Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Tanzania ni nchi ya amani sana. Kama ingekuwa West Africa au America, kw hali ya uozo wa uongozi, ufisadi na kuuzwa rasilimali za nchi jeshi lingekuwa lilishafanya mapinduzi ya kijeshi ili kuilinda nchi isipotee, na viongozi wengi waliokuwa madarakani kupigwa risasi au kufungwa. Lakini sio Tanzania, hilo halitatokea kamwe, sisi ni watu wa amani.Hili suala la jeshi kuamriwa kufanya usafi kila vyama vya upinzani vinapotangaza maandamano halikubaliki.
Wote tunalia hali ngumu ya maisha ikiwemo wanajeshi pamoja na familia zao na viongozi wa serikali wako kimya, halafu wanapotakiwa kufanya kitu walau hata kwa shinikizo la maandamano, wanakimbilia Kuomba wanajeshi wetu wakafagie barabara na kuokota makopo! Kweli jamani?!! Hapana. Hii haikubliki kabisa.
Wanajeshi tumikieni maslahi ya nchi na wananchi wake na wala siyo viongozi wa hovyo wanaotusababishia hali ngumu kutokana na matumizi yao ya anasa huku raia tunaumia.
Jitambueni nyinyi ni watu wa muhimu sana kwa nchi na mnapaswa kuheshimiwa na siyo kutumika.