila mwaka katika bajeti kwa ajili ya Wizara ya Ulinzi!
Fuatilia bunge la bajeti, kila mwaka wizarabya ulinzi na wizara zingine zote husoma kiasi tengwa kwa ajili ya wizara zao. Pia unaweza ipata bajeti hiyo ukipitia kwenye website yao.
 
Katika vitu ambavyo huwa napenda sana ni kuimarisha jeshi letu.

Nina hamu sana tununue ndege vita mpya , meli za kivita na silaha nyingine za kutosha.

I always pray tuwe na jeshi imara.
 
Tufanye yote ila mambo ya kuomba vita hapana ,acha askari wanenepeane tu ,mana si wao peke yao wanao nenepa,
Nchi yetu imejaa mambo ya ajabu ajabu sana.
 
Kati ya taasisi nyeti ninazoziheshimu na kuzienzi ni jeshi letu la JWTZ, limeonyesha ukomavu wake kwa miaka mingi sana hasa wakati wa vita ya ukombozi.

Ilipoingia 1978, November/December hadi 1979, jeshi lilipitia "baptism of fire" wakati wa Vita ya Kagera.

Kimsingi baada ya vita ile ikadhihirika kuwa Defence Policy iko safi na inafanya kazi katika mazingira ya wakati ule.

Najua leo jeshi liko complex kuliko wakati huo na lina vyuo vyake ambavyo ni Think Tanks, kama National Defence College pale Kunduchi.

Sasa leo kuna vita hivi vya Ukraine na vile vile Israel na Hamas. Mbinu zilizojitokeza na kuwa very effective katika kushambulia adui, ni matumzi ya Drones na Missiles.

Huko Ukraine drones zimekuwa a weapon of choice katika ku target sehemu za adui kwa pande zote.

Hamas juzi kwa vifaa ambavyo waweza kufikiri ni vya mchezo mchezo tu, katumia drones ambazo zimechakaza vibaya miuondombinu ya kijeshi ya Israel iliyokuwa mstari wa mbele.

Kwamba wameuawa wanajeshi zaidi ya 300 wa Israel katika mashambulio, hilo na jambo kubwa sana.

Maoni yangu ni; Jeshi letu vile vile litazame upya Defence Policy yake ili matumizi ya vifaa hivi viweze kujumuishwa katika ulinzi wa nchi yetu.

Nawaza tu!
Iran kaondolewa vikwazo vya kuuza siraha na UN so kuhusu drone tuanzie hapa
 
"""Maoni yangu ni; Jeshi letu vile vile litazame upya Defence Policy yake ili matumizi ya vifaa hivi viweze kujumuishwa katika ulinzi wa nchi yetu.
Nawaza tu!"""

Lishatazama...
Au unataka waoneshe hayo matumizi yake..
Au endelea kuwaza hivo hivo
 
Kwanini Israel miaka yote anasaidiwa na America, Uk; France na silaha kubwa zote wanazo. Lkn juzi wametekwa kama anakamatwa kuku ktk kibanda chake? Tujifunze kwamba Allah ni mkubwa sana
Eeehh...yamekuwa ya allah tena....makubwaaa...allah kafikaje tena hapa mjomba aake mwarabu koko wa paresitinaa
 
Tuko vizuri mkuu. Huoni askari wetu mmoja anaweza kuvuta truck ya jeshi kwa kamba na ikatembea ikiwa na dereva ndani.
 
Kwanini Israel miaka yote anasaidiwa na America, Uk; France na silaha kubwa zote wanazo. Lkn juzi wametekwa kama anakamatwa kuku ktk kibanda chake? Tujifunze kwamba Allah ni mkubwa sana
Hamas waliwavizia. Na zaidi waliwavizia na kuwaua raia. Kwa mashambulizi yanayoendelea sasa, kama Hamas wana uwezo wa kupigana, au huyo Allah ndiye anayewapigania, tulistahili kuuona ushindi wa Hamas. Mbona hao hamas wote wamekimbilia mahospitali, misikitini na makanisani, wakijichanganya na raia?

Kwenye kuviziwa, hakuna aliye mjanja. Hafa uwe na ujuzi na silaha za namna gani, mtu akija nyuma yako, ukiwa huna habari, akakutandika na rungu la mpingo kisogoni, lazima utakufa.
 
Ni kweli! Nadhani Jeshi letu liko vizuri tu, maana kama linashika namba 6 duniani kwa ubora, ni swala la kuwekeza tu katika Technology ya zana za kivita.
Lakini hata hivyo bajeti ni changamoto, na sijui Serikali inatenga kiasi gani kila mwaka katika bajeti kwa ajili ya Wizara ya Ulinzi!

Wewe, unaota? Jeshi gani la kwetu linashika namba 6 kwa ubora Duniani? Au unamaanisha namba 60 au 600?
 
Hamas waliwavizia. Na zaidi waliwavizia na kuwaua raia. Kwa mashambulizi yanayoendelea sasa, kama Hamas wana uwezo wa kupigana, au huyo Allah ndiye anayewapigania, tulistahili kuuona ushindi wa Hamas. Mbona hao hamas wote wamekimbilia mahospitali, misikitini na makanisani, wakijichanganya na raia?

Kwenye kuviziwa, hakuna aliye mjanja. Hafa uwe na ujuzi na silaha za namna gani, mtu akija nyuma yako, ukiwa huna habari, akakutandika na rungu la mpingo kisogoni, lazima utakufa.
Tumia akili wewe mjinga. Hamas wamekimbia miskitini na mahospital? Mbona mabwana zako wakisaidiwa na mabeberu wanachungulia kwa mbali na mizinga yao mwezi sasa? Mbona hawaingii Gaza wakaswagwa. Tumia akili usitumie uso kufikiria
 
Back
Top Bottom